REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WATU WANATAFUTA PESA: KUTANA NA MREMBO HUYU ANAYETENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA KWA KUPOST MIGUU YAKE INSTAGRAM

3:00:00 AM Add Comment

Na Rich Sam: 
WAUNGWANA bwana, kuna baadhi ya Watu wana akili ya Ziadaa kupita maelezo, na hii ni kwa sababu ya kutengeneza mkwanja ili waweze kuishi

Kutana na Mrembo ambaye pia ni Model, JESSICA GOULD ambaye ni raia wa Canada, anayetengeneza takribani 140,360,000 kwa Mwaka, ikiwa ni kwa kupost tu picha za Miguu yake hasa Nyayo zake kunako Instagram

Binti huyu ambaye ana umri wa Miaka 37, hupost Picha mbali mbali za miguu yake hasa Nyayo, akionesha Mapozi tofauti na followers wake ambao ni zaidi ya 10,000 katika Instagram yake, na kupata Likes Nyingi na commnents nyingi huku akiingiza Mamilioni hayo ya Pesa.

Picha lilianza ambapo alipopost Picha yake ya kwanza akiwa anaonesha unyayo wake, na kilichokuja kumshangaza ni baada ya kupata DM Messages nyingi kutoka kwa Wanaume ambao wanavutiwa sana na miguu mizuri ya wanawake, ambao huitwa "FootBoys"

JESSICA anaongeza kuwa, awali alishtuka sana kukutana na Maombi mengi sana ya wanaume ambao wanatamani kuona picha za Miguu yake mara kwa mara, na ndipo alipokuja kugundua kuwa kumbe anaweza kuingiza mkwanja kwa kufanya hivyo, na mpaka hivi sasa, maisha yake yanasogea fresh sana

Pia anaongeza kuwa, Wanaume wengi wamekuwa wakimtumia Message na kumuomba awe anawaonesha sehemu mbali mbali za Nyayo zake hasa kisigino, Upande wa Kanyagio, na hasa Urembo wa Kucha zake, kitu ambacho kilimfanya ajikite zaidi katika kuijali miguu yake na kuiremba zaidi

IMEBAINIKA NI KWELI: RAPPER MKONGWE MASTER P ANA SUGAR MAMY WA KIZUNGU

2:29:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WAUNGWANA bwanaaaa, tunaamini kabisa kuwa kila mtu anamfahamu vizuri mtu anayeitwa Master P ambaye pia ni Producer Mkongwe, Rapper Mkongwe na Baba wa Rapper Romeo.

Lakini ukiacha sifa hizo  ambzo tumeanza nazo hapo Juu, Master P pia anafahamika na kusifika kwa Kumiliki Mkwanja Mrefu sana ambao unakadiriwa kufika mpaka USD Milion 500 sawa na Zaidi ya Bilioni 900 za kitanzania, kitu ambacho kila mtu hakukipa uzito , lakini uzito uko katika Hili, Jamaa ana SUGA MAMA ambalo linamiliki mkwanja si kitoto

Kipindi cha Nyuma kidogo ziliwahi kuibuka Tetesi kuwa Rapper Huyo kahongwa Gari aina ya ROLLS ROYCE, gari ya Gaharama na Shuga Mama huyo, lakini bado haikuwekwa wazi kuwa Mwanamke huyo ambaye ana asili ya Kizungu alikuwa ni Partner wake kibiashara ama Ni Mupenzi kweli,

Lakini hivi majuzi, kila kitu kimeanikwa hadharani kuhsu Suga Mama Huyo

Suga Mama huyo wa Master P, anaitwa Simin Hashemizadeh, ambaye ni CEO wa South Pacific Surgery Centeriliyoko Beverly Hills, Califonia

SUNDAY BABE: HAVE YO SEEN RUBBY? LETS SEE

2:53:00 AM Add Comment

INSTACOP
On This Sunday, Let me take you to this Cute Lady from Tanzania. She goes by the name RUBBY, and believe me, she has the Cutest Voice that you cant Imagine

Infact, she has been quiet for while in the industry, but that does not make her go away from social networks (such as instagram).

