REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SKENDO 3 HATARI ZA BONGO KATIKA MWAKA 2014 KWA UPANDE WA BURUDANI

6:48:00 AM Add Comment

·        MISS TANZANIA NA SITTI MTENVU
Sitti Mtemvu alichaguliwa kuwa Miss Tanzania, na kamati ya Hashim Lundenga kama waandaaji wa mashindano hayo. Lakini watanzania wengi hawakukubaliana na Uteuzi huo, jambo ambalo liliwafanya kufanikisha Uwongo na Uozo wa Sitti Mtemvu ;
  • ·        Sitti Mtemvu alikutana na madai yafuatayo.
  •    Kudanganya Umri
  • ·        Rushwa/Kufahamiana/Nepotism Baina ya Lundenga na Abas Mtemvu-Baba Mzazi wa Sitti (Inasemekana hivyo ingawa hatuna uhakika na haijathibitika)
  • ·        Kuwa na Mtoto

Lakini hayo yote yalimalizika baada ya Bibie huyu Kuvua taji hilo na Kukabidhiwa Miss namba Mbili, Lilian…lakini Mashindano hayo yamepigwa Stop na Serikali kwa Miaka Miwili.
Hata Hivyo Sitti alikanusha Taarifa hizo


·        LAVEDA KUJICHUWA:
Laveda, Mshiriki wa Big Brother Africa Hotshots aliyekuwa akiiwakilisha Tanzania, aliingia kunako Hot Skendo, kwa madai kuwa alijichuwa “Yaani Masturbation” katika Jumba hilo

Tukio hilo liliweza kuvuma sana kwa Mwaka 2014, huku wengi wakionekana kumlaumu sana Laveda kuhusu Ishu Hiyo, kuwa amelidharirisha taifa





·        FAMILIA YA MBASHA:
FAMILIA Emannuel Mbasha na Mkewe Flora Mbasha, iliingian katika Skendo kali ikiwa ni Baada ya Kutokea tuhuma za Ubakaji zilizofanywa na Emanuel Mbasha

Emannuel Mbasha: alidaiwa kumbaka Shemeji yake (Mdogo wa Flora Mbasha), Jina lake tunalihifadhi na kuanza kusakwa Mara kadhaa na jeshi la Polisi.

Emannuel alifunguliwa Kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na Jarada la Kesi TBT/IR/1865/2014 na kudaiwa kufanya ubakaji huo mara Mbili (ijumaa na Jumapili) Nyumbani kwake Tabata Kimanga DSM

Flora Mbasha alijikuta akizama kunako skendo hatari ya kuishi kwa Mchungaji wake, Mchungaji Gwajima, huku ikisemekana kuwa, wamekuwa “Wakidandiana”, hali ambayo ilimfanya Emmanuel Mbasha, Mume wa Flora amsihi Mchungaji huyo aachane na Ndoa yake

Tunamnukuu:
“Nimesika mke wangu baada ya matatizo yetu amehamia nyumbani kwa Gwajima. Nataka mumwambie Gwajima aniachie mke wangu, mbona ananifanyia hivyo?”


Lawama nyingi zilitoka kwa Emmanuel kuhusu Flora “Kudandiana” na Mchungaji Gwajima, madai ambayo Flora Mwenyewe aliyakataa na kusema mumewe huyo anafanya hivyo maksudi

BAADHI YA CELEBRITIES WA BONGO WALIOPATA WATOTO 2014

6:08:00 AM Add Comment

Na Frank Magnus Joachim, BLACK TOUCHEZ
KWA UPANDE mmoja, kuna wasanii hapa Nchini Tanzania ambao walifanikiwa kuongeza Furaha katika Ndoa ama Mahusiano yao baada ya kufanikiwa kupata watoto


·        MWEZI OCTOBER: NAY WA MITEGO
NEY WA MITEGO na Mchumba ake SIWEMA, walifanikiwa kupata Mtoto wa Kiume, na alivujisha Mtonyo huo kupitia account yake ya Instagram
Mtoto huyo alizaliwa tarehe ambayo mama wa Nay Wa Mitego, alizaliwa Pia.


