REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PROJECT STUDIO: KUTANA NA HARSHBASE RECORDS WAKIZUNGUMZIA STUDIO YAO NA NAMNA WANAVYOFANYA KAZI (AUDIO)

8:05:00 AM Add Comment

Na Baba Juti (@babajuti)
HARAKATI za Kufahamu Recording Studios ambazo zinapatikana Mitaa Mbali Mbali ya Jiji la Mwanza ndo Imeshaanza.

Dhumuni Kubwa ni Kuzipa nafasi Studio Hizi za Muziki kusikika, na hata kutambulika namna ambavyo wanafanya kazi.


Hii Pia ni kutoa Fursa kwa wao kuzungumzia Ugumu ama Changamoto wanayokutana nayo, bila kusahau undani wa Kile kinachofanyika katika Studio Hizo.

WIKI, Nimeweza Kutembelea Studio za Harsbase (Harshbase Records) zinazopatikana katika Mtaa wa BUZURUGA MITI MIREFU, Jijini Mwanza.

Wasikilize hapa


INAWEZEKANA ROCK TOWN IKARUDI KWA KISHINDO BAADA YA MABORESHO HAYA?

7:24:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
INAWEZEKANA Ujio wa ROCK TOWN RECORDS ukawa na Utofauti baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Kadhaa, ikiwemo kutokuachia Kazi Yoyote Mpaka hivi sasa

Chanzo Cha Studio Hiyo Kukaa Kimya, ni pamoja na Kufanya Ukarabati na maboresho kwa ajili ya Wateja watakoifika hapo kwa ajili ya Kufanya kazi.

Tofauti na maboresho, Rock Town Records Chini Ya Mkurugenzi Wake, Mkubwa Hermidou, Imekuja na Project ya T-Shirt ambayo ina Logo Mpya kabisa na za kibunifu- ROCK TOWN RECORDS.



Katika Logo hiyo, Kuna Jiwe Maarufu linatambulisha Jiji la Mwanz\a (Bismark Rock) hali inayoifanya kuwa Tofauti na Studio Nyingi za Mwanza

LAKE ZONE FRUITS: OBBY HUYU HAPA TENA !!

7:04:00 AM Add Comment

Na BABA JUTI
Mdogo Wangu Huyu Hapa Tena, Anaitwa Obby, anakuja na Brand Track Baada ya Mkwaju wa TENA, kufanya Vema kunako Kanda ya Ziwa.

Mabile Kwa Mabwale, Get Ready, nab ado unaweza kuupata Mkwaju wake katika Website ambayo itakuwa Uploaded.
Pia Tembelea Blog Hii kuupata Mzigo Huu

#Support

HII NDIYO ZAWADI AMBAYO H BABA KAMNUNULIA MWANAE TANZANITE KATIKA BIRTHDAY YAKE

6:53:00 AM Add Comment

MSANII wa “Bongo-Bolingo Flava”, H BABA, amedai kuwa amempa Zawadi ya Kiwanja, Mwanae wa Kwanza, TANZANITE  ikiwa ni ndani ya Siku yake Maalum ya Kuzaliwa, yaani Birthday.


Kupitia Ukurasa wake wa Face Book, H baba anadai kuwa, Dhumuni la Kufanya hivyo, ni kumpongeza Mama Yake (Mke wa H baba-Flora Mvungi) kwa Kumvumilia.


Hiki Ndicho alichoandika:


“MWANANGU @tanzanitehbaba NIMEMPA ZAWADI YA #KIWANJA #MAENEO YA MBEZI BEACH CHENYE UKUBWA WA #52 KWA 44 ZAWADI HII NI YA #birthday YAKE YAKUZALIWA KWAKE NAMSHUKURU MAMA TANZANITEONE KWAKUNIVUMILIA KUPATA MSHANGAO WA KIWANJA CHA MWANAE #HAKUTEGEMEA #KIUKWELI MBEZI BEACH UWANJA SIO MCHEZO KWAWANAOJUA THAMANI YA ARDHI #WANAELEWA NINI NAMAANISHA #SIWEZI KUMPA MWANANGU ZAWADI YA GARI KWASABABU #BADO MDOGO PIA KIWANJA KILA ANAVYOKUWA NAKIWANJA KINAPANDA #THAMANI ILA GARI #LINASHUKA THAMANI #NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWAKUFANIKISHA HILI KUBWA KWA MWANANGU @tanzanitehbaba haya haya walee wa mbezi beach #JIRANI YENU MPYAA”

NOT THIS TIME AGAIN… CHRIS BROWN ANAFUNGULIWA KESI TENA YA KUMPIGA MWANAMKE?

