REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MISS TANZANIA HII HAPA TENA

12:14:00 PM Add Comment

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original pamoja na Kamati ya Miss Tanzania, jana wamezindua rasmi shindano hilo sambamba na kuanza kwa mchakato wa kumpata Miss Tanzania 2014/2015.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro, alisema wana furaha kutangaza udhamini wa mashindano ya kumsaka mrembo atakayemrithi Happipess Watimanywa.

“Nina imani wote tunakumbuka kuwa mwaka 2012 Redd’s ilisaini mkataba na Lino International  Agency, ambao ndio wanaoratibu shindano hilo na kuwa wadhamini wakuu wa shindano hili lenye  hadhi yake hapa nchini kwa miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014, hivyo huu ukiwa ndio mwaka wetu wa tatu kwa mujibu wa mkataba, tunayo furaha kubwa kusema kuwa, Redd’s imeweza kutoa mchango wake kwa jamii ya Kitanzania, hususan tasnia hii ya urembo,” alisema Kimaro.

Kimaro aliongeza kuwa, wametenga sh milioni 500 zitakazoendesha shindano hilo katika ngazi zote.

Naye Mkurugenzi wa Lino, Hashim Lundenga, alisema kuwa wao kama waratibu wakuu wana kila sababu ya kuwashukuru Redd’s Original, kwani zaidi ya kuwa mdhamini mkuu kwa miaka mitatu,  kinywaji hicho kimekuwa mdau mkubwa wa mashindano haya kwa miaka mingi.

“Kwa niaba ya Lino na wadau wa tasnia ya urembo, tunawapongeza sana Redd’s Original kwa imani yao kubwa na mashindano haya, ambayo hakika sasa yanavutia zaidi,” alisema Lundenga.

Aliongeza kuwa wana imani kubwa kuwa mwisho wa mkataba huo wa miaka mitatu si mwisho wa uhusiano mzuri kati ya Lino International, wadau wa urembo na kinywaji cha Redd’s Original.

Aidha, Lundenga aliweka wazi ratiba ya mashindano hayo, ambako kuanzia Aprili hadi Mei ni ngazi ya wilaya na Juni itakuwa mikoa kabla ya kusitishwa Julai kuupisha mwezi wa Ramadhani.


Baada ya hapo, mashindano yataendelea Agosti katika ngazi za kanda na shindano la taifa litafanyika Septemba katika tarehe itakayotajwa baadaye.

HIKI NDICHO MSECHU ALICHOKISEMA....

11:21:00 AM Add Comment
 “……mama yake mtoto wangu ,mother house, mother kitambi, mother misosi ,mother manager ,mother kila kitu... since 2002 till now 2014 we still gandana like super glue.... utatudanganya nini..... I love u so much na I wish u happy birthday uzidi nizalia mitoto mizuri mizuri kama lolo nipige hela mimi za posa.... live long live long live long! "

THE RETURN OF JANJARO TO TIP TOP CONNECTION:BABU TALE HANA NOMA NA JANJARO, ILA ANAMTAKA ASEME UKWELI WA MAMBO

10:51:00 AM Add Comment



Baada ya Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia vyombo vya habari uongozi wa Tip Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss wa Tip Top Connection Babu Tale amemiminika kuwa kuwa anataka rapper huyo aseme ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.

“Aongee ukweli tu haina shida, nimemsamehe yeye ni Muislamu mwenzangu tumetumwa tusameheane, mimi nimeshamsamehe ila nimezungukwa na mashabiki ambao wakati yeye ananitukana kuna mashabiki ambao walikuwa upande wangu ingawa walikuwa hawajui kama dogo alikuwa anaongea ukweli au uongo.” Amesema Babu Tale.
Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo anataka Dogo Janja aviweke sawa.

“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli.” Babu Tale ameeleza.

Pia Amegusia pia tukio ambalo lilimsikitisha zaidi wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya menejimenti ya Mtanashati Entertainment.

“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa!
Wazazi wake nao wakawa wamekubali uongo wa mtoto wao wakaanza kutuongelea na sisi maneno ambayo ni uongo. Ulikuwa uongo wa watoto halafu bado wao wanakandamiza uongo zaidi ya uongo. Kwa kuwa ni mtoto kuna wazazi ambao walisimama nyuma yake ambao nao walikuwa wanasapoti. Aongee ukweli mimi ntamsaidia.” Babu Tale ameeleza.

