REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MBUNGE W#A SINGIDA ATOA ZAWADI KATIKA JIMBO LAKE

11:40:00 PM Add Comment
 
 


Na Nathaniel Limu.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa pea za vitenge 7,500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya sherehe za CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.

Mh. Dewji ametoa msaada huo mkubwa na wa aina yake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na Katibu wa CCM manispaa ya Singida.

Msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi, amesema jumla ya vikundi vya uhamasihaji 112, vimenufaika na msaada huo wa vitenge.

Amesema  pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa halmashauri kuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu, boda boda na taasisi mbali mbali, watanufaika na msaada huo.
Msaidizi huyo wa mbunge, amesema kwa hali hiyo, sherehe hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wana- CCM na wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.

Katika hatua nyingine, Katibu tawi la Ughaugha (CCM), Hamisi Ramadhani, amesema msaada huo wa vitenge, ni mwendelezo wa misaada mingi ya kimaendeleo anayotoa mbunge Dewji, jimboni kwake.
“Kwa kweli mimi binafsi nakiri tu kwamba Dewji anafanya mambo makubwa sana jimboni kwake.  Hivi karibuni ametoa majembe mengi ya kukokotwa na ng’ombe pamoja na tani nyingi za mbegu ya mbaazi, dengu na choroko”,amesema.

Ramadhani amesema msaada huo ambao utamgharimu Dewji zaidi ya shilingi 250 milioni, unalenga kuwanufaisha wakulima watakaojiunga kwenye vikundi kujikomboa kiuchumi.
“Kwa sasa baadhi ya wakazi wa jimbo la Singida mjini wanakabiliwa na upungufu wa chakula.  Hivyo naomba nitumie nafasi hii kumwomba mbunge wetu Dewji asichoke, atusaidie chakula ili tuweze kunusurika na atharii za njaa”,amesema.

Kuhusu msaada wa vitenge, Hamisi amesema msaada huo hauna kabisa harufu ya rushwa, kwa madai kwamba hauna mambo ya kona kona wala kificho.
Naye mhasibu wa kikundi cha kijiji cha Misake, Mwajabu Haji, amesema msaada wa sare hizo, utachochea ari ya kikundi kuongeza bidii katika jukumu lao la uhamasishaji.

GOOD MORNING...

11:25:00 PM Add Comment
Nilikuwa nadhani Mishe kama hizi zipo Bongo tu....kumbe hata Mbele?...Habari za Asubuhi Wapendwa. Ingawa ni siku ya Siku kuu ya MAULID, ndo kwanza kijana wenu nipo ofisini, si unajua tena kazi zetu?

MNADA BANNER