REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: WALA USIPITWE NA HILI.....HEBU TIZAMA MWENYEWE HAPO

8:03:00 AM Add Comment
 Video making ya wimbo huu imefanyika chini ya director EDDYSON wa Creative Mind Tz. Utengenezaji wa video hii umekamilika tar 27/4/2014...... video hii inategemewa kutoka mapema mwezi ujao kabla mwezi wa 6

STAY CONNECTED na TTM ili kufahamu Video Hii iko Vipi. Ni Noumar Mazee...Pia Soon Tutakuletea TEASER ya Video hii kutoka kwa Msanii THE KISSER-STRAWBERY






























WAZINZI, WEZI, KUNA ADHABU YENU IKO HAPA

6:30:00 AM Add Comment

Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.

Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.

Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.

Sheria hii itatekelezwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.

Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.

Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.

Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.

Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.
Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.

Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.

Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.




RIPOTI YA KITENGO CHIMBUA CHIMBUA-UGOMVI WA P SQUARE UMEZUA MAKUBWA MAWILI

4:59:00 AM Add Comment

KWA MUDA wa Wiki Kadhaa, Ishu ya Kugombana kwa Ndugu watatu, PETER,PAUL (P SQUARE) na JUDE OKOYE ambaye ni kaka yao, Zimkuwa Zikivuma sana Huku na Kule, huku baadhi wakibaki kustaajabu kuhusu Mtiti Huo.

CHANZO ambacho kilidaiwa Kuwakosanisha watatu hao, ni pamoja na Mke wa Peter, anayefahamika kwa jina la LOLA, ambaye huwa hana maelewano mazuri na JUDE

Lakini baada ya Info hizo kuzagaa kila kona na kuwaacha watu wakiamini ule Msemo wa NDUGU WAKIGOMBANA, BEBA JEMBE KALIME, Hatimaye yakazuka Mengine kuwa huenda wawili hao wakapigana Chini, huku Judee ambaye amekuwa kama Meneja na Director wa Video za kwa Miaka 10, akitweet kuwa anaachana na Shughuli hizo ikiwa ni baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu

Kiujumla Kitengo hiki amininfu kilipata Info nyingine kuwa, kampuni ya Simu za Mkononi iliyokuwa ikifanya nao Kazi, ilikuwa na Mpango wa Kumwagana na P-SQUARE endapo Watashindwa kufikia Muafaka, na Kundi hilo kuvunjika kama sio Kusambaratika.

Baada ya Siku Kadhaa, hatimaye zikaibuka Details Nyingine kuwa, watatu hao wamemaliza Ugomvi wao na Kila Kitu Kiko sawa, huku Jamaa ambaye ni Mtoa Taarifa wa Kundi Hilo (PUBLICITY) akifungua ukurasa Mwingine kwa kudaiwa kuwa ETI alisema ishu hiyo haikuwa ni ya Kweli, bali ilikuwa ni SKENDO ili kutambulisha Ujio Wao mwingine, jambo ambalo jamaa mwenyewe amelipinga

SASA Basi….Baada ya hayo Kuvuma, hatimaye KITENGO kimebaini kuwa Ugomvi Ule Umesababisha mambo Makuu Mawili yafuatayo:

1.    WAMEONGEZA NGUVU MPYA KATIKA KAZI ZAO
Tofauti hizo ambazo zinadaiwa kuwa ni Kweli zimetokea (kwa Mujibu wa Peter) hakika zimewapa nguvu kubwa sana ya kufanya kazi mpya, tena kwa bidii za dhati. Peter amedai kuwa wanatarajia kumimina kazi kibao Mpya.

2.    WAMEPATA MZUKA WA KUPIKA VIDEO YA TESTMONY

Ili kudhirisha kuwa Hakuna baya Linaloendelea baina yao, Peter amepost Tweet ikisema kuwa watu wanatakiwa kusikilizia video lao la TESTMONY, huku akipost Picha za Behind The Scene….





MAFIKI ZOLO WAMEMFUATA DAVIDO NIGERIA.

2:25:00 AM Add Comment

WASHINDI wa Tuzo 8 Za Muziki Nchi Afrika ya Kusini, MAFIKI ZOLO, wamefunga Safari kuelekea Nchini NIGERIA kumfuata Mtu Mmoja tu, ambaye wanaamini ana kitu kwao, DAVIDO

TTM Tumeunyaka Mtonyo huu kutoka Nchini Nigeria, baada ya kuzinyaka Picha zao wakiwa katika Jiji la Lagos ambalo huwa halipatikani sehemu nyingine zaidi ya NIGERIA.

Unaweza kujiuliza kuwa Sababu ambayo imewafanya kumfuata Davido Nchini humo, lakini bila kupoteza Time, TTM tumeinyaka pia, na sababu yenyewe ni Kutambulisha Ngoma ambayo Wamefanya pamoja na ilipikwa Huko kunako studio za Afrika ya Kusini..

Kwaju ambalo linatarajiwa kuzinduliwa na Vichwa Hivi pamoja na Davido, Linafahamika kwa Jina la TCHELETE, na wamesema kuwa wanatarajia makubwa sana kutoka kwa wadau wao wa Muziki.


Pia Wameongeza kiuwa, wamefurahi sana kutua LAGOS, sambamba na kufanya Kazi na DAVIDO, ambaye wote kwa Pamoja watakuwa naye Kunako TUZO za MAMA

MNADA BANNER