REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MY SUPPER MEMORY OF THE DAY

2:54:00 AM Add Comment

BY FRANK M. JOACHIM.
I and My Class Mate Rachel Vummu, it was a Valentine's Day Special Party in our Class room, in This Year of 2012. I was giving her a piece of Cake which was special for all Clas Mates.
That was before graduating our Diploma Studies at ROYAL COLLEGE OF TANZANIA-RCT
Soon we shall be to gether in our Graduation Ceremony in 08th December of 2012.
I miss Her and all My Class Mates

MNADANI LEO : WAITING FOR MY GRADUATION

2:32:00 AM Add Comment
Na Frank M. Joachim "Hasta La Vista Baby"
 *****************************************
Hakuna Kitu ambacho ninakisubiri kama kuipokea Rasmi Diploma yangu ya Journalism and Broadcasting ambayo nimeisotea kwa Muda wa Miaka Miwili katika Chuo cha Royal "ROYAL COLLEGE OF TANZANIA-RCT"

Finaly Ndoto zangu Zitatimia kiasi cha kunifanya niungane na Swahiba wangu wa Kitambo NAH ABOUD JR katika Tasnia ambayo tulikuwa Tuitamani kwa muda Mrefu

NAWAPONGEZA WAFUATAO KATIKA JOHO LIJALO.
*****************************************************************
Wafuatao ni Class Mateswangu ambao Siku hiyo tutajaa Nyuso zenye Furaha.
1. Samwel Thomas
2. Rachel Vummu
3. Brian M. Thomas.
4. Yvone Mussa
5. Safiya Mohammed.
6. Khatim Naheka
7. Gladice Sigella
8. Joyce Buganda
9. Faster Gilbert
10. Grace G. Nkungu
11. Honesta Mzava
13. Emiliana David.
14. Haroun Kijazi
Sote kwa Pamoja tulikuwa katika Darasa Lililoitwa "Diploma May Intake 2010" na tukajipatia Title la "HEAVEN OF PEACE"

CHADEMA INAMVUTIA KASI KIKWETE

2:15:00 AM Add Comment





Na: Edson Kamukara

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwataka makada wa chama hicho kujibu mapigo ya wapinzani,akidai wanafanya kazi ya kueneza uongo na kupotosha wananchi, CHADEMA imesema inamvutia pumzi kabla ya kumjibu.Akihitimisha mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma juzi usiku, Rais Kikwete aliwataka mawaziri na makada wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara na kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za wapinzani badala ya kutegemea nguvu za Jeshi la Polisi.

 Huku akionekana kukasirishwa na kasi ya CHADEMA, Rais Kikwete alimtaja wazi wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kuwa aliwahi kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.

“Slaa aliita mkutano akasema mimi, mwanangu Ridhiwani na Rostam Aziz tulikutana kwenye hoteli moja jijini Mwanza, huku akijua siku aliyoitaja mi nilikuwa kusini nikiendelea na shughuli zangu,”alisema.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya upinzani,watu wazima hovyo,wanasema uongo mbele wananchi na hata wakati mwingine kwenye vyombo vya habari wakinukuu takwimu za uzushi.

Alipoulizwa jana kuhusu madai hayo ya kueneza uongo kwa wananchi,Dk.Slaa alicheka kisha akasema:“Tunawatafakari na tutawajibu,ila siyo leo, wala hatuna haraka.

 “Mimi kwa kweli sikusikiliza hotuba yake, na hata mkutano wa CCM sijaufuatilia, ila kama Kikwete kasema hayo unayoniuliza, basi tutamjibu kwa utaratibu rasmi wa chama, leo sisemi kitu.

“Sisi ni watu makini, tunaamini katika kile tunachokisema wala wasipaniki, tutawajibu.
  Maana wanadhani tunapoteza muda kufuatilia mkutano wao,nilimsikia hata Nape Nnauye akisema juzi kuwa anajua tumeacha kazi tunawakodolea macho,”alisema.

Dk.Slaa alisema kauli ya Nape ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC),Itikadi na Uenezi wa CCM,inachekesha, kwani CCM ya wao kuacha kazi zao na kuikodolea macho ilikuwa ya zamani si hii ya leo.
Katika kile kinachoonekana kama CHADEMA kuinyima usingizi serikali na CCM,

 Kikwete aliagiza mawaziri wote kujiwekea utaratibu wa kila mmoja kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya serikali katika vyombo vyote vya habari.

Alisema kwa vile viongozi wa chama na serikali hawajibu taarifa za upotoshaji zinazotolewa na wapinzani, wananchi wanapozisikia zikirudiwa rudiwa bila kukanushwa wanaziamini.

CONFIRMED : LINA NA AMIN WAMESEMA HIVI KUHUSIANA UHUSIANO WAO KWA SASA

1:42:00 AM Add Comment


Siku za hivi karibuni Amini na Linah ambao wamewahi kuwa wapenzi na hatimaye kuachana, wamekuwa karibu mno kiasi cha watu kuanza kuulizwa maswali kama wamerudiana tena. Leo November 15 wanaachia wimbo wao mpya waliofanya pamoja na ambao waliurekodi siku ya kuzaliwa ya Amini October 30.


Katika fainali za BSS zilizofanyika Ijumaa iliyopita,Amini na Linah waliimba pamoja na kushangaliwa mno kutokana na jinsi walivyokuwa wakiimba kama mtu na mpenzi wake. Ukweli ni upi? Wamerudiana ama ni marafiki tu? Tumewatafuta na kufanya nao mahojiano mahsusi ili kuyarusha leo siku wanayoachia wimbo wao ili wauseme ukweli.


Katika mahojiano haya Linah ameanza kwa kusema kuwa lengo la wao kufanya wimbo wa pamoja ni kukata kile anachokisema ‘kilimilimi’ cha watu kuwa yeye na Amini hawazungumzi tena baada ya kuachana. “Kulikuwa na maneno mengi sana kwamba mimi na Amini hatuelewani, hatupatani, hatuna mawasiliano mazuri,” anasema Linah.

“Lengo kubwa la sisi kufanya hivyo vitu kwa pamoja ni kuwadhihirishia kuwa bado tunapendana (anacheka na kumuuliza Amini) Kwani ni Uongo? Amini anajibu, “Hakika unenalo ni sahihi”. Linah anaendelea, “Hakuna ukweli wowote kuwa tumerudiana au lah! Sababu kila mtu anafanya mambo yake na tunafanya kazi kama kawaida japokuwa upendo bado uko pale pale.”


“Tutazidi kuendelea kuwepo kwasababu hatukugombana, hatukukorofishana, hatujawahi kutukanana hata siku moja mawasialiano yako vizuri tu, “anasema Amini.

MNADA BANNER