REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BREAKING NEWS : WASTARA AREJEA KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA

11:04:00 PM Add Comment

Kwa Mujibu wa Mwandishi wa habari hizi aliyeko moja kwa moja eneo la Msiba , NAHCEEB ABOUD, Mke wa Marehemu Sajuki amerejea Nyumbani toka Hospitali ambako alikuwa amepelekwa kwa ajili ya Huduma ya kwanza baada ya Presha Kushuka.

Ingawa bado hali yake sio nzuri kiasi kwamba hawezi kuongea wala kufanya Chochote, Wastara imebidi arudi nyumbani ili kuuaga mwili wa Marehemu mume wake Kipenzi, kwani yeye ni Mtu muhimu sana katika Hatua hizi za Mwisho.

BREAKING NEWS : WASTARA YUPO KATIKA HALI MBAYA..

10:56:00 PM Add Comment

Mke Wa Marehemu Juma Kilowoko "Sajuki", na Muigizaji wa Filamu Nchini Tanzania, Wastara Juma, yupo katika Hali mbaya kutokana na Msiba wa Mume wake

Aidha chanzo cha Wastara kukumbwa na hali hiyo ngumu katika siku ya Mazishi ya Mwili wa Marehemu mumewe, ni Presha kupanda kutokana na kutokuamini kama mume wake Kipenzi leo ndio anapelekwa kupumzishwa.


Hivi sasa Sasa Wastara amekimbizwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma ili aweze kurejea katka hali yake ya kawaida na hatimaye kuhudhuria Mazishi ya Mume wake. Mpaka hivi sasa taarifa hizi zinachapishwa katika Blog hii, hali ya Wastara bado haijarejea katika ahueni, ukizingatia amekuwa karibu sana na Mume wake licha ya wawili hao kukumbwa na Misuko suko kadhaa.


Mwili wa marehemu Sajuki utapelekwa katika Msikiti wa Upanga kwa ajili ya Dua majira ya saa Sita Mchana, na hatimaye kwenda kupumzishwa katika Nyumba ya Milele.

MNADA BANNER