REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TAFADHARI..ATAKAYEMUONA DIAMOND PLATNUMZ, HII INAMUHUSU SANA

6:08:00 AM Add Comment

Jina Ambalo Anajiita Mdogo wangu huyu Ni SWEET CAKE…basi, Ishia hapo Tu..wala Usiendelee kuniuliza

Ni muhitimu wa Kidato Cha NNe mwaka huu wa 2013, katika Shule ya St Mary’s na yupo katika Mchakato wa kusubiri kitakachotoka NECTA

SWEET CAKE ametengeneza kwaju hili huku akikiri kabisa kuwa idea ya ngoma yake hiyo, imetokana na Wimbo wa NITAREJEA wa Diamond Platnumz akiwa Na Hawa,iliyofanya Vema sana miaka kadhaa Iliyopita

UPCOMING Artist huyu mwenye makazi yake Mwanza kwa hivi sasa, ana Ndoto za kufanya kazi na Producers wakali akiwemo LAMAR wa FISH CRAB, pamoja na wasanii Mbali mbali akiwemo Diamond.

Katika IDEA ya Track Hii, Dhamira ya SWEET CAKE (Kama anavyojiita), ilikuwa ni kuifanya pamoja na Diamond, ambapo Sweet Cake angelalamika kama Mtoto Wa Diamond, Diamond angetakiwa Kujibu humo humo kama Baba ambaye aliahidi Kurudi Baada ya Kufanikiwa huko Town alikoelekea

Dhamira yake haikuweza Kufanikiwa, ingawa bado hajakata Tamaa ya Kumtafuta Rais huyo wa Wasafi (DIAMOND PLATNUMZ) ili wafanye Wote kazi ya pamoja.

 Katika hatua zake za kuchakarika kumpata Diamond, Sweet Cake anakiri kuwa ameshamtumia Tayari Ngoma Hii, na hivi sasa anasubiri kitakachojiri kama Jibu kutoka Kwa Platnumz Juu ya Ngoma Hii.

Kunako Pini Hili, Sweet Cake amemshirikisha Msaani Mkali hapa Jijini Mwanza ABOU MKALI (TIM), huku Mkono ukiwa ni wa Producer Kazi Moto na Side Poison wa SILKA MUSIC.

Atakayemuona Platnumz..tafadhari afikishe Ujumbe huu ili kutimiza Ndoto ya Mdogo wake huyu


STL NA COLLO WAOMBA RADHI KUFUATIA TRACK YAO…KUDINYANA

5:45:00 AM Add Comment



Ushalalaaaa..Ulalaaaa.. mazee, mtatuwia Radhi lakini inabidi tuseme tu

The Hot Kenyan Chick STELLA MWANGI – STL na King wa Rap COLLO wameomba radhi baada ya Track Hiyo kuvuja kunako mitandao Mbali mbali ya Kijamii na hata kuzua Tafrani kwa wadau kibwena

Aidha baada ya kuzua Utata, Producer wa Track hiyo alijitokeza na kusema kuwa, audio hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya mambo yao tu wakati wako Studio yaani masihala, na wala haikuwa imetengenezwa maalum kwa ajili ya Umma wa watu Kuisikia, na haikwa imetarajiwa kuvuja.

Kwa Upande wao COLLO na STL, wao pia wameomba radhi kwa tukio hilo ambalo halikuwa limepangwa Kutokea, huku wakiwasihi watu kuwasamehe kwa Moyo mmoja, na watalifanyia kazi Suala Hilo hasakwa wale wote walioathirika na kukwazwa na Track hiyo yenye tittle na maneno makali Ndani yake

MAJANGA BOY: KUMBE JUSTIN BIEBER ALISAINISHWA MKATABA WA NIDHAMU

5:37:00 AM Add Comment


Pengine hii inaweza ikawa ni ahueni katika Mishe chafu za kikorofi kwa Mdogo wetu huyu ambaye hivi sasa ni talk of the world kwa Kufanya majanga Kibao. Sasa imekuwaje katika Kurambishwa Mkataba Bila Yeye kupenda wala Kutarajia.. Zima.

Mkali wa Pop Nchini marekani JUSTIN BIEBER alirambishwa Mkataba wa Kuwa na Nidhamu ya hali ya Juu Pindi atakapokuwa katika Hotel moja iliyoko nchini New Zealand,

Kwa mujibu wa mitonyo wa wadakuzi na wakuda waliokubuhu katika udaku, inasemekana kuwa, Bwana Bieber alipigwa Bonge moja la Stop kuingiza wasichana  katika Chumba cha Hotel ya LANGHAM, alichokigharamikia kwa EURO 1000, pamoja na kula Sehemu tofauti na Wageni wengine, ili kuepusha Tafrani ambazo zinaweza Kujitokeza.

 

Kwa mujibu wa Chanzo cha Mtonyo huu, inasemekana kuwa Mkataba huo Ungemuamuru Bwana Bieber Kusepa haraka bila Ubishi endapo angekiuka masharti ya Mkataba.

Hata Hivyo, baada ya mkataba huo wa nidhamu kwa majanga Boy Huyo Mwenye umri wa Miaka 19, Management yake (Biebr) ililazimika kuusaini licha ya Kuwa na Msururu wa masharti ya kutosha, kwani Utawala wa hoteli haujarishi Umaarufu wa Justin bieber, bali wao wanamchukulia kama Mteja yeyote Yule anayekuja hapo

Pia mdaku huyo aliongeza kuwa, Justin bieber hakuwa na Budi kukubaliana na maamuzi hayo, ambapo masharti mengine makubwa mawili ni Kutokparty ndani ya hotel hiyo, ama kuwabugudhi wateja wengine.

KANYE NA KIM WAMESEMA HIKI KUHUSU PARODGY YA BOUND 3

5:17:00 AM Add Comment



Wengi huwa tunamfahamu Kanye West kama Mtu ambaye huwa hapendi masihala na hata Kufuatwa fuatwa katika Mishe yake ya aina yeyote.

Lakini Siku kadhaa baada ya Kutoa Video yake alomshirikisha Mchumba wake, Kim Karadshian, Jamaa wawili wanaofahamika kwa majina ya JAMES FRANCO na SETH ROGEN walitoa Bound 3 wakirudia kile ambacho Knaye na Kim Wamekifanya , ikiwa ni katika mfumo wa masihala Fulani


Lakini Baada ya Kanye West na Mchumba ake Huyo Kim Kuiona Video hiyo, waliisifia na hata Kuipongeza kwa Kadri ambavyo Jamaa hao wawili walitumia Ubunifu wao Wa Jinsia Moja, yaani Kanye Ni Mwanaume, na Kim ni Mwanaume Pia.

Tofauti na Watu ambavyo walitarajia kuwa wawili hao Kanye (36) na Kim (33) wanaweza kufungua mastaka na hata Kuwasakama James na Seth, video hiyo ilipongezwa na hata Kupigiwa Promo ili iweze kutizamwa na Watu ili wapate hata Fursa ya kucheka

Kupitia Account yake ya Twitter, Kim Kardashian ambaye ni mama Wa Mtoto wa Kanye, North West, aliweza kutweet kwa kuwaambia wameipatia na ilikuwa inafurahisha


Kim hakuishia hapo tu, bali alimtweet Seth Rogen na kusema kwamba, kanye West amechekeshwa sana na Video hiyo.

Kwa Upande wake Seth Rogen alimshukuru Kim kardashian kwa kuweza kuielewa kazi waliyoifanya

MNADA BANNER