REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

EMMY'S LAMODA: LADIES, UFANYE MTOKO WAKO WA WEEKEND UWE HIVI

7:43:00 AM Add Comment




KUNA HILI LA KUJUA KUTOKA KWA HUYU JAMAA... SOMA HAPO..

7:31:00 AM Add Comment

WIKI Ijayo Itakuwa ni Chance ya Wewe kumfahamu ABDALLAH “OXS” OKELEKY ambaye ni RAPPER, akiwakilisha Jiji la Mwanza.

Oxs ambaye ni Producer wa METRO FM 99.4 – Mwanza, na Presenter wa Kipindi Cha RIDDIM ROCKERS kinachoruka Kila Jumamosi katika kituo Hicho, ameanza Michakato ya Muziki Muda Mrefu na ameweza kufanya Nyimbo Kadhaa.

Tofauti na Hilo, OXS anayefahamika kama BIG DADY, pia amehusika kunako Collaborations Mbali mbali na wasnii Tofauti akiwemo GODFREY TUMAINI Maarufu kama DUDU BAYA, pamoja na wengineo wengi ambao wana jina Kubwa tu hapa Nchini Tanzania.

Kuanzia Wiki Ijayo, Mikwaju Lukuki ya Oxs, itaanza Kuflow kunako BLACK TOUCHEZ, na kusambazwa katika Mitandao Tofauti ya Kijamii.
Get Ready For This, na Kwa Shughuli Nyingine kama utahitaji kumhusisha, Basi, NEXT WEEK kila kitu Kitakuwa Wazi.


ROCK CITY CHAT: WAKUBWA WA JIJI, TEGA SIKIO BOYS WAMESHUKA, SPEED YA MO MUSIC INATISHA

7:16:00 AM Add Comment

This week bin Wiki hii TTM tumeweza kustick kunako jiji la Mwanza na kuona kuwa Yes, Mbadidi la Kumwaga lipo katika Mikwaju ambayo inazidi kukita kupitia jam session na hata vipindi vingine.
Ni nafasi tamu ya Kuzihesabu zile 5 ambazo zinafanya Byee kunako Metro Fm kwa Muda wa Wiki Nzinma, nikimaanisha Swagalinyu za Kuanzia Jumatatu Mpaka Ijumaa

5. HONEYA- UWE WANGU
Wiki hii katika nafasi ya tano TTM tumemnyaka This Beautiful Lady mwenye vocali tamu linalohamasisha kukubali kazi yake. Kwa mujibu wa Info kutoka kwake ni Kwamba hivi sasa tayari ana Package kubwa ya Mikwaju ambayo ameshaiandaa tayari kwa kuliteka Soko la Muziki. Bibie huyu ameshafanya Tracks za kutosha na DEEY CLASSIC kutoka revolution Sound, DONCHA MASTER ambaye hatujui kama still yuko OVER CLASSIC, na hivi sasa anapiga Projects nyingine na TIDDY HOTTER wa ONE LOVE FX, pamoja na LOLLIPOP wa K- RECORDS.
Good Info ni Kwamba, Sauti yake hivi sasa inakita Vizuri kunako Nchi ya Kenya na Cannada, baada ya kupiga Chourus tamu akiwa na JAMAA TU FULANI, MKENYA mwenye Maskani yake CANNADA, kunao Track ya FREEDOM ambayo Natty E, kashusha Verse Pia.
Ladies and Gentlemen, katika Nafasi ya Tano, Track ya UWE WANGU kutka Kwa Honeya.


4. ZIPATE TUKUJUE- WAKUBWA WAJIJI
Wakiwa bado wanazidi kukomaa na game, this time Kutoka ROCK CITY Mwanza hapa hapa, wameshuka kutoka nafasi ya Pili mpaka nafasi ya NNe na Track yao ZIPATE TUKUJUE.

Mpaka hivi sasa kunako Mtandao wa YOUTUBE, Video ya Wimbo huu imeshatizamwa na watu zaidi ya Miamoja kutoka sehemu Kibao Hapa Duniani.

Kwa mujibu wa Info za Chini Chini Tu, ni kwamba Vichwa hivi Vilikuwa vimejichimbia kwa ajili ya kujipanga na Shows ambazo soon , huenda zikaanza kumiminika.

3. TEGA SIKIO- K- STAR, NCHAMA THE BEST NA BRYTONE.
BIG UP SANA Kwao watatu hawa Kwa kuzidi kuonesha Uwezo wao wa hali ya Juu tangia wamefanikisha kuisukuma kazi hii ikiwa ni Track yao Kwanza kabisa.
.Lakini Guud info ambazo still TTM tunazidi kuziamini ni Kwamba Vichwa hivi vitatu, K-STAR kutoka Pasiasi, NCHAMA THE BEST kiutoka Bugarika, na BRYTONE representing Sengerema, Vinatarajia kushusha Tracks Nyingine ambazo zirtkuwa ni Balaa pengine kuliko hata hii iliyoko kunako nafasi Hii ya tatu

2. BASI NENDA- MO MUSIC
Hakuna ambaye atabishana na TTM kuwa Moja kati ya Vijana ambao wanasauti Nzuri na Ya kujivunia Ni huyu jamaa. Off Course ni Kwamba VIDEO yake ambayo ina wiki Moja tu ikiwa Imewekwa katika mtandao waYOUTUBE, imetizamwa  na Watu zaidi ya 1000, huku audio Ikipata Airtime kali ya kutosha kunako Media mbali mbali Nchini Tanzania
Lakini, kama Ulikuwa Hufahamu, this Bway ni Ex- Memba wa Kundi la wakubwa wa jiji.