Babu Tale ameeleza kuwa Dogo Janja ameshamtafuta kwa njia ya simu lakini amemwambia ujumbe ule ule kuwa awaambie ukweli watanzania.

Kwa upande wa dogo janja, ameongea amesisitiza kuwa. binafsi hakutaka kuizungumzia kwa undani kauli ya Babu Tale, zaidi alieleza kuwa alichokifanya kuomba msamaha alimaanisha kuwa alikuwa amekosea na hakuna aliyemsukuma kufanya hivyo.


“Mimi nimeomba msamaha kwa kuwa nataka kuweka mambo sawa na kumaliza tofauti na uongozi wangu wa zamani. Hivyo tu. Wakinikaribisha Tip Top itakuwa poa tu pia…fresh.”

EMMY'S LAMODA : HUU NDIO MTOKO WENYEWE WA OFISINI AMA KWENYE SHUGHULI MAALUM- "GENTLEMAN IN SUIT WEAR"

5:03:00 AM Add Comment





SHACK: HII NI ZAWADI KWA WAKAZI WA MWANZA

4:53:00 AM Add Comment

MSANII Chipukizi kutoka Jiji la Miamba MWANZA, SHACK DIZZONGA “SHACK” ameamua kutoa zawadi kwa mashabiki wake baada ya kumpokea vema Kupitia Track yake ya Kwanza inayofahamika Kwa jina la Tears.

Kupitia RCMS (Rock City Music Supporter,), Shack ametutonya kuwa hiyo itakuwa ni track nyingine tofauti ambazo tayari ziko tayari

Pata nafasi ya kuisikiliza Track yake Mpya ambayo amemshirikisha VM, inakwenda kwa Jina la ROCK CITY

PICHA: WAKATI NASUBIRI MISHE ZANGU SEHEMU FULANI..MARA NINAKUTANA NA KITU HIKI

4:23:00 AM Add Comment


PICHA: KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA ZANTEL ILIVYOWAJALI WAENDESHA BODA BODA WA JIJI LA MWANZA

3:15:00 AM Add Comment









CREDIT: G SENGO

TUMEMALIZA: HATIMAYE WIMBO MPYA WA NATTY E HUU HAPA…

3:06:00 AM Add Comment


BAADA ya kusubiri kwa Muda kadhaa Ngoma Mpya kutoka kwa “The Rap Chick”, Edna Elisha-NATTY E, Finally Exclusively kupitia BLACK TOUCHEZ, tunaishusha kwako Ngoma mpya ya Mwanadada huyu Kutoka jijini mwanza, anayesumbua sana kunako HIP HOP.


Pata nafasi ya kuusikiliza, na kama haitoshi, download na Ondoka nao kabisaaa..ukasikilize zaidi na zaidi

CMB PREZZO KATIKA TUHUMA NYINGINE YA MATUMIZI YA SILAHA

2:54:00 AM Add Comment

THE RAPCELLENCY JACKSON MAKINI “CMB PREZZO” Kutoka 254 (Kenya), ameingia katika Tuhuma nyingine baada ya kudaiwa kuwahi kumpa “Kifinyo”  Dj mmoja nchini humo kwa kutumia silaha yake ya Moto aina ya Bastola.

Kama utakuwa ni mdau mzuri wa TTM, kipindi cha Nyuma Tuliwahi kukupa mtonyo kuwa, Rapcelency Prezzo aliwahi kutuhumiwa kumpiga Jamaa mmoja hivi na Kitako cha bastora, basi imebainika kuwa, mnamo mwaka 2012, alifanya tukio la Aina hiyo kwa DJ STONE ambaye alikuwa ameandaa tamasha lililomshirikisha rappa huyo kutoka “Kenyatta land”

Kwa mujibu wa Maelezo kutoka kwa DJ STONE, inasemekana kuwa alikuwa ameandaa tamasha ambalo Prezzo alitakiwa Kuperform kunako Stage.

“Niliandaa tamasha ambalo lilifahamika kwa jina la BIG BROTHER TOUR huko Kitengela. Nilimpatia Prezzo Advance ya Kshs 40,000, na baadaye kumaliza Fedha zilizokuwa zimebaki baada ya kumaliza Show. Lakini Cha ajabu ni kwamba Prezzo aliniomba Tena pesa nyingine kiasi cha Ksh 5000 Kwa ajili ya mafuta ya gari lake, jambo ambalo lilikuwa ni kinyume cha makubaliano yetu” Alisema Dj huyo.