·        MWEZI OCTOBER: LAMECK DITTO
Msanii Lameck Ditto alifanikiwa kupata Mtoto wa Kiume ambaye Mkewe alijifungua salama kunako Hospitali ya SANITAS, iliyoko Jijini DSM
Dotto alimuita mtoto huyo LAMECK


·        MWEZI MAY: MWISHO MWAMPAMBA
Mwisho Mwampamba pamoja na Mkewe Merly , Raia wa Namibia, walifanikiwa kupata Mtoto wa Kiumea ambaye aliongeza Idadi ya watoto wawili kwa wanandoa hao
Mtoto Huyo walimuita King David, na alipatikana Mwishoni mwa Mwezi May.

MWISHO na MERLY walikutana katika Jumba la BIG BROTHER, kunako Mchakato wa BBS ALL STARS 2011, na kufunga Ndoa.
Mtoto wao wa Kike, walimpata 2012.


·        MWEZI MARCH : SUMA MNAZALETI
BAADA ya Mke wake Kuteseka Kwa Uchungu kwa Muda wa Siku tatu, rapper Suma Mnazaleti aliweza kutoa Taarifa Kuwa, My Wife wake amefanikiwa kushusha  Mtoto wa Kike.

Mtoto Huyo alikaribishwa Vyema Duniani, kupitia Hospitali ya Palestina, iliyoko Sinza, DSM


·        MWEZI  FEBRUARY : LUCCI
Producer Lucci pamoja na Mkewe Lisa, walifanikiwa Kupata Mtoto wa Kiume, kipindi hicho Lissa akiwa ni Mchumba wake
Mtoto huyo alipewa Jina la LEEROY KING TSERE, na Producer Lucci alionekana kufurahia sana uwepo wa Ninja hilo kunako familia.


·        MWEZI FEBRUARY: SOGGY DOGGY
Rapper na Mtangazaji wa radio, Soggy Doggy, alifanikiwa kuongeza Mtoto Mwingine wa Kike kunako Mwaka 2014, akiwa na mpenzi wake LEAH CHOMA

Soggy aliweza kuonesha Furaha yake kupitia Face book, na kubainisha kuwa, mtoto huyo anaitwa ABIGAILI


·        MWEZI FEBRUARY: PIPI DOREEN
Mrembo aliyefanya Vyema sana kunako Mkwaju wa Njia Panda, PIPI, naye alifanikiwa kuongeza mtoto wa Pili wa Kiume kwa Mwaka 2014
BRANDON alipatikana kunako Hospitali ya KAIRUKI, iliyoko Jijini DSM.


NDEGE YA ASIA: MIILI 40 YAPATIKANA

5:46:00 AM Add Comment
NDUGU Wa Abiria waliokuwa katika Ndege Hiyo, walijikuta wakiwa katika hali hii baada ya kubaini kuwa Miili 40 imeonekana katika Bahari

BLACK TOUCHEZ/BBC/DAILY MAIL
MIILI arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea, ikiwa ni Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia, yenye namba QZ8501At ,

Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo, moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.

Aidha taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Moja Ya Vitu vinavyodhaniwa kuwa katika Ndege Hiyo, kikielea Baharini

Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria 162, ilikuwa  ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,lakini ilipotea siku ya JUMAPILI.

Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
KIFAA Hiki, inasadikika kuwa ni Mlango wa Ndege hiyo, kikiwa katika maji 

Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .

Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .


Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.

UNAHITAJI KUFANYA SHOW NA DMX?..ANDAA BOX 3 ZA KONDOM

11:49:00 PM Add Comment

Na Frank M. Joachim, BLACK TOUCHEZ
KUNA VITU ambavyo Wasanii Wengi Maarufu ambao tayari wameshakuwa na majina, huvihitaji kila wanapoenda katika Show Fulani ambayo imeandaliwa kwa ajili yao, au wameandaa wao Binafsi.

