REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MUENDELEZO : SITOKI NA MR. NICE, NA HAITATOKEA - MISS WORLD KENYA

8:50:00 AM Add Comment
Baada ya kusemekana kuwa Mr. Nice ama LUCAS MKENDA anajivuta kwa Mrimbwende Nchini Kenya, basi hii, ndiyo kauli ambayo pengine itamkatisha tamaa kaka yetu Mr. Nice

SHAMIM NABIL - “I respect everyone’s feelings and sentiment. But for me to date Mr Nice just sounds like a bad joke . I am not even giving this a thought. Hell no!, I used to hear of him when i was pretty small. Nothing personal, but i think we come from different generationAs”

LONDON: MKUTANO WA AMANI YA SOMALIA WAANZA

8:30:00 AM Add Comment
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameandaa mkutano wa kimataifa jijini London utakaojadili njia za kuisaidia Somalia kumaliza zaidi ya miongo miwili ya machafuko.






Mkutano huo utajikita zaidi katika masuala ya kujenga upya vikosi vya ulinzi na kukabiliana na ubakaji ambalo ni suala linalooonekana kama mwiko.

Somalia inatafsiriwa kama taifa lililoshindwa, lililokumbwa na vuguvugu la wanamgambo wa Kiislamu, uharamia na ukame tangu mwaka 2010 hadi 2012.

Takriban watu saba waliuawa katika mlipuko wa bomu kwenye gari uliotokea katika mji mkuu Mogadishu siku ya Jumapili. Kundi la Al – Shabab ambalo lina mafungamano na Al – Qaeda linadai kuhusika na shambulio hilo.

Mkutano huo ambao utakua chini ya uenyekiti wa Bw. Cameron na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamoud unafuatia mkutano kama huo uliofanyika London na jijini Istanbul nchini uturuki mwaka jana, huku wasiwasi ukiongezeka katika jumuiya ya kimataifa kwamba Somalia imegeuka hifadhi ya wanamgambo wenye mahusiano na al Qaeda.

“Ninamatumaini kwamba, wote tunaweza kuafikiana kuhusu mpango wa usalama wa muda mrefu, ambao utamaliza vitisho vya Al Shabab moja kwa moja,” alisema Bw. Cameron.

“Pia ninamatumaini tutaboresha uwazi na uwajibikaji ili watu wafahamu wapi rasilimali zinakwenda. Pia tunahitaji kuendelea na mchakato wa kulijenga taifa la Somalia, ikiwemo mikoa yote ya Somalia na nchi jirani hali kadhalika.”

Mchambuzi wa masuala ya Somalia wa BBC, Mary Harper anasema, kumekuwa na mabadiliko ya ghafla nchini humo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

MNADA BANNER