REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MPENZI DEAR BABY : KWANINI NAKUPENDA

8:16:00 AM Add Comment

Na Frank M. Joachim.
Napenda Sana Kukuambia NAKUPENDA SANA ama I LOVE YOU SO MUCH mara Nyingi katika Mazungumzo yetu. Lakini unaju ni kwanini?  :

  • Unajua ni nini maana ya Uwepo wangu katika Maisha yako
  • Unamatarajio na mimi katika kila aina ya Mpango wako na hata wangu.
  • Unajua thamani ya Ahadi ambazo tulidhamiria kuzikamilisha.
  • Hupendi niwe Mpweke, Mnyonge, na hata kutokuruhusu Kutawaliwa na Mawazo katika akili yangu.
  • Unanipenda Mimi na Kila kitu nilichonacho.
  • Wewe ni Kipofu katika Mapungufu yangu Hasa katika Muonekano wangu wa Nje.
  • Unajua namna ya kucheza na sehemu kubwa ya Mahitaji yangu.
  • Unajua kutoa faraja hata nisipoihitaji.
  • Neno lako "Nakupenda" linabeba kila hisia ya Kimapenzi kutoka ndani ya Moyo wako.
  • Unafahamu Utani ninaouhitaji katika Muda Husika, na hata mazingira husika.
  • Hupendi kuchukia mbele yangu.
  • Hujui kunilinganisha na Mtu Fulani mwenye hadhi fulani.
  • Hupendi kunidanganya, maana unakuwa huru katika Kila kitu hasa ukiwa na Mimi.
  • Unatamani sana niwe Sehemu kubwa ya Furaha ya Maisha yako.
  • Unatamani sana Kujenga Familia yenye MAFUA (Mapendo, Furaha na Amani) na mimi. 
Sina Budi kusema "Ninakupenda" kila ninapohitaji kukuambia Hivyo. Ninakupenda

TANGAZO LA FIAT MPYA: TUPO KAZINI

7:16:00 AM Add Comment

HEBU Tizama Piacha Hii kwa Umakini...then Tizama kwa mara ya Pili

Yes, hao ni Wanamitindo (Mamodo) 13 Waliojipinda kadri ya Uwezo wao, katika Kutangaza Ndinga Mpya ya FIAT 500 ABARTH. 
Models hao walikuwa Uchi kama walivyozaliwa, lakini walipakwa rangi na kuonesha Muonekano Halisia wa Gari hiyo Mpya.

UNYANYASAJI: JAMAA AMFANYIA UKATILI MBAYA BINTI HUYU BAADA YA KUMKATAA KIMAPENZI

3:07:00 AM Add Comment
Victoria Akionesha Kovu Lake kubwa katika Mguu

Victoria akionesha Sehemu nyingine

                                    Victoria akionesha Makovu Mengine katika Mkono (PICHA ZOTE NA DJ. ALEX)

Na Frank Joachim & Dj Alex.
Licha Ya Kupigiwa kelele kila Siku, suala la Unyanyasaji bado linazidi kushika kasi katika Maeneo Mbali mbali.

VICTORIA LUMWA, alikutana na Mkasa ambao haukuwa na Maana ya kumpatia makovu yenye Mateso makali kama anayoyapata Hivi Sasa.

ANAISHI WAPI:
Victoria ni Mkazi wa jiji la Mwanza, na anaishi maeneo ya IGOMA. Binti huyu anaishi na Dada yake, ambaye ni Mlezi wake Kwa hivi sasa

KISA CHA KUKUTANA NA MKASA HUO:
Kwa Mujibu wa maellezo yake, kuna Kijana amekuwa akimtaka Kimapenzi kwa Muda Mrefu, jambo ambalo Binti huyu hakuwa tayari kulifanya kwa kuzingatia Hisia zake. Baada ya Victoria Kumkataa Kijana huyo, majibu yaliyotoka ni "Si Unajifanya unanikataa...sasa Ngoja utaona."

Kauli hiyo haikumshtua sana Binti huyu Mrembo wa Kiafrika, na kuamua kuendelea na Maisha yake ya kawaida. lakini siku moja wakati anasafisha Vyombo nyumbani kwa Dada yake, alishangaa Ghafla anatokea Mtu akiwa amebeba Sufuria, huku ndani yake kukiwa na maji ya Moto.

Baada ya Victoria kuhisi hali ya hatari, aliamua kujikinga na Mkono na Kugeukia ubavu mwingine, ili kuepusha maji hayo kumpata Usoni. Dhamira kubwa ya Mtendaji wa tukio hilo, ilikuwa mni Kumuunguza Victoria Usoni, ili kuiharibu Sura yake ambayo inasemekana kuwa ndiyo inayompatia Kiburi cha Kuwakataa wanaume.