Nchini Marekani, BLACK TOUCHEZ BLOG imeweza kunasa baadhi ya Mahitaji ambayo Wasanii wakongwe hawa  huvihitaji katika Vyumba ama Mahali wanapofikia kabla ya kupanda kwa Show, na hata Baada ya Kumaliza Show



KANYE WEST:
KIPINDI cha awali, KANYE WEST alikuwa akihitaji Urembo Mweupe mahali ambako angefikia kabla ya kupanda Kunako Stage, lakini kwa kuwa hivi sasa ni baba wa North West, basi huhitaji Watu wa kumtizama Mtoto wake huyo, Chumba maalum ambacho kitakuwa na TV maalum yenye Program maalum anazopenda Binti ake huyo (North West), na hugharim USD 8000.

Pia Kanye West Huhitaji Mpish Maalum ambaye ataandaa chakula maalum kwa ajili ya Mtoto wake…na hasa kile anachokifurahia.


JAY Z:
Chanzo Kimedai kuwa, Kipindi ambacho Jigger alikuwa katika Tour na Justin Timberlake, waliyoipatia jina la LEGENDS OF SUMMER TOUR, alihitaji Club maalum kwa ajili yake na wenzake mahali ambako alifikia.
Na moja kati ya vitu ambavyo alionekana kupendelea sana kutumia, ni pamoja na Sigara


DMX
Rapper Huyu hapa ambaye awali alivuma sana na Kundi la RUFF RIDERS, inasemekana yeye huwa hana Mbwembwe nyingi na mizunguko Mingi, kuhusu maandalizi ya mahali ambako atafikia kwa ajili ya Show.
Chanzo kimedai kuwa, DMX huwa yuko wazi kabisa kuwa anahitaji uwepo wa Box 3 za CONDOMS (Kinga) na Gallon moja ya HENNESSY


BEYONCE:
MAMITO huyu ambaye mwaka huu anaumaliza Vizuri, inasemekana kuwa katika Chumba anachofikia, hupenda kuwa Muwazi katika Bidhaa za Kibiashara ambazo huwa anafanya nazo kazi. Hivyo huhitaji Bidhaa ziwepo Chumbani Kwake, (Mfano PEPSI, HONEY NUT CHEERIOS, nk.)
Pia Beyonce Huhitaji Choo kiwe safi kabisa ili kuepuka Maradhi, na inasemekana kuwa huwa hapendelei Chumba chake kiwe na Chocolate au Vitu Vitamu Vitamu kama Vile PIPI.


SEAN COMBS “P.DIDDY”
MKONGWE Huyu anafahamika sana kwa kupenda Maisha ya “BATA” na raha tele. Sasa kama unamuhitaji katika Tour ama Show yako, basi andaa vitu Vifuatavyo katika Chumba atakachofikia:
TAULO 204, SABUNI 20, CHUPA 2 ZA HENNESY, CHUPA 2 ZAsanta Margherita Pinot Grigio, CHUPA MBILI ZA Veuve Clicquot, CHUPA MOJA YA  Dom Perignon, Grey Goose vodka, MAUA MEUPE , na GARI AINA YA MAYBACH yenye Bullet Proof, inayogharimu USD 300,000


PHARELL WILLIAMS:

HITMAKER huyu wa Happy, huhitaji akina dada ambao hucheza style ya BELLY DANCE (Belly Dancers)


50 CENTS ATOKA NDUKIIIIIIII

5:59:00 AM Add Comment

Na BLack Touchez
KABOOOOM !!. Wengi tunamfahamu Rapper Jackson Curtis ama 50 Cents kama Mbabe wa Ma-beef, na endapo utajaribu kumchezea , basi itakula kwako kwa atakachokufanyia.
Lakini This Time, amejikuta akitoka “Nduki” mbaya baada ya kukutana na Mbabe wake katika Mtandao wa Instagram, ambaye aliamua kuchana Fif kuhusu suala zima la Malezi.

PICHA LILIVYOANZA:
Fif alipost Picha ya Mtoto wake wa pili ambaye bado ni Mdogo, aliyemzaa na mwanamitimndo maarufu DAPHNE JOY katika account yake hiyo ya IG, hali ambayo ilimfanya fan wake mmoja wa kike kucomment kuwa anamuonea huruma Mtoto wa Kwanza wa 50 ambaye ni MARQUISE JACKSON mwenye Umri wa Miaka 16.


