REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KENYA : UHURU KENYATTA KAFANYA HAYA !!!

8:29:00 AM

Rais Uhuru Kenyata amepunguza kiwango cha wizara serikalini kutoka 44 hadi 18.

Kwenye mabadiliko hayo; afisa ya Rais itakuwa na afisi tendaji ya Rais na afisi tendaji ya Naibu Rais ambapo kutakuwa na wizara mbili ambazo ni Wizara ya Masuala ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Taifa na Wizara ya Ugatuzi na Mipango.

Wizara nyingine ni ile ya Ulinzi, Wizara ya Masuala ya Nje, Wizara ya Elimu, itakayokuwa na idara za elimu na ile ya sayansi na teknolojia, Wizara ya Taifa ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Uchukuzi na 
Miundomisingi, itakayokuwa na idara za huduma za usafiri na ile ya miundomisingi.

Aidha kuna Wizara ya Mazingira, Maji na Maliasili, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Miji, Wizara na Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa, Wizara ya Leba, Huduma za Jamii na Usalama, Wizara ya Kawi na Masuala ya Mafuta, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Wizara ya Biashara na Utalii na Wizara ya Uchimbani Majini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER