REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

AKOTHEE: KAANGALIE SIKU YA MWISHO ULIVYOBADILISHA NGUO YAKO YA NDANI. (INSTA CHOCHO)

12:18:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
BANANGE !!!!!
AKOTHEE amechefukwa zaidi ya "Babu Kachefukwa" kudadadadeki. Na Hii inatokana na baadhi Coments za bandugu kuwa alifanya mchapio katika Mpangilio wa Mavazi.

Kama utakuwa ni Mfuatiliaji Mzuri sana wa Akothee, utakuwa unafahamu namna ambavyo raia wengi wa Kenya walimchamba na kumlambisha Ndimu baada ya kuonekana amevalia Kivazi cha Kuogelea wakati wa OUTING ambayo inasadikika kuwa ni ya Usiku.

Tofauti na kuvalia Kivazi hicho, Pia kwa ndani, Akothee alikuwa amevalia Skin Tight Nyeusi sambamba na Viatu Virefu Vyeupe, mkononi akiwa ameshikilia Pochi Kubwa Nyeusi na Simu yake, na masikioni akiwa na Headphones Kubwa

Sasa Baada ya kuchambwa sana, Akothee aliamua kutoa Uvivu na kumjibu shabiki aliyeanzisha Ndimu hiyo.. kwa kumwambia kuwa, akacheki yeye mara ya Mwisho, amebadilisha Nguo ya Ndani Lini.

NUKUU
" Kama unaliita hili ni Vazi la Kuogelea kwenye Maswiming Pool, Well, sikulaumu kwa kuwa umekuwa ukiziona kupitia Internet, na Tunaelewa hilo. Sikiliza, Nisipojibu kwenye coments zenu, ni kwa sababu ninataka niwe mtu mzuri na mstaarabu. Ila ninaweza kuwamaliza baadhi ya watu hapa hapa, kwa Sentensi moja tu. Nenda Mkatizame Mara ya Mwisho Mmebadilisha Nguo zenu za ndani ni Lini. Sio za Mwaka 2014?.. Nimeuliza Tu"

VIDEO: RAPPER P DIDDY AMEANDIKA BARUA KWA JARIDA LA FORBES WASIMUWEKE TENA KATIKA ORODHA YA WASANII WA HIP HOP WENYE PESA KWA SABABU HIZI MBILI

12:00:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.
P. DIDDY  kwa Mwaka huu pia alitangazwa na Forbes kuwani Msanii wa Hip anayeshikilia namba 1 kwa kumiliki mkwanja Mrefu kuliko wengine wote Dunia, kitu ambacho kimekuwa ni Muendelezo kwa Msanii huyu wa Hip Hop na Mjasiliamali pia.

Lakini Jambo ambalo Diddy amelisema ni kwamba, alichukua Uamuzi wa Kuwaandikia Barua Forbes kuwa, anawaomba wasimuandike ama kumuweka katika Orodha hiyo kwa Miaka inayoendelea kwa Sababu kuu mbili ambazo kwake ni za Msingi na hata jamii itaelewa kabisa.

Sababu yake ya kwanza ni kwamba, Forbes wanavyomuandika vile kuwa ana mkwanja wa kiasi hicho, Basi wengi huamini kuwa Rapper Huyo ana pesa hizo katiika account yake ya Bank, kitu ambacho sio Kwel;i, kweny account yake hana kiasi Hicho, ila Namba hiyo hutokana na Harakati anazofanya pamoja na makadirio ya kiasi cha fedha, ingawa ni kama Baraka kwake

Sababu Kuu ya Pili, Diddy amedai kuwa, hivi sasa hataki na hapendi kuwa maarufu kwa kuongoza kumiliki kiasi kikubwa cha fedha, bali anatamani kuwa maarufu na hata kuheshimika zaidi kwa kutoa Misaada, na anatamani akamate namba moja katika Hilo.

MNADA BANNER