REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

LADIES & GENTLEMEN.....Namleta Kwenu, SHEMEJI YANGU...Finaly Mdogo Wangu JOHANESS MAGNUS JOACHIM mepata Furaha Yake...Miss JULIANA

10:02:00 AM Add Comment


WANA-MAKETE WASHAURIWA KUACHA KUKUMBATIA VYANZO VYA MAAMBUKIZI YA VVU

8:51:00 AM Add Comment
  Mkuu Wa Wilaya ya Makete, Mhe. Josephine Matiro akizungumza na wakazi wa Makete waliohudhuria Sherehe hizo hapo Jana



Na Edwin Moshi, Makete
Imeelezwa kuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona bado wanamakete wanakumbatia sababu zinazopelekea kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI licha ya elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kuendelea kutolewa siku hadi siku

Miongoni mwa sababu hizo zinazokumbatiwa na wanamakete ni pamoja na kurithi wajane bila kupima wala kujua mumewe alikufa kwa UKIMWI ama la, ulevi uliokithiri hasa wa pombe za kienyeji, kufanya ngono isiyo salama pamoja na watu kutokubali kubadili tabia licha ya kupewa elimu ya namna ya kujikinga na VVU

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Mh. Josephine Matiro, ambayo kiwilaya imeadhimishwa katika kata ya Ikuwo tarafa ya Ikuwo wilayani hapa

 Mkuu Wa Wilaya Makete Mhe.Josephine akiteta Jambo katika Meza Kuu

Amesema kwa hivi sasa kutokana na dhana iliyojengeka katika maeneo mengine nje ya wilaya kuwa wilaya ya Makete inaongoza kwa kuwa na watu wenye VVU, jambo ambalo amesema si kweli lakini pia dhana hiyo itaondoshwa vichwani mwa watu huko nje ya wilaya kwa kuacha kukumbatia sababu zinazopelekea ongezeko la VVU

“Unajua wakati nakuja Makete kila mtu alikuwa ananishangaa wanasema Makete hakuna watu, wengi wamekufa kwa UKIMWI, lakini nashukuru nimekuja na nimekuta watu, na si kweli kwamba wote mna VVU kama wanavyosema lakini kikubwa tubadilike hivi sasa ili kuondoa hiyo hali zaidi ya hapa tulipo” alisema Matiro

 Mmoja wa Watumishi wa Shirika la SUMAMSESU Wilayani makete akiwa amevalia Tshirt Yenye Ujumbe Huu

Mkuu huyo ametoa agizo kwa viongozi wote wa kata na tarafa ya Ikuwo kuhakikisha wanadhibiti wale wanaofungua vilabu ya pombe na baa muda wa kazi kwani nao wanachangia ongezeko la VVU hiyo sheria ifuatwe kwa wale wote watakaokaidi

Awali kabla ya kutoa hotuba yake kwa wananchi waliofurika katika kijiji cha IKuwo, mkuu wa wilaya alipata wasaa wa kutembelea chumba maalum kilichotengwa kwa ajili ya ushauri nasaha na upimaji, ambapoa alijionea jinsi shughuli hizo zinaendeshwa kwa watu wanapofika kutaka kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Makete, Ndg. Francis Chaula akiwa Meza Kuu

Akisoma risala ya siku ya UKIMWI duniani mbele ya Mgeni rasmi na wananchi waliofika kwenye maadhimisho hayo muelimishaji rika Bw. Boniphace Mbilinyi ambaye anaishi na virusi vya Ukimwi amesema hadi juni mwaka huu jumla ya watu 246 kutoka kata ya Ikuwo wamepima na kugundulika kuwa wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI na taarifa zao zipo kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya kwa waviu kwani miongoni mwao 112 tayari wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV)

Amesema kutokana na kuwepo kwa sababu zinazochangia watu kupata VVU, bado kata hiyo ina mikakati ya kupambana na ugonjwa huo kwa kuendelea kutoa elimu, kudhibiti sheria kuhusu unywaji pombe muda wa kazi, pamoja na kuendelea kuwaelimisha wanaume ili nao wakapime VVU kwa hiari kama wanavyofanya wanawake
Katika hatua nyingine shirika la SUMASESU limetoa taarifa ya mapambano dhidi ya UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia katika tarafa ya Ikuwo na Matamba ambao unatekelezwa na shirika hilo kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa jamii hiyo

 Wasanii wa Shirika La SUMASESU Wakitoa Burudani Matata kwa Wana- Makete

Akisoma taarifa hiyo kwenye maadhimisho hayo Bi. Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU amesema katika kipindi cha mwaka mmoja Machi 2012 – Februari 2013 shirika hilo linatekeleza mradi wa mapambano dhidi ya UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia ujulikanao kama shule salama unaofadhiliwa na mfuko wa dharura wa mapambano dhidi ya UKIMWI (RFE) ambapo katika tarafa hizo mbili mradi unawafikia wanafunzi wa shule za sekondari nne ambazo ni Matamba, Itamba, Ikuwo na Mlondwe pamoja na wanajamii kutoka vijiji 12 ikiwemo vijiji vitatu vinavyozunguka kila shule

Amesema pamoja na malengo mengine ya kumjengea uthubutu mwananfunzi pia inasaidia wanafunzi hao kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kujikinga na VVU, ambapo kwa kata ya IKuwo shirika hilo limewafikia vijana 351 ndani na nje ya shule

Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani kw amwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana”


JICHO KU MOYO - PIcha za Kipindi cha Wanawake Live (EATV na Joyce Kiria) Huwa Zinavutia Kiukweli..Hebu oneni na Ninyi

8:24:00 AM Add Comment





HIZI NI BAADHI YA MALI ZA MAREHEMU SHARO MILIONEA ZILIZOIBIWA, ZIKIWA ZIMESALIMISHWA

6:03:00 AM Add Comment

MNADA BANNER