One the cutest quotation from her, was this.... which she posted on her instagram account
"If you pay too much attention to people you will surely perish!ignorance is a bliss I tell you..!"

Today, I have decided to Remind you that, the Chagga Gir is active and shinning well in her instagram account, thats why we made her the "SUNDAY BABE"

Take a look at her Pics:





VIDEO: MWANA FA x AY x FID Q- UPO HAPO?

2:39:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
WATU wa Mungu kuna Mzigo Mpya huu hapa kutoka kwa Rappers Watatu Hapa Nchini Tanzania ambao pia wana historia pana zaidi na Muziki wa Kizazi Kipya hapa Nchini Tanzania

Wamekusanyana FID Q, MWANA FA, na AY ambao wamekunjua Video iliyopewa jina la UPO HAPO.

Audio imekunjwa kutoa Studio za B HITZ chini ya Hermmy B huku Video ikisimamiwa Poa na Director Alessio kutoka Kampuni ya Studio Space Pictures (SSP)
CHECKI

WACHA KUZUBAA WEWE !!! : AMBER ROSE ANASEMA KUWA TENDO LA NDOA NI KAMA VITAMIN !!!!

2:28:00 AM Add Comment

Na Rich Sam
WAZEE Wa Kazi ni wangapi ambao mnaungana Mkono na Huyu Bibie Amber Rose ambaye alijipatia Umaarufu kwa Kukunjuka na Kanye West na Kisha kuolewa na kuachika kwa Rapper Wiz Khalifa?

Ukiacha Mbali hayo yote, Amber Rose ambaye hivi sasa anaonekana kupigwa "Mdenge" Mkali na Boyfriend wake ambaye pia ni Rapper, 21 Savage, anaonekana kabisa kuwa "amedata" haswa na na jamaa huyo kiasi cha kuamua kuanika mara kadhaa namna ambavyo anafurahia kufanyiwa vizuri Tendo la Ndoa na Rapper Huyo

Sasa Hivi majuzi akiwa maeneo ya BEVERLY HILLS, amber Rose alidai kuwa "Sex" ni jambo zuri sana kwake na ni lazima afanyiwe Kila siku maana linaleta afya na ni kama Vitamins kabisa

Kauli Hiyo aliitoa wakati akiulizwa kama atahitaji zawadi ya "tendo la Ndoa" katika Birthday Yake, na kujibu kuwa yeye hana haja ya kuomba Kitu hicho siku ya Birthday yake, maana anaomba kila siku

" Ninaomba Tendo la Ndoa kila siku. Inaleta Afya sana."

MAKUBWA !!!!: ASHANTI ANATUHUMIWA KUHARIBU BIKINI YA DESIGNER

2:05:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
WAUNGWANA Bwana, weekend Hii ilikuwa ni Mbovu sana kwa Mrembo ASHANTI ambaye alikamuliwa "Ndimu: bila kifico na mmoja kati ya Designers kutoka Nchini Marekani

Designer Huyo aliyetambulika kwa Jina la AIDAN EUAN, aliamua kuliamsha Dude kupitia Instagram account yake na kudai kuwa Amechukizwa na Kitendo cha Ashanti Kurudisha Bikini ambayo alimuazima kwa ajili ya Shughuli Maalum,ikiwa Imeharibika

Akifunguka Bila Ubishi, Designer Huyo alidai kuwa Ashanti na Timu yake walifika katika Duka Lake na kuhitaji wapewe Mzigo huo kwa ajili ya Shughuli Maalum na yeye kufanya Hivyo, lakini kilichokuja kumuumiza, ni bada ya Team ya Asha kurudisha Bikini Ile ambayo ilimgharimu Muda kuiandaa ikiwa imeharibika na kuchafuka hatari

