REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PONGEZI: KANYE WEST ANAFANYA VIZURI SANA SHUGHULI ZA KIJAMII

7:24:00 AM Add Comment

HAKUNA Mtu ambaye huwa anapingana na makali ya Sheria hasa ukizingatia marungu makali ambayo unaweza ukakutana nayo hapo baada ya kujifanya kiburi cha Wenye Viburi.

THIS time Sifa kali zimeshushwa ka Rapper Mkorofi na Mwenye Kiburi, KANYE WEST, baada ya kufanyiwa Tasmini katika Adhabu aliyopewa na mahakama, ya Kifungo cha Nje, pamoja na Kufanya Shughuli za Kijamii

Kwa Mujibu wa Info kutoka kwa Hakimu pamoja na Mwanasheria wa rapper Huyo Siku ya jana, Tasmini imedai kuwa, Rapper Kanye West anafanya Vema sana katika Shughuli za Kijamii, pamoja na Kujiweka Mbali na matatizo ambayo yanaweza kumsababishia hasira na hata kukiuka Makubaliano ya Adhabu yake

Moja kati ya Shghuli za Kijamii ambazo ameshafanya na kuvutia Wengi, ni baada ya Kanye kuhudhuria katika Mahafali Moja hivi ya wanafunzi wa Chuo Kinachojihusisha na Masuala ya Fashion, na kuzungumza nao kuhusu uzoefu alio nao katika Masuala hayo, ikiwa ni kuwaongezea elimu.


KANYE WEST ambaye ni Baba wa Mtoto North West mwenye Mwaka 1 na Mwezi Mmoja, alikutana na Ahdabu kali ikiwemo ya kuwa Chini ya Uangalizi wa Miaka Miwili katika Suala la Kupiga watu, hasa Waandishi wa habari, pamoja na adhabu ya kufanya Shughuli za kijamii ambapo ameshamaliza masaa 250, sanjari na kuhudhuria mafunzo ya kujua namna ya kucontrol Hasira zake, kwa muda wa masaa 24.

GARI YA MAREHEMU GURUMO, ALIYOPEWA NA DIAMOND, INAPIGWA BEI…….

7:20:00 AM Add Comment


IKIWA takriban ni miezi minne kasoro tangu gwiji wa muziki Muhidin Mohamed Gurumo ‘Maalim Gurumo’ aiage dunia, gari aina ya Toyota Fun Cargo alilopewa kama zawadi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdu ‘Diamond’ limedaiwa kupigwa bei.

Kwa Mujibu wa info ambazoTTM, inasemekana kuwa, chanzo cha Ndinga Hiyo kuingizwa Sokoni, ni baada ya kutokea Mvutano baina ya baadhi ya Ndugu wa Mke wa Marehemu, PILI NASSORO, ambao walifikia mpaka hatua ya Kufikishana katika Kituo cha Polisi.

Taarifa zaidi zimezidi kumiminika kuwa, kuna watoto wa Marehemu ambao walitaka kulipiga Bei gari hilo , Muda Mchache tu baada ya kumalizika kwa Masiba wa Marehemu Gurumo, lakini utata ulizidi kuwa mkubwa zaidi baada ya Mke huyo wa marehemu kutia Ngumu, huku akisemekana kuwa, Marehemu aliacha Wosia kuwa, pindi atakapofariki, Kadi ya Mkoko huo ikabidhiwe kwa Mkewe, maana kabla hajafariki alishajua tamaa ya baadhi ya Ndugu yake

Hata hivyo inasemekana kuwa, kwa Kulitambua hilo, Marehemu alimkabidhi  Kadi ya Gari, Meneja wa Diamond Platnumz, HAMIS TALE “Babu Tale” ili amkabidhi Mkewe (Bi Pili Nassoro) pindi atakapofariki.
Babu tale aliposakuliwa kunako Simu ili aseme hayo, alithibitisha kuwa ni Kweli Kadi ya gari la Marehemu Gurumo anayo, na alishapewa maagizo na Mke wa marehemu kuwa liwekwe Sokoni, hivyo Yeyote mwenye kutaka kulinunua, basi milango iko Byee


Diamond alimkabidhi marehemu gari hilo Agosti, mwaka jana katika Ukumbi wa Serena, Posta jijini Dar baada ya kuguswa na mchango mkubwa alioutoa Gurumo katika tasnia ya muziki nchini.

STAMINA..NA NAY WA MITEGO

7:12:00 AM Add Comment

LEO Ni siku ambayo another Mbwadidi linashuka kunako Music Industry hapa Bongo, huku ikithibitika kabisa kuwa, Nay na Stamina Walipeana makali katika Track ambayo wawili hao wamehusika.

Kwa mujibu wa maelezo ya Stamina ambaye ndiye mmiliki wa Track hiyo, amedai kuwa Mkwaju huo ambao leo ndo unaingia sokoni, utazua utata mkubwa sana kwenye game la muziki hapa Home, ukizingatia wawili hao wamechanana kiukweli.

Aidha Stamina ameongeza kuwa, Track hiyo ni ya majibishano, ambapo Nay wa Mitego ameact kama Msanii ambaye alikuwa anafanya Hip Hop lakini kwa sababu yeye amejikita zaidi kwenye kusaka hela, basi hivi sasa kaisaliti Hip Hop, huku Stamina “Shorobwenzi” Himself amesimama kunako Hip Hop ambayo yuko nayo mpaka Hivi sasa.

Pia kwa mujibu wa majibishano hayo, basi wawili hao wanatoa taarifa ama details za aina ya Muziki wanaoufanya, kitu kinachokamilisha jina la Track hiyo HUKO KWENU VIPI.

Rapper huyo amesema kwamba, wameamua kuiachia kwa haraka ngoma hiyo iliyofanyika siku tatu zilizopita katika studio za MR. T-TOUCHEZ, kwa sababu vitu walivyoviongea ni vitu vya muda huu kwa hiyo hawataki kukawia kwa sababu mambo yanaweza kubadilika.


STAMINA amemalizia kwa kusema kuwa, kuwa katika ngoma hiyo Nay amefanya ubabe wa maneno bila kuogopa kutaja majina ya watu na kwamba hata yeye (Stamina) amefanya hivyo kwa kuwa makubaliano yao yalikuwa kuchanana bila kuogopa.

MNADA BANNER