IMANI ZA KISHIRIKINA :
Victoria anaamini kuna uwezekano wa Imani za Kishirikina kuhusika kwa namna moja ama nyingine. Sababu za Victoria kusema hayo ni :

  • MTENDAJI wa Tukio hilo alikuja kimazingara, baada ya Kutokea Ukutani akiwa katika Mavazi ya ajabu na kuchukua hatua hiyo, kisha Kupotea Ghafla.
  • Jamaa aliyemtongoza na kumtishia Hilo, ni Mkazi Wa KIGOMA, ambako KWA IMANI zake yeye (Victoria) anadai kuna Imani za Kishirikina


SHAVU: OCTOPPIZO KUSHARE ONE STAGE NA 2 CHAINZ

1:47:00 AM Add Comment
2 Chainz kwa Stage

Baada ya Ya CAMP MULLAH kuchangia Jukwaa Moja na SNOP LION (Zamani Snoop Dog Dogy), sasa ni Time ya Mkali wa Michano OCTOPIZZO kukutana na 2 Chainz kuna Stage Ileile.

Mkali Huyo wa IVO IVO tokea 254- Kenya, anatarajia kuzima na Bonge Moja la Show litakalofanyika Nchini Uingereza, huku akishea Stage Moja na Rapper Nchini Marekani 2 Chainz katika Ukumbi wa UN-CONVENTION CONFERENCE ulioko BIRMINGHARM.

Show hilo ambalo litashushwa Mnamo September, ni Maalum kwa ajili ya Kuhamasisha hasa katika madhara ya Masuala hasa ya Vita ama migogoro mbali mbali ya Kisiasa.

OCTOPIZZO "Mr IVO IVO"

Lakini, hii inaweza kuwa ni sehemu ya RUNGU ambalo atamuumiza Adui yake RABBIT maarufu kama KAKA- SUNGURA ambaye Siku chache zilizopita alionekana kumdiss vilivyo kupitia Mtandao wa Twitter

TETESI: KASHFA YA PEKEE KWA SIZE 8.

1:25:00 AM Add Comment

IKIWA ni Muda Kadhaa tangia Amamua Kuzima katika Michakato ya Mikwaju ya Kidunia na Kuamua kuingia katika Mikwaju ya Injili, Mwanamama Size 8 al the way from 255 Kenya, amekumbana na CLASSIC Skendo. Unataka kujua ni Ipi, Basi Zima nikupe Mtonyo.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Daily Post kupitia Nairobi Exposed, inasemekana Kuwa Mwanadada huyu mweye kila hadhi ya Kuitwa Sexy beibe amewatupa Wazazi wake waili ambao maiosha yao ni Magumu.

Mwanadada huyo anayemiliki Mamilioni ya Fedha huku akitikisa na Kwaju la MATEKE, anadaiwa kuonekana kumwaga Mikwanja katika kunisa ambalo inasemekana Eti, ndilo ambalo hulitumia kufikisha Maombi yake kwa Mwenyezi Mungu.

Tofauti na Kulisupport sana kanisa hilo linaloitwa BARAKA INTERNATIONAL CHURCH liliopo Kairobangi South Mjini Nairobare, Size 8 anadaiwa kusitisha huduma na Kumpotezea kabisa Bi. Mkubwa ake, yaani mama ake.

Wadaku hao wamefafanua Chanzo cha SIZE 8 Kuwakaushia wazazi wake hao, ni kutokana na kutokuwepa kwa Maelewano mazuri baina yao (Wazazi Wake)


Pia inasemekana kuwa, Wazazi wake wamekuwa wakijitahidi kumpigia Simu mara kwa mara, lakini Eti, SIZE 8 huwa anazipotezea kabisaaaa

BBA THE CHASE :KUNACHIMBIKA NDANI YA RUBY…ZIMA KWANZA NIKUTONYE

12:54:00 AM Add Comment

NA FRANK JOACHIM
PENGINE Game limeanza kushika  Fleva katika Mjengo wa BBA. Inaonekana Dhahiri kuwa huenda kukawa na KIJIBIFU cha Kimya Kimya kwa wana RUBY 3, namzungumzia CLE, FEZA (Tanzania) na ONEAL (Botswana).

Katika Muda wa Diary, Mrembo CLEO alionesha msononeko Mkali katika Hisia zake, huku akitoa Machozi wakati akipiga Story na BIG BROTHER. Cleo alifunguyka kuwa, tayari anamini yupo katika Maelewano mabaya na Wanandoa Wapenzi wawili FEZA na ONEAL ambao wanafahamika kama ONEZA.

Akizungumza kwa Masikitiko na Hisia kali, CLEO alionsema kuwa, chanzo ni yeye kukaa katika Moja ya Corner iliyopo katika Nyumba ya RUBBY, inayoaminika kuwa maalum kwa Wawili hao (Feza na Oneal). Ninamnukuu CLEO akisema “Ninahisi kama Wana matatizo na Mie. Na Kama wana tatizo na Mie, Basi wanatakiwa waje kuzungumza na Mie. Ila nimemuomba Mwenyezi Mungu kuhusu hili na aweze kuniepusha nalo.”

Katika Upande wa FEZA, yeye alimfungukia BIG BROTHER kuwa Cleo anaonekana  ni Mbinafsi, ingawa haamini kama ni Mtu Mbaya. Ila tu anatakiwa kubadilika hasa katika Baadhi ya Vitu vichache.

ONEZA walionekana kumlalamikia sana Mzambia huyo hasa katika Muda huo wa DIARY, wakisema kuwa Kuna matukio mbali mbali ambayo ameyafanya na yanawakwaza

MNADA BANNER