Ninamnukuu tafadhari kwa uchache tu
"ASHANTI unaonekana Mrembo sana katika kampeni yako ya Ciroc. Lakini nimejitahidi kutumia Njia ya Busara kumtafuta Stylst Wako na Timu yako Nzima lakini sijafanikiwa kupata ufafanuzi na majibu ya Bikini Yangu iliyoharibiwa na kuletwa hivyo hivyo na Timu yako. Ni aibu kwa wamiliki wa Biashara wadodogo wadogo kupitia njia ya Mitandao kama mimi, kukaa kimya na kuogopa kuharibu sifa na hata kupteza wateja wengine wakati tumetumia nguvu, moyo kuwekeza na kufanya kazi kwa juhudi kubwa katika kile ambacho mtu atakichukulia kama Bikini ya Kawaida. Bikini hii kwa mfano kama nilivyosema awali, imetengenezwa kwa Mkono kwa masaa 16 huku ikitumia vitu vingi vya gharama......"

Mpaka hivi sasa , Ashanti hajajibu Chochote kuhusu Hili, lakini Tunazo Picha akiwa amevalia na kujiachia na Bikini Hiyo ambayo inadaiwa kurudishwa ikiwa Imeharibika Balaa





WANAWAKE WA NYERI, KENYA: "HATUTOTOA UNYUMBA KWA WAUME ZETU MPAKA WAMPIGIE KURA UHURU KENYATTA"

2:10:00 AM Add Comment

Na Nyangi Kimani  
Kenya kuna Mambo Mengi sana yanatokea lakini kuna hili ambalo tunaomba mulisikie ili kuweka hali halisi wazi wazee wa kazi

Wanawake kadhaa kutoka Nyeri, Nchini Kenya, wamesema kuwa hawatotoa "Unyumba" kwa waume zao kama hawatompigia Kura Uhuru Kenyatta .

Wanawake hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Waume zao wengi wamekuwa wakipeana taarifa za kutokumkubali Uhuru Kenyatta na kupanga kutokumpigia Kura hata kidogo, kitu ambacho kimewafanya na wenyewe wafikie maamuzi mazito ya kuwanyima "unyumba" waume zao hao kama Tarehe 26 hawatoweka "Tik" kwenye jina la UHURU KENYATTA

Kauli hizo zilitoka katika Mkutano wa wanawake hao na Mwakilishi wao ambaye ni Mbunge Pia, RAHABU MUKAMI, ambapo waliapa kuwa, ifikapo Tarehe 25 Usiku, wanawake hao watabania "NUNU" zao ili waume zao wakione cha moto na hata kuamka mapema ili wakapige Kura Tarehe 26 na wampigie Uhuru Kenyatta.

ALICHOKISEMA THE GAME KUHUS KUMPA UJAUZITO BINTI WA MIAKA 15 KIKO HAPA

1:42:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu kama mko "active" sana katika Mitandao ya Kijamii, mtakuwa mmekutana na Skendo mpya tena ambayo inamkabili Rapper The Game, maana mzee huyu amekuwa ni mwingi wa Majanga lukuki.

Kama hukufahamu, ni kwamba, kumekuwa na taarifa ambazo zinazagaa sana kuwa The Game amemjaza Ujauzito Binti mwenye Umri wa Miaka 15, kitu ambacho kilishtua sana kiukweli.

Lakini baada ya kukutana na "Ndimu" nyingi sana kunako Twitter hasa zikimlaumu sana The Game kumjaza ujauzito Binti huyo mwenye Umri Mdogo ukizingatia imekuwa ni mara kwa mara akionekana kumendea Vibinti vidogo Vidogo, hatimaye The Game kaamua kutoa Jibu Sasa

Akifafanua kuhusu hilo, The Game alidai kuwa, hakuna ukweli wowote na wala hajawahi kukutana na binti huyo ambaye kwake bado ni kinda sana

Tunamnukuu:
Taarifa hii ni Uwongo Mtupu, ambao umeandaliwa na kitoto ambacho hata sijawahi kukutana nacho au kuongea nacho maishani mwangu. Natamani Media kubwa zingacha kabisa kutoa taarifa za uwongo na uchochezi,maana zinaharibu Brand zao, na kuonekana kama ni uchafu tu"


KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI KAKA YAKE NA NICKI MINAJ, MAMBO BADO NI MOTO !!!!... SAFARI HII IMEFIKA PABAYA ZAIDI

