REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

F*CK WIZ KID: MANENO YA MSANII KUTOKA UGANDA, NI BAADA YA KUMDHARAU JOSEE CHAMELEON

2:50:00 AM Add Comment
KAMPALA, Uganda
USIKU wa jana kunako GOLF COURSE HOTEL Jijini Kampala, Msanii Wiz Kid kutoka Uganda alishusha Burudani tamu katika THE GUINNESS VIP PARTY

Sasa, Mbwadidi lilikuja katika kujikuta akitukanwa na Msanii kutoka Nchini Uganda katika mtandao wa facebook, hasa kutokana na kile kitu ambacho alikijibu katika Interview na Kituo cha NTV-Uganda.

ILIKUWAJE?
WIZ KID, ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya BET AFRICAN ACT 2014, aliulizwa Swali kama anamfahamu msanii anayeitwa JOSE CHAMELEON (infact kila mtu anamfahamu Star huyu wa Uganda), lakini cha ajabu alijibu hamfahamu na wala hana wazo kama kuna mtu wa jina hilo anayemfahamu.

Tofauti na hilo, katika kujibu kwake, Wiz Kid alionesha Vitendo Fulani hivi ambavyo vilitafsiriwa kama Dharau.


Sasa, bada ya hayo kutokea, yalionekana kumkwaza sana Msanii PALLASO wa Uganda, ambaye aliamua kuingia kunako ukurasa wake wa Facebook na kushusha matusi haya:

HUYU NDIYE MSANII WA KENYA, ATAKAYEFANYA KAZI NA ROSE MHANDO.

2:41:00 AM Add Comment
KENYA
TRACK yake ambayo imemuweka mahali pazuri, inafahamika kwa jina la  AIRA MAGILANI ENKAI, ambayo kwa sehemu kubwa imepata Airtime Nchini Tanzania.

Jina lake anaitwa MARYANE TUHUMA, msanii wa Gospel mwenye Umaarufu mkubwa sana Nchini Tanzania kuliko Nyumbani kwao Kenya.
Ni Mzaliwa wa Eneo la KAJIADO huko Nchini Kenya, Maryane yuko Mbioni kuachia Kazi yake Mpya, akiwa amemshirikisha ROSE MHANDO kutoka Nchini Tanzania.

Awali alikuwa anasoma Chuo Cha Uuguzi, lakini aliachana na Chuo akiwa Mwaka wa tatu, ili kujikita zaidi katika Muziki wa Injili muda wote

§  Anamzungumziaje Rose Mhando
Maryane amesema kuwa, Rose Mhando amekuwa ni rafiki yake wa karibu sana, na ni kama mama yake, kwa sababu muda mwingi wanashauriana katika masuala ya Kidini zaidi


Wimbo Huo utakuwa katika Lugha ya Kiswahili na unatarajiwa kuwa Hitsong Balaa

TIZAMA HAPA: HIVI NDIVYO BINTI MLEMAVU ALIVYOBAKWA NCHINI KENYA

1:45:00 AM Add Comment

TYGA AMFUNGUKIA DRAKE. ASEMA NI MNAFIKI KWAKE. PIA HAZIIVI NA NICKI MINAJ

1:28:00 AM Add Comment
HNHH & BLACK TOUCHEZ
KAMA ni time ya Ku-ride Solo and Independent, basi ndiyo inayopatikana kwa rapper Tyga, ambaye hivi sasa yuko katika Mchakato wa kupigana Chini na Label yake ya YMCMB (Kwa mujibu wa Tweet Yake)

TTM tumenyaka mbwadidi jingine kuwa, Tyga “amefyatuka” kuwa hivi sasa haziivi na Vichwa viwili kutoka katika Label hiyo, DRAKE “Dreezy” na NICK MINAJ

Sababu kubwa ambayo imewafanya watu hawa kuchuniana, inasemekana kuwa ni baada ya Tyga kutweet kuwa YMCMB wanamuwekea “Kiwingu” katika Albam yake mpya, na anahisi itabaniwa kutoka katika Tarehe iliyopangwa

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, tulikupa mtonyo kuwa Tyga alifikia hatua ya kutishia kuvujisha Albam nzima endapo haitaachiwa siku husika, na tayari ameshaachia mkwaju mpya, hali ambayo kama sio Game la biashara, basi atakuwa amepigana chini moja kwa moja na YMCMB.

