REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UMASIKINI WAZIDI KUWATAFUNA WAFARANSA KILA SIKU

11:52:00 PM Add Comment

PARIS, Ufaransa.
Siku hadi siku idadi ya Wafaransa wanaoishi nchini ya mstari wa umasikini inazidi kuongezeka. 

Televisheni ya France 24 jana ilitangaza ripoti ya kila mwaka ya taasisi ya misaada ya Kanisa Katoliki kuhusiana kuendelea kuongezeka kiwango cha umasikini nchini humo. 

Ripoti hiyo iliyotangazwa jana asubuhi inasema kuwa, hivi sasa mwananchi wa Ufaransa badala ya kutatuliwa matatizo yake ya kiuchumi yanayomkabili, ndio kwanza anazidi kukabiliwa na matatizo zaidi. 

Televisheni ya France 24 imeendelea kusema kuwa, ukosefu wa ajira na makazi, ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayozidisha hali ya umasikini nchini humo na kwamba, juhudi za kuepukana na hali hiyo zinazidi kukabiliwa na changamoto nyingi na ngumu. 

Idadi ya watu wanaoishi chini ya kipato cha Euro 680 kwa mwezi inazidi kuongezeka ikilinganisha na miaka miwili iliyopita nchini Ufaransa. Hivi sasa kiwango hicho kimeongezeka kutoka watu 65 elfu na kufikia watu milioni mbili. Na Sudi Jafar

WANAFUNZI NCHINI MAREKANI WAPINGA USHINDI WA RAIS OBAMA

11:42:00 PM Add Comment
NEW YORK, Marekani.


Duru za habari kutoka Marekani zimearifu kuwa, mamia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Mississippi katika jimbo la Mississipi, wamefanya maandamano makubwa kupinga ushindi wa Rais Barack Obama. 

Wanafunzi hao wanaokadiriwa kufikia 400 walimiminika mabarabarani kupinga hatua ya kuchaguliwa mara ya pili rais Obama. Chuo kikuu hicho kimetoa ripoti kuwa, mikusanyiko ya wanafunzi ilianza tangu siku ya Jumanne usiku na kuongezeka zaidi jana na leo. 

Wanafunzi hao waliokuwa wamejawa na hasira walibeba mabango mbalimbali huku wengine wakitoa nara za kulaani ushindi huo wa Obama. Kufuatia purukushani hizo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi hao.

UN Yasisitiza Kuacha Mapigano Nchini Libya

11:37:00 PM Add Comment

NEW YORK, Marekani.



Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilisisitizia udharura wa kukomeshwa mara moja mapigano ya watu wenye silaha nchini Libya.

 Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Twariq Matri, ambaye aliwahutubia wajumbe wa Baraza hilo hapo jana kwa kupitia mkanda wa video, alisema kuwa, viongozi wa Libya wanapaswa kutekeleza marekebisho ya haraka katika sekta za kiusalama na vyombo vya mahakama kwa ajili ya kuzuia mapigano, uvunjwaji wa haki za binaadamu, mateso na vitendo vyote vinavyokinzana na sheria za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. 

Kuhusiana na uundwaji wa serikali mpya ya Libya mwezi Julai amesema kuwa, hiyo ni hatua muhimu nchini humo itakayosaidia kuleta uthabiti na wakati huo huo kumaliza changamoto za kiusalama na vitendo vinavyokinzana na sheria za taifa hilo.

 Aidha mjumbe huyo wa UN nchini Libya, amezungumzia hatua hafifu zilizochukuliwa na Tripoli kwa ajili ya kukabiliana na makundi ya wabeba silaha na kusema kuwa, serikali ya Libya inahitaji kutekeleza marekebisho katika jeshi na taasisi za kiusalama za nchi hiyo.

MNADA BANNER