Shabiki huyo aliashilia kuwa, ama alimaanisha kuwa Muda Mwingi 50 amekuwa akionesha upendo wa dhati nje nje kwa Mtoto huyo Mdogo, na kumsahau kabisa Mtoto wake huyo wa Kwanza, jambo ambalo halipendezi kwa mzazi kama 50.

Baada ya Bibi huyo ku-comment Hivyo, 50 alionekana kukaa kimya na hata kutokujibu chochote juu ya Maoni ya Fan wake Huyo

UKWELI UKO VIPI?.
Inawezekana kabisa 50 haoneshi mapenzi ya Dhati kwa Mtoto wake huyo wa Kwanza, ukizingatia hata kipindi cha Nyuma ameshawahi kulalamikiwa, hasa kwa kutohudhuria mahafali ya Mtoto wake huyo wakati akihitimu High School.


MUNGU WANGU: NICKI MINAJI AKIRI KUVUNJA AMRI YA SITA NA RAPPER MEEK MILL..

8:24:00 AM Add Comment

Na Frank Joachim/ Black Touchez
NICKI MINAJI KUMBE ALIVUNJA AMRI YA SITA NA MEEK MILL
UGOMVI Wa Nicki Minaj na Aliyekuwa Boy Friend Wake SAFAREE SAMUELS, unazidi kuibua Jipya Hadi Jipya, na hili ni jingine ambalo TTM tumeweza kulinyaka na Tunalishusha kwako rasmi.

Rapper Nicki Minaj amekiri Mwenyewe kuwa, ni Kweli “alidandiwa” na Meek Mill kipindi ambacho alikuwa yuko katika Mahusiano na Bioyfriend Wake huyo, Safaree


First lady Huyo wa YMCMB, alifikia hatua ya Kukitri kufanya Kitendo Hilo, kupitia majibishano ya Message na Ex wake, ambapo alimthibitishia kabisa kuwa alifanya usaliti huo na Rapper Meek Mill kutoka MMG, Miezi 9 iliyopita.

Malalamiko ya Nicki Minaj kwa Safaree ni kwamba eti jamaa alikuwa akimfanyia Visa kadhaa, ikiwemo kugombana naye mara kwa mara, na amevumilia mengi sana katika Mahusiano hayo.


Nicki Minaj na Safaree Samuels wamedumu katika Mahusiano kwa Muda wa Miaka 12

HATIMAYE SHEDDY CLEVER AMEOMBA MSAMAHA

7:08:00 AM Add Comment

Na Frank Joachim/instagram
Tunajua Kuna Mambo mengi ambayo kila Mtu anayafanya na yasimpendeze Mtu ama yakamkwaza Mtu kwa namna yoyote

Hiki Ndicho alichoshtukia Producer Kutoka Burn Records , SHADDY CLEVER, na hatimaye kuamua kuomba Msamaha kwa wale Wote aliowakwaza.


Kupitia account yake ya INSTAGRAM, Sheddy ameomba Msamaha kwa Yeyote Yule ambaye alikwaza na kile alichokifanya kwa Mwaka Mzima wa 2014.. na hiki ndicho alichokiandika:



INSTACOP: AUNT EZEKIEL- IKO WAPI (MIMBA) MBONA HIVYO LAKINI?

6:31:00 AM Add Comment

Na Frank Joachim- @babajutibebe
KABOOOOM!!!!…haya SASA, Sawa, kumekuwa na Tetesi kuwa “Kali la Muvi” hapa Bongo hasa klwa upande wa akina Dada, AUNT EZEKIEL ameanasa “Kibendi bin Ujauzito kama sio Mimba” kutoka kwa Mwanaume ambaye sio Yule Husband tunaye Mfahamu..(Wa Dubai)

Sasa, Leo Kunako Instyagram, Mamito huyu ambaye ukimpa Scene yeyote anaichinja, amepost Picha huku akiwa amepigilia gauni Refu, Jekundu na Kubwa, huku akiuliza Kuwa Huo, mnaouita Ujauzito uki wapi?


