REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ISABELA DOS SANTOS : MTOTO WA RAIS WA ANGOLA< ANAYEONGOZA KWA UTAJIRI BARANI AFRIKA

11:56:00 PM Add Comment
IKO HIVI...
ISABELA DOS SANTOS kifungua Mimba wa Rais wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, ndiye Billionea wa Kwanza Barani Africa, yaani hakuna Tajiri mwingine katika Nchi yoyote ile Africa anamshusha bi Mdada huyu kwa kuwa na Mkwanja Mrefu




Hiyo inatokana na Jarida la Kiuchunguzi la Forbes, ambapo inasemekana kuwa, Mrembo huyo amekuwa akinunua hisa mbali mbali katika Mkampuni mbali mbali Nchini Portugal, ukijumuisha Hisa za BENKI na CABLE TV COMPANY. Kwa kujumisha hayo, inaonesha dhahiri kuwa , Mrimbwende huyo anaweza kumiliki Benki Moja Nchini Angola.





WABUNGE WAANGUA VILIO

11:24:00 PM Add Comment


WABUNGE waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu zilizotokea Mtwara juzi; Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana waliangulia vilio walipotakiwa  kuzungumzia tukio hilo.
Nyumba za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali zingine kadhaa za taasisi mbalimbali, ni miongoni mwa vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo pia zilisababisha vifo vya watu wanne wilayani Masasi.
Akizungumza kwa huzuni,  Anna alisema hajui sababu za uharibifu huo, hasa ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu siku tatu na hakuona dalili za uhasama wowote dhidi yake.
Anna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho alisema: “Nina siku ya tatu hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa halmashauri kwa mwaliko na wakati wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi kujua sababu ya chuki iliyofanya nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.
Alipotakiwa aeleze hali ilivyokuwa, alisema, “Wavamizi hao walipora kila kitu nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla ya kumwaga petroli kila chumba na kuwasha moto.”

Aliendelea kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia uchungu kwani nyumba hiyo niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”
Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.


“Hali si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba imechomwa moto, hakuna kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua muda mwingi kujua thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.
Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”
Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.
“Wamepora kila kitu katika nyumba na kuichoma moto, sijui atakuwa nani huyu, kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na sina mgogoro na mtu yeyote. Nashindwa hata kuhisi nani kafanya uchochezi,” alisema Kasembe.

Alisema wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo mama yake, walikimbia na kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa hawajui wataishi vipi baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.
“Jana wanafamilia walilala hotelini na leo tupo nje ya gofu la nyumba yangu ambayo imeteketea kabisa kwa moto, tunasubiri majaaliwa mengine, lakini nimechanganyikiwa kwa kweli na sijui ni kitu gani hiki, siamini,”alisema.
Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu mkubwa mali.
CHANZO : MWANANCHI

MAANDAMANO NCHINI MISRI JANA YALIKUWA KATIKA STAILI HII

11:07:00 PM Add Comment
 Mmoja wa wa Vijana walioandamana jan Nchini Misri akiwa katika Style kai ya Kuandamana, huku akionekana kurusha Jiwe, na Suruali ikiwa chini...

Waandamanaji wakipambana na Jeshi la Polisi

KUTOKA KENYA

11:02:00 PM Add Comment

Tume huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka IEBC Jumapili imetoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa vyeti bandia ambavyo inadai vimekuwa vikisambazwa jijini Nairobi na vinadaiwa kutolewa na tume hiyo.

Kulingana na IEBC vyeti vitatolewa na IEBC baada ya vyama kuwasilisha vyeti vya uteuzi, na wagombezi wa viti mbalimbali. IEBC inatarajiwa kutoa vyeti kwa wagombezi wa urais tarehe 29 na 30. 

Watakaowania nyadhfa za ugavana, useneta na wawakilishi wa wanawake katika kaunti na wengine watawasilisha karatasi zao za uteuzi tarehe 31. IEBC imebaini kwamba vyeti hivyo bandia ambvyo vinasambazwa vina maelezo bandia ikiwemo sahihi ya mwenyekiti wa IEBC Isaac Hassan na baadhi ya wakuu wengine.

Tayari IEBC imewaarifu maafisa husika wa usalama na mshukiwa mmoja ametiwa mbaroni.

MNADA BANNER