Katika nafasi ya pili Kimwanza mwanza, wiki hii, Mo Music, na Track ya BASI NENDA.

1.HAINAGA NOMA- NATTY E
Katika nafasi Hii, wala huwa hainipi Noma, coz Mhusika Mwenyewe hanaga Noma, Track yenyewe hainaga Noma, na hata Producer aliyehusika Hanaga Noma.
Ikiwa ni baada tu ya Kuachia Mbwadidiz kibao ambazo zimempatia heshima yake, This Time amekuja Kwa Level Nyingine, na Mzuka Mwingine.

Tofauti na hilo, Kipaji cha Mamito huyu kimedhihirika baada ya kukatanishwa na JAMAA TU FULANI, na hatimaye kupika Track ya Freedom Chini ya Deey Classic, na mwisho wa yote kila Kitu kikawa Byee

Ladies andGentle men, katika Nafasi ya Kwanza Wiki hii Kutoka hapa hapa Rock City, NATTY E, HAINAGA NOMA.



2 CHAINZ KUPANDISHWA MAHAKAMANI JUMA LIJALO

6:48:00 AM Add Comment

MIEZI 10 liyopita Rapper 2 Chainz alikutwa na msala wa Kukamatwa na Dawa za CODEINE ambazo mara nyingi hutumika kutengenezaa dawa za Kulevya aina ya SIZZURP.

TTM tumezinyaka kuwa Rapper Huyo ambaye maskani yake ni GEORGIA, Marekani, Week Ijayo atapandishwa Kizimbani ili Kesi yake hiyo iweze Kusikilizwa na hata maamuzi kutolewa.

Aidha Info ambazo TTM tumezinyaka Pia, ni kwamba Endapo 2 Chainz atabainika Kuwa na hatia, basi atatumikia Kifungo cha Takribani Miaka 3 Jela.


Tofauti na kukutwa na Aina hiyo a Madawa ya Kulevya, 2 Chainz ambaye ni Mbaya katika Collable anazopewa, aliwahi Kudakwa na BANGI jambo ambalo linamuweka mahali pabaya.

BONGO MOVIE KUNA HILI LA KUJIFUNZA.

6:45:00 AM Add Comment


Ukubali ukatae, TIM TUKO MBELE Still tunakubali sana Kila Product ya Burudani kutoka Nchini Tanzania.

SONGERA ZIGI ZIGI kwa Kitengo Chimbua Chimbua kwa kuweza kulibaini hili na Sisi kamwe hatuwezi kuikataa Ripoti yao.

NCHI ya Kenya imekuwa ni moja kati ya Mfano mzuri sana wa kuigwa Tangia LUPITA NYONG’O  aonekane kuwa na mafanikio mazuri sana katika tasnia ya Filamu Ulimwenguni, lakini kadri Siku zinavyozidi Kwenda, ulimwengu wa Filamu Nchini humo unazidi kuingia katika mabadiliko mazuri na Makubwa.

TTM tumeapata nafasi ya Kucheki Kipande cha Filamu ya PUMZI ambacho kinagharimu jumla ya Dakika 21kutoka Nchini Kenya kikiwa kina maudhui ya Science Fiction.

Tunapozungumzia Filam za Scince Fiction, Tunamaanisha Filam ambazo zinahusisha masuala ya Kisayansi ambayo hukushawishi wewe mtizamaji kuamini kuwa Hilo linalofanyika hapo, ni Kweli loipo na limetokea, ingawa huwa ni Masuala ya kibunifu.

Filamu hiyo Fupi ya Pumzi ambayo Imeongozwa na Muongzaji Mkenya WANURI KAHIU, inazungumzia AFRIKA MASHARIKI Ijayo, Miaka 35 Baada ya Kutokea kwa Ukame wa maji ikiwa ni madhara ama Athari ya VITA KUU YA PILI YA DUNIA.

Filamu Hii imenekana Kupendwa na wengi na Kuendana na Uhalisia wa tamko la UMOJA WA MATAIFA (UN), kuwa Mpaka kufikia Mwaka 2030, Kuna Uwezekano wa kuwepo kwa Uhaba wa maji Duniani kutokana na Ongezeko la watu.


Binafsi tunadhani BONGO Moviez wanatakiwa kutumia akili pana zaidi, kuendana na matukio makubwa ambayo hulenga Kumtokea mwanadamu hasa katika maisha yake, tofauti na Kufikiria Ideas za kawaida tu ambazo Ni MAPENZI kwa asilimia kubwa

MNADA BANNER