Soma hapa:


ROMA ANAJIPANGA KWA AJILI YA 2015?..AMA NDO ANAFUNGA 2014?

6:02:00 AM Add Comment

Na Frank Joachim-@babajutibebe
WENGI this Time wamekuwa kama hawako karibu sana na Mikwaju ambayo Rapper Roma amekuwa akiachia ikiwa ni kuanzia 2030.

Ikiwa ni baada ya kuachia Mkwaju wa Mwanakondoo, Hatimaye Roma ameamua kustua Hisia za Mafanz  wake na hasa wanaokubali Muziki wake tangia kipindi kile anaanza kutesa Air Waves na Mzigo wa TANZANIA.

Kupitia account yake ya Instagram, Roma amepost Video Clip ambayo inamuonesha akiwa Studio, kunako Session ya mkwaju ambaio unaweza kuwa ni Mpya kwa namna moja ama Nyingine.


Kuna Uwezekano mkubwa kabisa, Mzigo Huo Ukapwa Unapikwa TONGWE RECORDS, na Producer ambaye anasuka kila Kitu, inawezekana akawa Ni J RYDER, ambaye alipika mikwaju Mingi sana ya rapper Huyo, ikiwemo MATHEMATICS, MECHI ZA UGENINI na Nyinginezo kadhaa

ANNIE KANSIIME NDIYE TU MWENYE NGUVU NA USHAWISHI NCHINI UGANDA-2014

5:55:00 AM Add Comment

Na Black Touchez/Satisfashion Ug.
TTM Tunaamini Kabisa Kuwa Jina La Annie Kansiime Ni Moja Kati Ya Mvuto Hasa Katika Kucheka Kwa Watu Wengi Ambao Wanapenda Comedy Za Aina Mbali Mbali.

Sasa Kama Ulikuwa Hujafahamu, Mtandao Mmoja Wa Masuala Ya Mitindo/Fashion  Nchini Uganda, Unaofahamika Kwa Jina La Satisfashion Ug Umemtangaza Rasmi Kuwa “Mvunja Mbavu” Huyo Ni Mtu Ambaye Ameonekana Kuwa Na Nguvu Kubwa Ama Ushawishi Mkubwa Sana Kwa Mwaka 2014 , Nchini Uganda.

Kwa Mujibu Wa Taratibu Zao, Mtandao Huo Umesema Kuwa, Annie Alipigiwa Kura Na Wadau Wengi Sana, Na Hatimaye Kuwalaza Chini Washiriki Wengine 39 Ambao Pia Wana Majina Yao Tu Na Wanajihusisha Na Masuala Kadha Wa Kadha Ikiwemo Fashion, Burudani, Na Hata Mitindo Na Maisha Nchini Humo


Waliokuwa Wakichuana Na Kansiime Ni Pamoja Na Bebe Cool, Eddy Kenzo, Juliana Kanyomozi, Na Wengineo Kadha Wa Kadha

ROAD TO 2015: LIL WAYNE AMEMWAGA WINO MWINGINE KATIKA SURA YAKE

5:50:00 AM Add Comment

Black Touchez
Lil Wayne Ni Moja Kati Ya Rappers Ambao Wanapenda Sana Kuchora Tattoo Katika Sehem Kadha Wa Kadha Za Mwili Wao.

Na Hivi Sasa Unaweza Kukubali Kabisa, Katika Rappers Duniani Ambao Wana Tattoo Mwilini Mwao Ni Pamoja Na Lil Wayne Ambaye This Time Ameamua Kuongeza Another Tatoo

Kupitia Account Yake Ya Instagram, Lil Wayne Amechora Tattoo Nyingine Mbili Ambazo Zinaonekana Kuwa Na Maana Tofati..

Katika Upande Wa Kidevu, Wizzy F Baby Ambaye Hivi Sasa Haijulikani Kama Ni Tayari Kashapigana Chini Na Cash Money Records Ama Lah, Amechora Tatto Ya Jicho Ambayo Tunaamini Very Soon Ataachia Maana Ya Tatoo Hiyo.

