REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAFISI : RAPPER FUTURE ANASWA AKIMNYEMELEA BINTI MWINGINE... SIJUI ATAKUWA NI WA NGAPI HUYU !!!!!

1:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
HAKUNA mtu yeyote hapa duniania ambaye anapingana na sie kuwa Rapper Future kutoka Nchini Marekani, ni Rapper anayekubalika sana kwa kuachia Mikwaju Heavy ambayo humfanya kila mtu afungue hisia zake na hata kubang nazo sehemu yoyote

Lakini kama Haitoshi, hakuna Mtu asiyefahamu kuwa Future ni baba wa watoto wengi kutoka kwa mama tofauti ambao mpaka hivi sasa hakuna hata mmoja ambaye anaishi naye ama kutarajia kufunga naye Ndoa, akiwemo Ciara ambaye hivi sasa tayari yupo katika Ndoa yake iliyotulia tuliiii


Sasa kingine cha Nyongeza, kama ulikuwa hujui, Future bado anazidi kudhihirisha kuwa hawezi kamwe, kutulia na mwanamke mmoja hata awe na utamu ama uzuri wa aina gani, na hilo limethibitishwa hii leo na tunalianika kupitia hapa hapa.

Hit Maker huyu wa Track ya MASK OFF, ambaye alituahidi mwaka jana kuwa atabadilika na kuwa mtu mwema, asiyewaumiza na kuwakwaza watu, atakayewajali watoto wake, atakayejituma kwa hali na mali kuwafanya watu wamuamini, amenaswa akimnyemelea Binti mwingine

kama ambavyo tumewahi kuanika hapa hapa kuwa hivi sasa ana mahusiano na Ex ambaye pia ni mzazi mwenzake Bow Wow, anayefahamika kwa jina la Joie Chaviz, huku tukiamini na wao waili hasa Future akionesha kuwa wawili hao wameshibana na wana mahaba ya dhati, Lakini Future bado hajanogewa na Utamu wa bibie Huyu

Rapper huyo ambaye yuko Paris kwa ajili ya Maonesho ya Fashion, alionekana kabisa kuwa anahitaji mwanamke wa kumpa kampani na hata kuamsha naye Dude, hali iliyomfanya amnyemelee Binti mmoja mwenye asili ya ki-british, kupitia DM

Chart hiyo imeanikwa na binti huyo baada ya kuona jamaa anazidi kumtext kila mara kitu ambacho kwa upande wake hayuko tayari kukifanya, na ili kumfanya aachane na unyemeleaji huo, kaamua kumuanika moja kwa moja ili atambue kuwa kuna watu hawashoboki na mastaa wa aina yoyote hata kama wanakunya moto

RACHEL KIZUNGUZUNGU AFAFANUA KUHUSU YEYE KUTOKA NA T.I.D

1:14:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAHENGA hawakuwa Nyuma kusema kuwa Ukiona Mtu Mzima, analia mbele za Watu, basi ujue kuna jambo ambalo limemfanya abubujikwe machozi, na hii ndiyo tunaiona kwa Rachel Kizunguzungu

Hatimaye Bibi huyu hapa ambaye alikuwa na kashfa za aina tofauti tofauti huku kubwa zaidi ikiwa ni madawa ya kulevya ambayo alikiri ni kweli yalimkosesha vitu vingi ikiwemo kazi zake na hata watu wake wa karibu, ameweka bayana kuwa hakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Msanii T.I.D kama ambavyo wengi walikuwa wakidai

Akielezea kuhusu kauli hiyo, Rachel anadai kuwa, aliumizwa pia na kauli za watu wengi kuwa Msanii huyo, yaani T.I.D ndiye aliyemfundisha kutumia madawa ya kulevya kitu ambacho kwa upande wake sio Kweli

Aidha, Rachel anadai kuwa Taarifa za kutelekezwa Dubai na Boyfriend wake, Visa Kuisha, kuswekwa Rumande huko Maskat, hazikuwa taarifa za Ukweli na kitu ambacho kilimuongezea Stress zaidi, ni namna ambavyo baadhi ya jamii zilikuwa zikimtafsiri tofauti na hata kumuuliza mara kwa mara na Maswali ya Muziki wake na kutokuachia kazi mpya

HAIWEZEKANI: ETI WATU WAMELISHWA PANZI NA SIAFU KWENYE PARTY YA KUSIKILIZA ALBUM YA JUSTIN TIMBERLAKE?

12:41:00 AM Add Comment

Na Rich Sam
Watu Wa Mungu tunajua utaratibu wa kuandaa party ama event ndogo ya kusikiliza Album au Wimbo kwa upande wa Industry ya Tanzania, bado haujapata mwamko kiviile kulingana na uhaba wa tabia ya kuachia Album ama kukosekana kwa utamaduni wa aina hii kwa Wasanii Wetu

Lakini kwa upande wa Nje, yaani mataifa ya Nje, ukizingatia kuwa kwao ni utamaduni na ni muhimu kwa msanii kuachia Album, basi tukio hili huitwa ALBUM LISTENING ambapo wasanii mbali mbali na management zao huandaa na kuwaalika wadau mbali mbali wa muziki kwa ajili ya kuisikiliza kabla haijaachiwa

L:akini imekuwa ni tofauti kwa Msanii JUSTIN TIMBERLAKE ambaye husifika sana kwa kuachia Hit Songs kadha wa kadha, ambaye amefanya Event ya Album Listening kwa kuwalisha watu Vyakula vilivyo katika Mfumo wa PANZI na SIAFU

Kama ulikuwa hufahamu, Justin Timberlake ambaye ni hitmaker wa Track ya SUIT & TIE aliyomshirikisha Jay Z, anatarajiwa kuachia album yake aliyoipa jina la MAN OF THE WOODS,  na  event hiyo ilikuwa katika Muonekano wa aina yake

Wahudhuliaji wanadai kuwa Event hiyo ilidizainiwa na Miti mbali mbali, Mbao mbao, vichaka vya hapa na pale, yaani muonekano wa porini kabisa

Ukiachilia mbali muonekano huo, Pia menyu ya msosi ilikuwa na Vyakula ambavyo vilikuwa katika muonekano wa Panzi na Siafu na mengineyo ya pirini, kitu ambacho baadhi walishtuka awali lakini baadaye wakafurahia hali halisi ilivyokuwa

Sambamba na hayo yote, Baadhi ya wadau wanasema kuwa hawakuona kitu chochote cha Suprise katika album hiyo ukilinganisha na walivyotarajia kuwa pengine atafanya Makubwa sana

Cha msingi tusubiri tuopne kama kweli utamu umo ama ni namna gani Vipi

   @babajutiblog  

MNADA BANNER