REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DIAMOND ! DIAMOND ! DIAMOND ! DIAMOND !..POLE KWA HILI

10:34:00 PM Add Comment




Richard Bukos, Dodoma GPL
KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.
Aibu hiyo ilimkuta staa huyo ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma ambako sukari huyo wa warembo alikuwa akifanya shoo.

AIBU YENYEWE
Aibu yenyewe iliyompata Diamond ilisababishwa na kuzimika kwa muziki wake mara tatu katika onesho hilo na hivyo kuwafanya mashabiki kupiga kelele huku wengine wakidai pesa zao za viingilio.


MAFUNDI MITAMBO WAHAHA
Hali hiyo iliwafanya mafundi mitambo kurekebisha nyaya kwa zaidi ya dakika 20 kila pale muziki ulipozimika hali iliyosababisha watu kuzidi kupiga mayowe na kumtolea maneno ya shombo Diamond, wengine wakitishia kumpopoa kwa mawe.

Muda mfupi baada ya mitambo hiyo kurekebishwa, mashabiki walianza kuserebuka tena lakini baada ya dakika 45 muziki ulizima tena na kusababisha mayowe mengine ya mashabiki wakiendelea kusema wameliwa pesa zao.

WEMA ATAKIWA
Katika zomeazomea ya safari hii,  mashabiki walikwenda mbele zaidi wakimtaka Wema apande jukwaani  kusalimia wakati mitambo ikirekebishwa wakiamini Diamond alikwenda na bebi wake huyo kwenye onesho hilo.

Hata hivyo, mafundi mitambo waliingia tena kibaruani na kurekebisha mambo baada ya dakika 23 muziki ukaendelea.


MAIKI NAZO ZAKOROMA
Diamond alianza kufanya tena makamuzi ndipo maiki nazo zikaanza kukoroma ambapo alianza kuwaomba wasaidizi wake wambabidilishie lakini kila waliyompa ilikuwa ikikoroma na kuwafanya mashabiki wazidi kupandwa na hasira.

Kitendo hicho kilimfanya Diamond asimamishe onesho na kuanza kumtupia lawama muandaaji (Matei) akidai kuwa ameshindwa kuweka hata betri mpya kwenye maiki alizomuandalia wakati amewatoza mashabiki kiingilio kikubwa cha shilingi 35,000 (kawaida) na 40,000 kwa VIP.

“Haiwezekani bwana, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu, mwandaaji gani unaandaa shoo, unawachaji mashabiki kiingilio kikubwa halafu unashindwa hata kuweka betri mpya kwenye maiki?





DIAMOND ABANWA NA RISASI JUMATANO
Kufuatia hali hiyo, baada ya shoo, Risasi Jumatano lilimfuata Diamond na kumuuliza kulikoni muziki wake kuwa mwepesi pia kukatikakatika kila mara huku maiki nazo zikikoroma.

“Braza huu muziki siyo kabisa, huu ni muziki wa kupiga kwenye vigodoro lakini siyo wa kufanyia shoo zangu hasa kama hii ambayo watu wameingia kwa bei mbaya, ni kuwaibia watu.

“Mimi ni mtoto wa Kiislam ni lazima niongee ukweli, niliposikia sehemu yenyewe ninayokuja kufanyia shoo inaitwa Matei Lounge nikajua ni sehemu bab’ kubwa lakini kumbe ni ubabaishaji mtupu,” alilalama Diamond.

INTAVYUU FUPI
Katika intavyuu fupi, Diamond, alisema anadhani kama anahujumiwa kwani haiwezekani muandaaji ashindwe kuweka vitu muhimu kwenye shoo. alidai wanafanya hivyo wakijua inapotokea tatizo kama hilo anayejulikana ni Diamond.

UJERUMANI, UINGEREZA
Ilianza nchini Ujerumani ambapo staa huyo alinusurika kudundwa kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili ya Agosti 31, mwaka huu baada ya kucheleweshwa kupanda stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart.

Nchini Uingereza nako, Septemba 20, mwaka huu, Diamond alijikuta ndani ya aibu kubwa kwa mashabiki wake kufuatia mwandaaji kuingia mitini katika ukumbi wa LafACE club jijini Londan licha ya mashabiki kujaa.


KASORO YA DAIMOND NI MAMBO YA ‘USWAHILI’
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa, Diamond licha ya kuwa msanii mkubwa kwa sasa lakini bado anaendesha mambo yake ‘kiswahili’ sana.

Kwa kawaida, msanii anapokwenda kupiga shoo mahali, kuna utaratibu unaoitwa kwa Kiingereza kama Technical Rider ambapo wasimamizi wake, akiwemo meneja huenda kuukagua ukumbi, usalama, muziki wenye viwango na hata steji shoo ilivyo.

Kama mambo hayo hayatakuwepo, msanii anaweza kugoma kufanya shoo. Lakini mambo yote hayo hutakiwa kuwepo kwenye mkataba wa makubaliano.Meneja wa Diamond, Babu Tale alipopigiwa simu juzi ili kuulizwa kwa nini hakuwepo Dodoma kuhakikisha uwezo wa vyombo vya muziki na maandalizi mengine, hakupatikana hewani!

NSSF YASHUSHA NEEMA KATIKA MBIO ZA ROCK CITY

7:52:00 AM Add Comment


Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 15 ili kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta (kushoto) katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. (Picha na DEWJI BLOG).

MWANZA, Tanzania
Zawadi za washindi wa mbio za Rock City zitakazofanyika katika mkoa wa Mwanza tarehe 26 mwezi huu zimetangazwa jana huku mdhamini mkuu wa mbio hizo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) likitoa shilingi milioni 15 kuboresha mbio hizo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano wa NSSF, Bw. Jumanne Mbepo amesema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizi kwa mwaka wa sita mfululizo kutokana na kuona maboresho yanayofanyika katika mbio hizo kila mwaka.

“Mbio hizi zitaambatana na kutoa elimu kwa wakulima na wachimbaji wadogowadogo wa madini katika kanda ya ziwa, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa NSSF ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na shirika kama vile mkopo, bima ya afya pamoja na mafao mbalimbali,” Alisema Bw. Mbepo.


Mratibu wa mbio hizo, Bw. Matthew Kasonta amesema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kuleta maboresho makubwa katika mbio za mwaka huu. Amesema kuwa maboresho hayo ni pamoja na kuwepo kwa mbio fupi zitakazo jumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo shule za msingi madarasa ya juu.

“Baada ya kupata udhamini huu, tunafaraja ya kutaja zawadi watakazopatiwa washindi. Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi wa pili watapata laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.
 
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2014 kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi. Anna Nguzo (Kulia). 
Kwa mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.”

Bw. Kasonta amesema kuwa kwa mbio fupi ambazo zimeanzishwa mwaka huu (mita 100, mita 400 na mita 1,500) jumla ya shilingi laki nne na themanini pesa taslimu zimetengwa kwa ajili ya washindi huku washindi wote wa kwanza (wa kike na kiume) watapata king’amuzi cha Continental Decoders.


Bw. Kasonta aliwataja wadhamini waliofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

 “Nawasihi watu waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za usajili katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza na Uwanja wa Nyamagana,” alisema Bw. Kasonta.



KUTIZAMA MECHI YA SIMBA VS YANGA, NI TSH 7000/-

7:40:00 AM Add Comment




 Tanzania Football Federation (TFF), Dar Es Salaam
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.


Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

MNADA BANNER