REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ISHU YA LIL WAYNE KUFARIKI…DATA KAMILI HIZI HAPA..

1:19:00 AM Add Comment


KUMEKUWA NA Huge Story Kunako Angle Mbali mbali Duniani Kuwa Rapper Nchini marekani LIL WAYNE WEEZY F BABY, amefariki Bin Kudanji akiwa Jijini NEW TORK Nchini marekani

Lakini baada ya Kupenya huku na kule na kufanya Uchokonozi wa hali ya Juu, Finally TTM tumepata  Full data Kuhusiana na Story Hizo ambazo zinazidi kuzunguka Kunako Mitandao Kadhaa ya Kijamii.

LIL WAYNE AMEKUFA ? AU LA?
Hii Sio mara Ya Kwanza kwa Taarifa kuhusu Lil wayne AMEFARIKI DUNI, kwa maana Hiyo unaweza kusema hii ni zaidi ya maa Moja kwa Rapper Lil wayne Kuzushiwa Amekufa. Lakini kwa Mujibu wa taarifa halali kutoka kwa Uongozi wa YMCMB, Ni Kwamba  Mkali wa ORIGINAL SILENCE “LIL WAYNE” Hajafariki Dunia, na Huo Ni Uzushi tu ambao Umeanzishwa Na Mtu mabyae haijulikani ametokea wapi na Anafanya Nini, na Ananioa gani na fanz wa Lil wayne na YMCMB Kiujumla.

CHANZO CHA UVUMI HUO.
Baada ya Kufanya upekuzi makini, tumekuja Kubaini kuwa Uvumi huo umeanzia Kunako Mtandao wa Kijamii, na Kuhamia katika mtandao wa Tweeter, ambapo TTM tulibahatika Kufuma Tweet Moja ya Mtu anayetumia Jina la BRETT FARR kutweet Kuwa LIL WAYNE AMAEFARIKI ASUBUHI HII. R.I.P 2014.



Tweet Hiyo Ilikuwa Posted Majira ya SAA NNE na dakika 51 Usiku, Tarehe 7 Mwezi Huu., jambo ambalo liliwashtua Wengi huku baadhi wakiamnini kuwa niuzushi ambao umekuwa Ukizushwa mara kwa mara.



Hata Hivyo, Jamaa aliyepost taarifa hiyo facebook, bado aliweka Video kama Kithibitisho, lakini Cha ajabu ni Kwamba Video Hiyo Haichezi hata Kidogo, jambo ambalo pia Linaonekana kuwafanya watu waamini kuwa Si kweli

UP DATE: YOUNG JEEZY ASEMA HAKUMPIGA MTOTO WAKE

1:09:00 AM Add Comment

DAKIKA CHACHE Zilizopita, Young Jeezy Amekanusha Kuwa Hajampiga mtoto wake wa Kiume JADARIUS Mwenye Umri wa Miaka 17. bali ni Plan ambayo ilipangwa na Mzazi mwenzake ambaye ameshaachana naye.

Jeezy Ameongeza Kuwa Mzazi mwenzake huyo alifanya Hivyo ili akamatwe na hata Kumchafulia Jina, Ingawa anakiri Kuwa Ni kweli , SEPT. 2012 aliingia katika Ugomvi na Mwanae huyo

YOUNG JEEZY ATIWA KIZUIZINI KWA KUMFUMUA MTOTO WAKE

1:03:00 AM Add Comment

HUWA ni mara Chache sana Kusikia Tukio kama Hili hasa kwa Celebrities wakubwa, licha ya Kwamba ni mara Nyingi Celebrities huwa Wanakwaruzana na watoto wao.
Kiukweli hatuwezi kusema kuwa Ni Story ya Kufurahisha ambayo imetua Kunako Meza ya TEAM TUKO MBELE.
RAPPER Young Jeezy ambaye alitambulika sana Kupitia Kwaju Zito la BLACK PRESIDENT, hivi sasa anashikiliwa na Polisi Nchini marekani na huenda akafunguliwa mashtaka ya Kujeruhi pamoja na Kutishia Kumuua Mtoto Wake
Kwa Mujibu wa taarifa Kutoka Mamlaka Husika, Tukio hilo lilitokea Mnamo Mwaka 2012, na hatimaye kukamatwa Siku ya Ijumaa iliyopita.
MTONYO WENYEWE UKO HIVI.
Inasemekana Kuwa JEEZY alimpa kipigo Mtoto wake huyo wa Kiume, huku akimrusha kutoka Bafuni na Kupitia katika Mlango wa Kioo, jambo lilimfanya Kijana huyo Kuanguka kwa Kupiga Kichwa Chake Chini.
Aidha TTM (TEAM TUKO MBELE) Imeendelea Kutonywa Kuwa, JEEZY Hakuishia hapo, bali alimfuata Mtoto wake huyo na Kuanza kumchapa Ngumi Pale Pale chini alipokuwa ameanguka, kasha akamburuza Mpaka Chumbani kwa na Kuanza kumpa makonde ya Kutosha huko Huko Chumbani.

Pia imefahamika Kuwa, JEEZY alitamka maneno Ya Kutishia Kumuua mtoto wake Mara Kadhaa wakati akimpa Kifinyo hicho, na Hata kudiriki kumwambia atampasua Kichwa chake Kwa Risasi.
Hata Hivyo JEEZY alionekana kukiri na Kuiheshimu Kibali cha Kukamatwa, na alisalimisha Kiasi cha Dolar za Kimarekani 45,000 sawa na  takribani Tsh MILIONI 67 na LAKI 5

Pia Jeezy aliua Story Kwa Kusema kuwa, anaamini Ishu Hiyo itakwisha kabisa na kila Kitu Kitakuwa Byee baada ya Muda Kadhaa

MNADA BANNER