REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HUDDAH : MOUSTAPHACOLONEL SIYO TYPE YANGU, NA KILA MTU ANALIJUA HILO

6:20:00 AM Add Comment

ZA FASTA ambazo zimelifikia “Suppa Room” la TTM ni Kwamba hatimaye Huddah amemtoa Nishai aliyekuwa anasadikika kuwa Mpenzi wake MOUSTAPHA COLONEL ambaye Hivi majuzi tu alijitapa kuwa hawezi Kumwacha Huddah.

Kwa Mujibu wa Interview ambayo amefanya katika Kituo cha Televisheni Nchini Kenya, KTN, HUDDAH amedai kuwa, hayuko katika mahusiano ya kimapenzi na COLONEL, bali hali hiyo ilitokea baada ya Kuambiwa kufanya hivyo na Moustapha mwenyewe.


Aidha Huddah alizidi “Kumiminika” kuwa, hakushtushwa na mitonyo hiyo ilivyokuwa ikizagaa siku hadi siku..

“Simfahamu MUSTAPHA, Sifahamu anakoishi. Kwa Mara ya Kwanza Tulikutana katika Zoezi la Upigaji Picha, na Kisha tukaelekea katika Interview na KTN. Lakini Kitendo cha kumuona akifanya Interview sehemu kibao akizungumzia mien a yeye kuwa na uhusiano wa Kimapenzi, kimeharibu sana jina langu, kwa sababu Moustapha na OGOPA DJ, ni Meli inayozama baharini. Hivyo walifanya hivyo ili kurudi kwenye game kupitia Jina langu.” Alisema Huddah


Tofauti na Hilo, Huddah ambaye aliiwakilisha nchi ya Kenya katika Shindano la BIG BROTHER AFRIKA Mwaka 2013, aliamua kuvunja ukimya na Kudai kuwa MOUSTAPHA Kamwe sio Type yake hasa katika Suala la “Kubiringika”

“Ninaomba kuliweka sawa hili suala. Moustapha Siyo Class yangu hata kidogo na kila mtu analijua hilo. Siwezi kudate naye . hata siku ile nilipoulizwa swali la kuhusu kutoka na Mustapha, nilicheka sababu nilijua kinachoendelea, na niliambiwa nifanye hivyo” alimalizia kabisa Huddah.


SO……KIFUATACHO?..Tumsubiri Moustapha na OGOPA DJS

MISHE ZA MPITA NJIA: WASIKILIZE WAHUDUMU WA BAR WALIO KATIKA UMRI MDOGO JIJINI MWANZA

4:45:00 AM Add Comment

MZEE WA MIAKA 60 AGONGWA NA DALA DALA MBILI JIJINI MWANZA

4:09:00 AM Add Comment

Marehemu Mihayo Ngofa anaye kadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 65 hadi 70 aligongwa na daladala ya kwanza iliyokuwa ikitokea mjini kati kuelekea Igoma na kisha kugongwa na daladala nyingine ambapo zote zilikuwa zikipishana kwa wakati mmoja nyingine ikitokea Igoma kuelekea mjini kati.

Mara baada ya tukio hilo daladala hizo hazikusimama ziliunganisha safari zake kwa mwendo wa kasi bila kufahamika zilipoishia.
Vielelezo vinaonyesha kuwa marehemu alikuwa akitoka sokoni kuinunulia mboga familia yake.


Tukio hili linatokea wakati Wakandarasi wa wa ujenzi wa daraja la kivuko kipya cha juu cha watembea kwa miguu kikiwa katika hatua zake za mwisho kukamilika na kuanza kutumika.


CREDIT: ZEPHANIA MANDIA

HAPPY BIRT DAY MY FRIEND VICTOR MGENI

3:14:00 AM Add Comment

LEO ni siku ya Kuzaliwa ya Swahiba wangu na mdau Mzuri sana wa BLACK TOUCHEZ BLOG, JAM SESSION, TTM na METRO FM 99.4 MWANZA.

Victor Pia ni Mmoja kati ya Lile Crew la ROCK CITY EYE MAGAZINE ya hapa hapa Jijini Mwanza Tanzania, pamoja na Ishu za MODELING

HAPPY BIRTHDAY VICTOR MGENI “ASTARAVICTOR”

H.BABA IS BACK

2:10:00 AM Add Comment

MKALI wa Bongo Blingo Fleava, H-BABA, ameamua kuja kwa Nguvu katika Gambaada ya kukaa kimya kwa muda.

KAMA Ulikuwa hujui, H.BABA ambaye amewahi kufunika EAST AFRIKA  na kwaju la MPENZI BUBU, This Time amerejea na Mzigo Matata ambao uko katika Style yake hiyo hiyo ya BONGO BOLINGO FLEVA, inayofahamika kwa jina la TUBEBANE…


H BABA hivi sasa ni Baba wa Mtoto mmoja ambaye amempata akiwa na Muigizaji wa Filamu Nchini, FLORA MVUNGI

NATTY E NA "HAINAGA NOMA"

1:55:00 AM Add Comment

EDNA ELISHA "Natty E"  rappa wa Kike Representing Mwanza (ROCK CITY) ameamua Kurejea Upya, baada ya Kufanya Kufuru kupitia Track yake ya VUTA TASWIRA aliyomshrikisha KALA JEREMIA 0444 na NURU MUSIC

Natty E ameiambia TTM Kuwa this Time amekuja na Brand New Track, Brand New Mzuka, Brand New Flow, with Brand New Hasira  kwa ajili ya kurejesha Heshima ya akina dada ambao bado wanaonekana kusahaulika katika HIP HOP MUSIC hapa Nchini tanzania.