Katika Maelezo yake, Tyga alisema kuwa hivi sasa hana mahusiano mazuri na wawili hao, na anajaribu kuwa Huru na watu ambao anaamini ni “kiwingu” kikubwa kwake.

v Hampendi Sana Drake Sababu Ni Mnafiki Kwake
Pia Tyga ameongeza kuwa, Binafsi hampendi Drake kwa sababu ni Mnafiki kwake, ingawa bado atazidi kupenda Nyimbo zake sababu anazipenda.

Aidha Tyga ameongeza kuwa, anaamini kuwa ni kama walikuwa wanalazimisha uhusiano baina yao wawili.

Na hiyo ni kwa sababu Lil wayne aliamua kuwaweka kundi moja ambalo ni YMCMB ndo maana wamekuwa wakifanya kazi pamoja lakini ukweli ni kwamba hampendi DRAKE.

v Hii Ndiyo Sababu Iliyomfanya Ajiunge Ymcmb
Katika kuzidi “Kubumbulua” mambo Mengi, tyga ameongeza kuwa, Mtu aliyempeleka YMCMB, ni Lil wayne, hivyo huyo ndiye aliyemfanya amwage wino kunako mkataba wa Kundi hilo. Hivyo sio Drake, wala Nicki Minaj aliyemshawishi ajiunge na Team hiyo iliyotesa sana na Mkwaju wa BED ROCK


 Pia tyga ameongeza kuwa, asilimia kubwa ya majembe yaliyoko YMCMB, si kusema kwamba ni marafiki wa Dhati, bali kuna wengine wanalazimisha uhusiano wa kirafiki ili wapige kazi, ukizingatia wako kundi moja

JIPYA KUHUSU NDOA YA JAY Z NA BEYONCE, BAADA YA UVUMI WA KUACHANA KUENEA

1:21:00 AM Add Comment
HNHH, Marekani
KIPINDI fulani hivi kulikuwa na info kuwa wawili wapendanao katika ndoa huku wakiwa na Mtoto mmoja, JAY Z na BEYONCE, wanazinguana vya hatari na huenda wakapigana Chini kama sio Kuachana

Sasa, Kwa Mujibu wa PEOPLE MAGAZINE, ttm tumepata Mtonyo wa Juu kwa juu kuwa wawili hao hivi sasa wanatarajia Kurenew Ndoa yao..
Jarida hilo limemwaga Mtonyo kuwa, ni kweli ndoa hiyo ilikutana na mbwadidi la migogoro kwa nafasi kubwa, lakini hivi sasa wameamua kuweka kando tofauti zao, na kulianzisha  upya Jahazi lao, ambalo walipeana ahadi kuwa watakomaa nalo mpaka lizame na wote wawe humo humo.

v Sababu Kubwa Ni Hii Hapa
Jarida hilo halikuishia hapo, bali limezidi kufyatua info kuwa, Sababu kubwa na maalum ambayo imewafanya wawili hao kufikia uamuzi huo, ni kuweka picha nzuri, pamoja na kuelekeza majeshi yote kwa mtoto wao BLUE IVY.

Aidha inasemekana kuwa, wawili hao wamegundua kuwa, Kumlea mtoto wao wakiwa pamoja na kukiwa hakuna Tofauti ya aina yoyote ile, basi italeta mazingira mazuri na malezi imara yenye furaha kwa Mtoto huyo


Wawili hao wamedhihirisha kupendana zaidi na zaidi hasa walipokuwa wakitembelea sehemu mbali mbali wakiwa na mtoto wao huyo, na inasemekana hivi sasa wako very Busy Studio, kupika ALBAM ya pamoja

MNADA BANNER