REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HEBU SIKILIZA HII TRACK, HALAFU UNIAMBIE WHY UP COMING ARTISTS HAWAPEWI HAKI ZAO?

2:16:00 AM Add Comment

JAY DEE FT. PROF JAY- Joto, Hasira

1:57:00 AM Add Comment


Hii Ni Collabo Kali ya Wakongwe wa Muziki wa Bongo Flava, ambao wamepata Mafanikio Makubwa. 

MAREHAMU HUGO CHAVEZ APEWA HESHIMA ZA MWISHO

1:36:00 AM Add Comment
    HESHIMA ZA MWISHO: Mwili wa Chavez ukipitishwa katika barabara za mji mkuu Caracas


MWILI wa marehemu rais Hugo Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo ya jeshi katika mji mkuu Caracas

Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.

Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao .
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.

Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.

Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.

Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na bwana Chavez alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha ealisema angependa kuendelea kuishi.

Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini

Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner.

HOT PIC: SIO KWENYE TENNES TU...

1:18:00 AM Add Comment

MSUKUMA Tenis kutoka Hispania, Rafael Nadal akidhihirisha kuwa hayupo katika Kusukuma Tenis tu, balo hata katika Malovelo yumo. Hapa alikuwa Nchini Mexico na KISHTOBE wake (GF) Maria Francisca Perello wakila Bata


ELIMU NA AFYA: WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA MBEYA VIJIJINI HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA VYOO DUNI

12:59:00 AM Add Comment
 HATA WAO: Hivi Ndivyo Vyoo vya Walimu wa Shule hiyo ya Msingi

 WANAJISAIDIA HAPA : Haya Ndiyo Matundu ya Vyoo vya Wanafunzi wa Shule Nzima


 MALIWATONI : Hivi Ndivyo Vyoo vya Wanafunzi wa Shule hiyo ya Italazya

 TAIFA LA KESHO : Wanafunzi wakiwa Darasani

 TUNATAFUTA DIVISION 1. Wanafunzi walio katika hatari ya kukumbwa na Magonjwa ya Mlipuko wakiwa Darasani

MALIWATO MAPYA: Hii ndiyo sehemu ambayo wanafunzi hao wasadikiwa kujisaidia kwa sasa

PICHA: KAMANGA MBEYA

UKATILI KWA WANAHABARI TANZANIA: ABSALOM KIBANDA ASAFIRISHWA KWA MATIBABU ZAIDI

12:41:00 AM Add Comment
 NDANI YA NDEGEMhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink

 POLE MUME WANGU. Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella Semaya, tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu

 TUKO PAMOJA NAYE Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali.


 MSAADA : Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink wakimpandisha Absalom Kibanda ndani ya Ndege.


 TUMESIKITISHWA SANAOfisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Hussein Bashe akizungfumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kutekwa kwa, Absalom Kibanda

POLE SANAMwenyekiti wa CHADEMA, Freema Mbowe akimjulia hali Absalom Kipanda katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili Dar es Salaam.

PICHA: AMANI TANZANIA

MNADA BANNER