Ngoma Mpya ambayo "The Rap City Chick" atakuja nayo itafahamika kwa Jina la HAINAGA NOMA ambayo amemshirikisha Mwanadada Mwenzake ZED-Y katika Chourus, na Studio ambayo imepika Mkwaju huo ni FINE TOUCH AUDIO LAB huku Mkono uliotumika kusukuma kila Kitu ukiwa ni wa Kazimoto “KAZI 2 THE FIRE”

Aidha NATTY E ameongeza Kuwa, Ijumaa ya March 21, HAINAGA NOMA Itaachiwa Rasmi kupitia Vituo Mbali mbali ikiwemo Metro FM 99.4 Mwanza katika Kipindi cha Jam Session, pamoja na Mitandao mbali mbali ya kijamii ikiwemo BLACK TOUCHEZ BLOG

Hivi sasa Natty anafanya Vema katika Track ya Kundi la WAKUMBWA WA JIJI, inayofahamika kwa Jina la ZIPATE TUKUJUE akiwa na KING SILVE na OP MTATA.

STAY TUNED MAZEE

CHRIS BROWN ALIFANYA MAPENZI NA MWANAMKE NDANI YA REHAB

1:02:00 AM Add Comment

BAADA ya kusambaa kwa Info za UHAKIKA kuwa Mkali wa R&B na POP, Chris Brown atatupwa Jela kwa Muda wa Mwezi Moja baada ya kukiuka Sheria za Rehab alikopelekwa kwa ajili ya matibabu ya tatizo la Hasira, limezuka lingine tena ambalo ni muhimu kulifahamu.

TTM tuliponyaka hizo info, ilitubidi kufuatilia kiundani zaidi sababu ambayo ilimfanya Breezy haswa, akafukuzwa Rehab, mpaka “Kuswekwa” Jela kwa Muda wa Mwezi Mmoja.

Kwa mujibu wa Chanzo ambacho kimethibitisha kile ambacho tumekipata na tunatarajia kukutaarifu, ni kwamba eti, Chris Brown alifikia mpaka hatua ya kufanya Mapenzi na mmoja wa wanawake , wakiwa ndani ya Rehabu , kitu ambacho kilikuwa ni ukikwaji wa sheria ya kukaa mbali na mwanamke yeyote akiwa hapo.


Aidha Chanzo hicho kimeongeza kuwa, Kutokana na kosa hilo, Mkali huyo wa DEUCES alikiuka ,asharti ya Rehab na Mahakama, jambo ambalo lilimfanya atimuliwe na Mahakama kumtupa Jela Mwezi Mmoja

KANYE WEST AKUMBWA NA GONJWA LA CHRIS BROWN..

12:55:00 AM Add Comment

KUTOKANA na Tukio ambalo lilitokea Mnamo JULAI 2013, kumpiga  PAPARAZI Mmoja huko LA, Nchini Marekani, Hatimaye mahakama imetoa hukumu yake kwa Msanii huyo ambaye alilalamika kuwa yeye ndiye aliyekosewa..

TTM tumebaini kuwa Rapa Huyo wa Chicago alibainika kuwa na Makosa, jambo ambalo lilimfanya akumbane na adhabu ya Kuwa Chini ya Uangalizi wa Miaka Miwili dhidi ya Matukio ya Aina hiyo.

Tofauti na Adhabu hiyo, YEEZY amekumbana na adhabu ya kufanya Shughuli za Kijamii kwa Muda wa Masaa 250, pamoja na Kuhudhuria Msaada ama huduma ya kupunguza ama kukabiliana na Tatizo la Hasira (Hunger Management) kwa Muda wa Masaa 24.

Baada ya kuinyaka hilo, Finally TTM tumebaini na hata kuamini kuwa KANYE WEST huenda akawa na tatizo kama La Chris Breezy ingawa lake halifikii kipimo hicho.

Duh..Balaaaaa

OCTOPIZZO MPAKA BERLIN, UJERUMANI

12:47:00 AM Add Comment

REPRESENTING 254 (KENYA) Rapa Octopizo anatarajia kuelekea Nchini Ujerumani kwa ajili ya kuutangaza Muziki wake na Nchi yake Kiujumla.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kunako Ukurasa wake wa FACEBOOK, okto amesema kuwa bado wiki mbili aelekee katika Tour yake hiyo katika Jiji la Berlin ambayo itamkutanisha na Mashabiki zake..

TTMM tumeipata Nukuu yake kuhusu Tour Hiyo Hii Hapa, Direct kutoka kwa Page yake Mwenyewe


THE SPOKEN WORLD #BLACKSTAR BERLIN TOUR IS HERE! 2 WEEKS TO GO, I’ve come to believe that all my past failure and frustration were actually laying the foundation for the understandings that have created the new level of living I now enjoy.#LEVEL & #LANES,Few things in the world are more powerful than a positive push. A smile. A world of optimism and hope. A ‘you can do it’ when things are tough.

MNADA BANNER