6:34:00 AM Add Comment

LETS hope kwamba Kila Kitu kitaenda Fizuri kwa Baba Royalty Himsefu, Chris Brown

Mwanamke mmoja amemtaja Breezy katika mashtaka yake, kwa Kuhusika Kumpiga na kuharibu Simu yake, baada ya Kusukumwa kutoka kunako Bas Tour la Mkali huyo wa LOYAL

Kwa Mujibu wa maelezo ya Bibie huyo, anadai kuwa Tukio hilo lilitokea SEPTEMBA 14, ambapo Bus Hilo la Chris Bizzo lilipaki Nje ya Strip Club ama Club ya Akina dada wacheza Utupu, kipindi ambacho FETTY WAP, Breezy na French Montana walikuwa wakifanya Video.

Mwanamama Huyo anaendelea Kudai kuwa, Alijikuta akisukumwa kutoka Ndani ya Bus hilo, na Kuanguka Nje kisha Simu yake Kuharibiwa, lakini ni baada ya Kuambiwa Kuwa haruhusiwi kuingia Ndani ya Basi hilo na Vitu kama Kamera, ama Kitu chochote Cha Kurecord, sheria ambayo iliwekwa na Chris na Watu wake


Jeshi la polis nchini marekani, wanafanya uchunguzi Juu ya Tukio hilo, nab ado wanahitaji kufanya mahojiano na Baba Royalty pamoja na watu wake

RICK ROSS AMESHINDWA KUFUA DAFU MBELE YA LMFAO

6:30:00 AM Add Comment

THE BIG BOSS Kutoka Ufalme wa MMG-Rick Ross, Mwaka huu unaweza kumalizika kwa Kupigwa Chini katika Kila madai anayofungua, huku yale anayofunguliwa dhidi yake, yakimkomba Mkwanja Mrefu.

Kama Utakuwa unafahamu tangia Kitambo, Rozay alifungua Mashtaka dhidi Ya Kundi la Pop Nchini Marekani, LMFAO, kwa Madai kuwa wanatumia Maneno yake, ambayo ni EVERY DAY I’M SHUFFLIN, hivyo anawataka kuacha kutumia Swagg hiyo, maana inatokana na maneno yake ya EVERY DAY I’M HUSTLING kunako Mkwaju wa HUSTLING

Kesi Hiyo ilifunguliwa Mwaka 2013, ambapo Rozay alikuwa anadai kuwa, Yeye Peke yake ndo ana haki ya Kutmia kauli Hiyo, na kitendo cha Kundi Hilo la LMFAO kufikia hatua ya kuprint mpaka T-Shirt ya Slogan Hiyo, ni Ukiukwaji wa hakimiliki Yake.

Lakini Hakimu ambaye alikuwa anaendesha Kesi hiyo, alimkata maini kabisa Rick Ross kwa kusema kuwa, hakuna haki Miliki ya Neno Hustin ambalo Rozay analalamikia, hivyo Kesi hiyo haina Mashiko.

Katika Kufafanua zaidi, hakimu Huyo, Kathleen Williams, amesema kuwa, Wimbo wa HUSTLIN alioutoa Mwaka 2006, utabaki na Hakimiliki ya Wimbo kama Wimbo, na Sio Neno ama Kauli Mbiu.


Katika Kutoa Mifano, Judge William alinukuu Misemo kama Vile “Holla Back”, “We Get It Poppin” na Mengineyo, kama vitu ambavyo havina Copyright lakini Vinatumika na Kila Mtu

MNADA BANNER