REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

LORD EYEZ AMESEMA HIVI KUHUSU OMMY DIMPOZ

11:59:00 AM Add Comment




  
SIMPLE AND CLEAR....Huyu Hapa EYEZ
 “Mi ninachosema wasimuhukumu mtu kwanza wala wasipandwe, wanahitaji kujua ukweli na wasifanye matukio yoyote ambayo ni ya uvunjaji wa sheria na pia wachague marafiki, wawe wastaarabu, wawe wapole na wawe na subira… wasimjengee chuki binadamu, mi mwenyewe nimekua mtu wa kusamehe sana ndio maana nakwambia wamwachie Mungu, kwa kuwa mimi sina chuki na mtu siwezi kumshauri mtu awe na chuki na mtu lakini malipo ni hapahapa duniani na Mungu yupo wamwamini sana sababu ndio anafanya kila kitu”



HUYU DEMU ANAMTISHIA NANI?

11:39:00 AM Add Comment


Hii Si Mara Ya Kwanza kwa Mtangazaji huyu wa Clouds FM, Loveness Love DIVA, kutuzingua mara kadhaa hasa kupitia FACEBOOK na TWEETER  kuwa anataka Kujiua

HAMJAMSHTUKIA TU?
Huyu Demu ni Mjanja sana, na Ujanja Wake mi nauona wa KIPUUZI kabisa. Hapa anachokitafuta, ni kufahamu Takwimu ya Watu wangapi Wanamjali, Wanampenda na kumthamini, huku akitegemea kuwa, wengi watambembeleza kama katoto Fulani hivi.

Sasa Hii sio Utu uzima ama Busara..hata kama unatutisha au kututania.

R.I.P MARIAM KHAMIS

11:29:00 AM Add Comment

Mungu ailaze Roho yako Mariam Khamis, Mahali Pema Peponi...Amen.
Tutakukumbuka kwa Utunzi wako Mzuri wa Nyimbo za Taarabu, Sauti yako Mwanana, na Tunzi zako Mahiri zilizoazimia kukuza Mziki wa MODERN TAARAB Nchin Tanzania.

Hakika Tumepoteza Kiungo Muhimu sana katika Tasnia ya Burudani hasa Taarabu.

BAADA YA MABADILIKO...SHETA YUKO TAYARI KABISAAA

9:58:00 AM Add Comment



Bonge La Bwana ni wimbo wa Rapper Shetta uliotangazwa kutoka mwisho wa mwaka huu na kwasasa ipo tayari baada ya mabadiliko kufanyika.

 Awali Shetta alitangaza kufanya wimbo huu na komando Lady J Dee ila baada ya mabadiliko aliwekwa Linah . Shetta ameongea na sammisago.com na kusema baada ya Lady J Dee kuskia beat na idea ya wimbo huu alimshauri afanye na msaani anaye endana nae kiumri zaidi ili ata akimwimbia Bonge la Bwana ieleweke zaidi, Fahamu kuwa Lady J Dee na Shetta bado watafanya wimbo mwingine ila sio huu. 

Baada ya kushauriwa hivyo Shetta aliona atakaye fanya vizuri kwenye Bonge la Bwana ni msanii Linah kutoka THT Na ndio amewekwa kwenye Wimbo huu kwa sasa. Kuhusu Video ,Tayari Adam wa Visual Lab anayo na anauskiliza kwahiyo muda wowote itaanza kufanyiwa kazi. Imesha thibitishwa kuwa Bonge La Bwana ni Shetta Ft Linah.

Kuhusu uzinduzi wa wimbo huu Shetta amesema kuwa kuwa uzinduzi utafanyika maisha club Terehe 25 November na atasindikizwa na wasanii kama Jafarah ,Stereo, Shilole , Linah , Young Dee , Feruuz ,Suma Mnazareti na Pasha.

WANAWAKE MTATUUA KWA HALI HII....

9:06:00 AM Add Comment



IKO HIVI...
KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya moto mwilini.

 YEYE ANASEMAJE........
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.


“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa, nikajiuliza kulikuwa na nini?

“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea,  jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia  mke wangu akiingia chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni.

 AISEE....POLE SANA...IKAWAJE TENA?
Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .

“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia,”  alisema Mahamba.

SOURCE : MPEKUZI

MNADA BANNER