Aidha Dj Stone alizidi “kumiminika” kuwa, baada ya kukataa, Przzo na rafiki zake walimsukuma Ndani ya Gari na kuanza “kuonesha Mikono” ya kutosha, huku wakimkanya kuwa endapo taarifa hizo za kumchapa zitafika kwa vyombo vya habari, basi atajua nini maana ya maisha kudadadadaddddeki !!!


Kutokana na tukio hilo, DJ STONE andai kuwa tukio hilo lilimletea Athari Kubwa sana katika FIGO yake pamoja na kuvuja Damu ndani kwa ndani.

WATOTO WA BILL GATES WASITEGEMEE KURITHI UTAJIRI WAKE

2:20:00 AM Add Comment

KAMA Unajiita “mtoto wa kishua” halafu unategemea kila kitu kutoka kwa Dady na Momy, basi inabidi uwe na akili ya Ziada, huenda wazazi wako wakawa na Akili kama za BILL GATES.

Katika mkutano wa TED 2014 huko Vancouver, Colombia, Bilionea nayaeongoza kwa mkwanja ulimwenguni kote kupitia biashara yake ya MICROSOFT, BILL GATES na mke wake  MELINDA GATES, wamesema kuwa hawana Mpango wa kuwatajirisha watoto wao watatu kupitia utajiri walio nao.

Ingawa ni Kweli wana utajiri wa kuwafanya watoto wao kuwa mabilionea kwa kila Mmoja, Bill gates amesema kuwa kitu ambacho wanadhani Ni kizuri na kina ubora, ni kuwapa uhuru watoto wao kujishughulisha kwa bidii zote ili waweze kujivunia Nguvu na juhudi zao.

Pia katika ufafanuzi mwingine, Bill gates amedai kuwa, Watu wasidhani kuwa watoto wao wamekulia katika maisha ya hali ya juu sana huku wakipata matunzo ya Gharama kubwa, bali waliishi maisha ya Kawaida.

“Watoto Wetu wamelelewa na kukua katika mazingira ya kawaida sana. Tuliishi katika nyumba ya hali ya kawaida ambayo niliinunua Mwaka 1958. Tofauti na hayo, bado watoto wetu hawakupata nafasi ya kupanda Ndege Kubwa za Binafsi. Walikuwa wakienda shuleni kwa Mabasi ya shule ya kawaida, na walisoma Shule ambazo ni za umma, maana hata mama yao alisomea huko huko”

Alisema Bill Gates

NYUMBA YA MWANARIADHA PISTORIOUS, AMBAYO MAUAJI YA MPENZI WAKE YALIFANYIKA, SASA IKO SOKONI

1:52:00 AM Add Comment

MWANARIADHA Mlemavu, Oscar Pistorious ambaye anakabiliwa na mashitaka ya Kumuua Mpenzi wake, mwanamitindo REEVA STEENKAMP, ameamua kuiuza nyumba yake kubwa ya kifahari iliyoko katika mji wa Pretoria, nchini Afrika ya Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwanasheria wa familia ya Pistorious, BRIAN WEBBER, amesema kuwa, awali Oscar Pistorious alikuwa amepanga Kufunga nyumba hiyo na Kuiacha mpaka pale Maamui dhidi ya kesi yake yatakapotolewa, lakini kulingana na kuongezeka kwa Gharama za uendeshaji wa kesi yake,, imemlazimu kuipiga bei.


















Pia Webber ameongeza kuwa, Pistorious hajawahi kurudi tena katika Himaya yake hiyo tangia siku aliyompiga Risasi Mpenzi wake huyo, na hana mpango wa Kurudi tena katika nyumba hiyo Mpaka hivi sasa..
Mjengo huo unauzwa kwa Kiasi Cha Dolari za kimarekani 456,000, sawa na Shilingi za kitanzania 7,29,600,000.

Aidha baadhi ya wataalamu wa masuala mbali mbali hasa ya kibiashara, wamedai kuwa kuna uwezekano nyumba hiyo ikachukua muda mrefu kununuliwa, kutokana na tukio lilitokea ndani yake

Kesi ya Oscar Pistorious, itaendelea kusikilizwa tena Kuanzia mwezi wa Nne, na huenda ikachukua muda zaidi, kutokana na ushahidi kuzidi kutafutwa 

MNADA BANNER