REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MUNGU OKOA JAHAZI !!!! : HUYU NDIYE RAPPER WA KIKE ALIYEKULA PINGU KWA KUIBA KUPITIA INSTAGRAM !!!!

2:54:00 AM Add Comment

Na Hezroni Munisi  
#WatuWaMungu kumbe bado kuna masuala ya kuibiana bado kupitia Instagram na watu bado wanapumbazika kabisa hivi hivi !!!!

Sasa , Soko la Muziki wa Hip Hop hasa kwa upande wa "Wachanaji" wa Jinsia ya Kike, limeingiwa na ka-dosari ambako wakikachukulia poa katakuja kuwaaibisha

Rapper ambaye amejipatia Umaarufu kupitia Instagram, wengine mnasemaga "Instagram Rapper", anayefahamika kwa jina la YOUNG ASH, amejikuta akiramba Pingu bila matarajio baada ya kubainika kuwa amekuwa akiwaibia Followers wake zaidi ya 360,000 kupitia card ya Benki ambayo ni Feki

Picha Liko Vipi sasa Wazee wa Kazi !!!!!
Young Ash ambaye ameachia Tracks kadha wa kadha ikiwemo PRETY AGAIN, RIDE OR DIE, LETTING YOU GO na nyinginezo kibao, amekuwa akitoa taarifa za uwongo kwa baadhi ya Watu na wale ambao wangeingiwa na mioyo ya Huruma, basi wangesalimisha pesa na hata kujikuta wakitoa taarifa zao nyingi sana za Kibenki.


Pia inasadikika kuwa, Kumekuwa na jengo lililojificha huko huko Nchini Marekani, ambalo lina vifaa mbali mbali , ambalo hupokea taarifa hizo na ndani ya Dakika Moja tu vijana hukomba kila kitu kutoka kwenye account zao za Bank

Ingawa yeye kwa upande wake amekanusha kashfa hizo kupitia Instagram account yake YOUNG ASH MUSIC, ila polisi bado wanashughulikia madai hayo ya walioibiwa

ETI NINI !? : MZAZI MWENZAKE NA RAPPER FUTURE ATAMANI AMRUDISHIE MBEGU ZAKE ZA KIUME

2:37:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
Wahenga walisema, "NINGEJUA HUJA BAADA YA......" na hiki ndicho ambacho inabidi ukifahamu hivi sasa ili baadaye usije ukajuta hata kidogo

Wiki Hii imekuwa na Matukio ya aina mbali mbali, lakini hili la Rapper FUTURE na Mzazi mwenzake Brittni, lilichukua nafasi ya aina yake ikiwa ni kitu kinachotafsiriwa kuwa ni "Wivu uliokithiri kwa mtu ambaye unajua ni Kicheche ama ni Msaliti ama ni Mchepukaji maridadi kuliko Kawaida"

Hii ilitokea baada ya Future kubainika kuwa alionekana akichepuka na mmoja kati ya Mabinti alipokuwa ameenda kwenye "kimeo" chake huko Nchini Canada kwa ajili ya kupiga mkwanja, na hii ilinaswa na mapaparazi na wadakuzi wa mambo na hatimaye kuanza kusafirisha Picha kadha wa kadha za Future na Mrembo huyo kunako mitandao ya Kijamii...

Sasa, Hali imeonekana kuwa Ngumu kupita maelezo, maana maumivu ya Wivu yanazidi kumtafuna sana Brittni, Mama wa PRINCE ambaye alimzaa na Hitmaker huyo wa MASK OFF, pengine alidanganywa danganywa na bata la siku ile.

Safari Hii Brittni amefikia hatua ya kujuta na hata kutamani kuzirudisha Mbegu za Kiume za Future ambazo hazina nidhamu katika maisha yake licha ya kwamba tayari keshapata naye mtoto.

Kukazia Zaidi, Brittni ambaye hivi sasa ameweka wazi kuwa Yuko Single, amedai kuwa anajuta kupata mtoto kabla hajafunga Ndoa ama hajaolewa, ahadi ambayo alipewa na Rapper Huyo, namnukuu

" Ninataka Yule atakayemjali mwanamke kama mwanamke bila chenga chenga za huku na kule, na sifanyi hili kwa ajili ya kuweka kitu sawa zaidi kuhitaji Hilo nililoanza nalo"

Bibie huyu hakuishia hapo, bali aliamua kutoa ushauri kwa mabinti ama wanawake wengine hasa akitumia uzoefu wa kile alichopitia...namnukuu

"Msizae watoto mpaka mtakapofunga Ndoa!"


MNADA BANNER