REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

#DakaHiiFasta JASON DE RULO NI KINYOZI?

6:53:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
TOFAUTI na ishu nzima ya kufanya muziki, wasanii wengine wamekuwa na uwezo wa kufanya shughuli Nyingine kama kitu ambacho walianza nacho kabla ya muziki au kama ni kitu ambacho kilikuwa kichwani mwake na Muziki umekuwa kama Daraja lake.

JASON DE RULO yule yule wa "Wigle Wigle Wigle Wigle" tofauti na kufanya muziki ama kipaji cha Muziki, Ni Kinyozi hatari tena yule ambaye hategemei mashine, bali ni Kiwembe.

Akifafanua kuhusu Hilo, Jason De Rulo ambaye hivi sasa anadai kuwa hawezi kuzungumzia mahusiano yake, amedai kuwa, Kipaji cha Kunyoa, alikitoa kwa Baba Yake, ambaye zamani alikuwa akipenda kumnyoa pale ambapo alikuwa akibaini kuwa mwanae nywele zake hazijakaa poa.

Tofauti na kutokukaa poa, Pia Baba Yake Jason De Rulo alikuwa akimyoa pindi ambapo Bwana mdogo ahuyo alipokua akinyoa Style ambazo hazikuwa zinaingia akilini Mwake.

MSIKILIZE HAPA



#DakaHiiFasta KUTOKA KWA MTOTO WA MAREHEMU NOTORIOUS B.I.G

6:44:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
CHRISTOPHER JORDAN WALLACE maarufu kama CJ WALLACE ni Mtoto Marehemu NOTORIOUS BIG, ambaye ameweza kuunyaka Umaarufu Kupitia Kipaji tofauti na Baba Yake, Nazungumzia UIGIZAJI WA FILAMU.

Kama Ulikuwa Hujafahamu kuhusu Bwana Mdogo huyu ambaye mama yake ni FAITH EVANCE, ameweka wazi kabisa kuwa, Baba Yake alifariki akiwa na miezi 7, hivyo hakuufaidi utamu wa baba yake, kitu ambacho anakimiss hadi hivi sasa.
Lakini kitu ambacho kilikuja kumfanya Mtoto huyu aufahamu Umaarufu wa Baba Yake, ni kipindi ambacho alikuwa Shule, na baadhi ya Watu kuanza kumzungumzia Baba yake kila walipokuwa wakikutana naye.

LAKINI tofauti na kujaribu kujihusisha na Muziki, SEPTEMBA 9, Mtoto huyu wa NOTORIOUS anatarajia kuonekana katika Filamu Mpya THE KICKS ikiwa ni Filamu yake Nyingine na akizidi kukua haswa katika Soko la Filamu.

TIZAMA TRAILER YA MOVIE YA KICKS

MNADA BANNER