Na Katika Upande Wa Juu Ya Nyusi Zake , Weezy Amechora Tattoo Ambayo Ina Maandishi Fulani Hivi Yaliyo Katikan Lugha Ya Kiarabu, Inayomaanisha Mumm’as Boy.


Jombaa Amabye Alihusika Katika Uchoraji Wa Tatto Za Lil Wayne, Anafahamika Kwa Jina La Spider, Na Alienjoy Sana Kumpiga Tattoo Hizo Rapper Huyo Mkali Na Mwenye Tittle La Aina Yake Ulimwenguni.

MUACHENI MTOTO WANGU TAFDHARI- TYGA

5:45:00 AM Add Comment

Na Black Touchez & Tyga Tweet
Siku Ya Jana Kunako Mtandao Wa Kidaku Ulimwenguni, Tmz, Kulikuwa Na Taarifa Kuwa, Rapper Tyga Yuko Katika Mchakato Wa Kumshtaki Blac Chyna Ambaye Ni Mzazi Mwezake, Kwa Madai Eti Anatafuna Bat Asana, Hali Ambayo Sio Nzuri Kwa Mtoto Wao King Cairo

Ishu Hiyo Imeweza Kubadilishwa Na Mhusika Mwenyewe Yaani Tyga Ama T-Raw Baada Ya Kukutana Nayo Katika Mtandao Huo, Huku Ikionesha Kumkwaza Kwa Namna Kubwa.

Tyga Ametweet Kuwa Tmz Wana Mpango Wa Kutaka Kumfanya Aonekane Mbaya Kwa Blac Chyna Na Hata Watu Wengine, Jambo Ambalo Ameona Halina Tatizo Kwa Jina Lake Na Maisha Yake.



Lakini Kitu Ambacho Kamwe Hataki Kiguswe Na Wala Kuhusishwa Katika Maisha Yake Na Kila Linalomsibu, Ni Mtoto Wake King Cairo, Ambaye Hivi Sasa Analelewa Na Mama Yake (Blac Chyna)

MTOTO WA NAS..NA BIASHARA YA MAKE UP

6:27:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ BLOG
MNAMO mwaka 1994, Rapper Nas alikuwa na Project iliyokuwa ikifahamika kwa jina la ILLMATIC, na safari Hii binti ake ameamua kuanzisha LIP GLOSS (Tumezoea LIPSTIC) yenye jina kama hilo hilo

Kupitia account yake ya Instagram, NAS aliweza kupiga Promo kuhusu kuanzishwa kwa kampuni mpya ya Binti ake huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 20, ambayo itakuwa inatengeneza make Up mbali mbali pamoja na Lip glossy hiyo ya ILLMATIC


Aidha inasemekana kuwa, Binti huyo aliamua kuiita lip glossy hiyo jina la Mkwaju wa baba ake kwa sababu ni moja kati ya nyimbo anazokubali kupita maelezo.

MTOTO WA LIL WAYNE , MIAKA 16, NA GARI MBILI MPYA

6:20:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ 
HOLD ON FELLAZ! Miaka 16 haijafika with nothing, bali imekuja na Ndiga kutoka kwa Baba yake mzazi , LIL WAYNE

·        Iko Hivi…
REGINAE CARTER ambaye ni Bint wa Lil Wayne kutoka YMCMB, amejikuta akishindwa kuamini zawadi kali alizopewa na baba yake katika Siku yake maalum ya kukumbuka kuzaliwa kwake.


Reginae ambaye ametimiza umri wa Miaka 16, amepewa Ndinga Mbili na Dingi ake huyo, ambazo ni FERARI GTO yenye rangi Nyeupe pamoja na BMW SUV yenye rangi Nyekundu, ingawa hatujafahamu kama anaweza kukanyaga Gia..ama lah

·        Mama Mzazi Wa Reginae Na Mumewe….

Mama Mzazi wa Reginae Carter, TOYA WRIGHT alikuwepo wakati tukio zima linafanyika, sambamba na mumewe wa sasa MEMPHITZ, inagawa bado haijafahamika kama walichangia katika siku hiyo maalum

MNADA BANNER