REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SHAKIRA APIGWA STOP KUSHIKWA SHIKWA NA WANAUME KATIKA VIDEO.

6:57:00 AM Add Comment

THIS IS WHAT WE CALL LOVE..na hayo ndiyo yaliyomtokea Shakira.
Iko hivi, Mwanamama anayeheshimika Dunia nzima kwa Viuno na mahips, Shakira, amesema kuwa, byfriend wake hataki ashikwe shikwe na Mwanaume yeyote katika video anazoshiriki.

Kwa mujibu wa maelezo yake katika Jarida la BILLBOARDS, Shakira amekiri kuwa Boyfriend na Mzazi mwenzake ambaye na Msakata Kabumbu katika Club ya BARCELONA, GERALD PIQUE (PIKE), hataki kabisa na wala hayuko tayari Rihana ashiriki katika Video na Mwanaume yeyote ambaye atamshika mshika katika maungo yake ya mwili, kutokana na Wivu alio nao juu yake.


Katika kudhihirisha hilo, Shakira alifunua kuwa, ndio maana katika video yake ya CANT REMEMBER TO FORGERT YOU , amemshirikisha Rihanna na hata kumruhusu amshike kwa sababu ni Mwanamke mwenzake, na PIQUE (PIKE) ambaye ni boyfriend wake hakuwa na tatizo Juu ya hilo, kwa sababu ni Bora ashikwe na mwanamke kuliko Jembe.

Tofauti na hayo, Shakira amesema kuwa kutokana na hali hiyo, Shakira ameona ni vema abadilishe system ya kuwahusisha wanaume wanaomshika katika Video yake yoyote, badala yake atakuwa akiwahusisha wanawake, maana anayaheshimu maamuzi ya Boyfriend wake huyo, nab ado anampenda huku akitamani na kuomba Uhusiano wao uzidi kudumu.


Shakira na Gerald Peque wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka 2011, na Mwaka 2013 walfanikiwa kupata Mtoto wa kiume anayefahamika kwa jina MILAN PIQUE MEBARAK


JAY Z AGOMA KUWA BEST MAN WA KANYE WEST KATIKA NDOA YAKE NA KIM KARDASHIAN

6:32:00 AM Add Comment

TTM Tumenyaka Mtonyo Kuwa RAPPA JAY Z amegoma kuwa  best man wa  Swahiba ake wa karibu, KANYE WEST, katika Ndoa yake na Mchumba wake Kanye West, ambayo inatarajiwa kufungwa hivi karibuni..

Baada ya kupata Mchakato huo, kitengo cha chimbua kilamua kuzama mitandaoni kusaka Full Details, maana ukizingatia Kanye na Jay Z ni marafiki wa karibu, wamewahi kufanya kazi ya pamoja katika Albam yao ya WATCH THE THRONE, pia hawajawahi kugombana.

Baada ya kufuatili kwa ukaribu, TTM tumebaini kuwa, Chanzo cha Jay Z kugoma kuwa Best man wa kanye West , ni kutokutaka kuonekana katika TV Show ya akina Kim kardashian inayofahamika kwa jina la KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS.

Aidha taarifa bado zinaeleza Kuwa, JAY Z hapendi kabisa Kipindi hicho cha Kim kardashian, na wala hayuko tayari kuonekana katika Kipindi hicho.

Pia inasemekana kuwa, baada ya mazungumzo kadhaa yaliyofanyika, JIGGA alikubali kuhudhuria katika Sherehe ya Ndoa hiyo, lakini kwa Sharti la Yeye na familia yake, yaani mkewe Beyonce na Mtoto wao wa miaka Miwili, BLUE IVY, kutokuchukuliwa Video katika Show ya Kim kardashian.

Katika kuongeza hilo, Beyonce pia alikiri kutokukipenda kipindi hicho na hayuko tayari kumuona mumewe na binti yake sanjari nay eye, wakionekana katika Reality Tv Show hiyo.

Kwa upande wao maboss wa ETV ambao ndio warushaji wa kipindi hicho cha Kim kardashian, wamedai kuwa, watatumia Gharama yoyote kuhakikisha kipindi Hicho kinarushwa live, huku wakijitahidi kuangalia watafanya nini ili Jay Z abaki kuwa Bestman wa jay Z


WARWANDA WAMEMMAINDI VIBAYA JOSEE CHAMELEON

6:15:00 AM Add Comment

Ubabe wa Chameleone umeamsha hasira za kumwaga, hasa kwa mashabiki mbali mbali ambao walihudhuria katika tamasha la Dr. Josee Chameleone lililokuwa limeandaliwa huko Nchini Rwanda.

Josee Chameleone ambaye ni moja kati ya wasanii wakali na wakongwe Nchini Uganda na Afrika mashariki Kiujumla, alitia Ngumu Kupiga Show katika jiji la Kigali, baada ya kubaini kuwa Vifaa vilivyokuwa Vimefungwa Kunako Steji Hiyo kwa ajili ya Show yake, Vilikuwa havitoi Sound Nzuri.

Chameleone aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kubaini tatizo hilo ambalo anaamini lingemuangusha sana katika Perfomance yake, na Lawama kubwa akizipeleka kwa Waandaaji wa tamasha Hilo.

Baada ya kufikia Uamuzi huo, wasanii nyota Nchini Rwanda pia, nao walishindwa kupanda Stejin kutokana na Hali ilivyokuwa Mbaya hasa kutoka kwa Nyomi la mashabiki ambao walitia Timu Eneo hilo kumshuhudia Mkali huyo wa TUBONGE akishusha Mbwadidi la Kiburudani.

Kutokana hasira za mashabiki hao, Wengi walisikika wakitamka Kuwa wanataka Pesa yao , pamoja na damu ya Chameleone, hasa kwa kupoteza Muda wao, pamoja na Maandalizi yao ya kuja kumshuhudia akiwa stejini.


Aidha mpaka hivi sasa, Chameleon ambaye ameanza Shughuli zake za Muziki kuanzia Miaka ya 1990, hajaomba Msamaha kutokana na Kitendo hicho ambacho hakika kimewachukiza sana Mashabiki zake Nchini Rwanda

MNADA BANNER