1:20:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
KESI ya Ubakaji ambayo inamkabili Kaka wa Nicki Minaj, Jelan Maraj, imeendelea kusikilizzwa na safari hii kumeibuka madai mapya ambayo kila mtu ameonekana kushtushwa nayo kiukweli

Kwa Mujibu wa Jelan Maraj, inasemekana kuwa, Familia ya Binti anayedaiwa kubakwa akiwemo mama yake mzazi, walitumia kesi hiyo kwa ajili ya "kuitikisa" familia ya Nicki Minaj hasa Nicki Mwenyewe, ili kuvuna mkwanja.

Akifafanua zaidi kuhusu Madai Hayo, Mwanasheria wa Jelani Maraj, DAVID SCHWARTZ ambaye haukwa na ugumu kuliweka wazi jambo hilo mbele ya mahakama, alidai kuwa Mama wa Mtoto huyo ambaye ni wa Miaka 12, alimpigia Simu Nicki Minaj na kumwambia kuwa anatakiwa amlipe USD Milioni 25.

Mwanasheria huyo aliongeza kuwa, Mama wa Mtoto ambaye anadai kubakwa, alikuwa ni Mke wa Jelani Maraji kwa Takriban Miezi minne, hivyo aliunda kila aina ya Mbinu kuhakikisha kuwa anapandikiza Kesi ya Ubakaji kwa Kaka wa Nicki Minaj ili kuweza kuvuna mkwanja huo na ndio maana alitumia kila mbinu kuwasiliana na Nicki minaj, huku akitoa vitisho kuwa, endapo Mkwanja huo hautotolewa, basi atatoa Taarifa kwa watu kuwa alimbaka Binti yake

Mwanasheria huyo alidai hivi:
"Haitengenezi mantiki yoyote kwa mzazi kumtumia mtoto wako kutengeneza Pesa hata Kidogo> Mama huyu alifikia mpaka hatua ya kuchukua mbegu za mumewe na kuziweka katika Nguo ya ndani ya Mtoto wake ili aonekane amembaka"

MAHAKAMA
Baada ya kusikiliza Malalamiko ya Pande zote mbili hasa Utetezi uliofanywa na Mwanasheria wa Jelani Maraji, Mahakama ilitoa Taarifa kuwa, licha ya hayo yote kusemwa, bado inaonekana kuwa Jelani alianza kumrubuni Binti huyo wa Miaka 12 kipindi ambacho Ndoa yake na mama wa Mtoto ilikuwa katika wakati mgumu kutokana na Ugomvi wa hapa na Pale pamoja na Ulevi wa kupindukia ndani ya Nyumba
 Mwanasheria Msaidizi wa Jimbo la Nassau kwa ngazi ya Wilaya,  EMMA SLANE aliiambia Mahakama kuwa, Maraj alianza kuwa karibu na binti huyu kwa kuanza kumbusu, kumtomasa tomasa mara kadhaa na hata kuingia naye chumbani (kwa binti)

"  Alikuwa akimchukua na kumpeleka Chumbani kwake, kisha anamuinamisha na kupitisha MDENGE wake katika Uke wa Binti Huyo. Hata Hivyo, binti huyo pamoja na mdogo wake wa miaka 8, walikuwa wakimchukulia mtuhumiwa kama baba yao mzazi. Lakini mambo yalibadilika baada ya Mdogo wa Binti kuingi chumbani kwa Maraj na kumkuta baba yake wa kambo akifanya tendo la Ndoa na Dada yake. Baada ya maraj kuona hivyo, alimpiga Mtoto huyo wa Kiume makofi na kumtishia kumfanyia jambo baya kama angemwambia mtu yeyote"

Pia Slane aliongeza kuwa, Mpaka Kesi inakuwa Kubwa kiasi hicho ni baada ya Mtoto wa kiume kutoa taarifa katika Kitengo cha Kulinda haki za watoto kuhusu kitendo alichofanyiwa Dada Yake

UTAFITI: MTUMIAJI WA POMBE ANAWEZA KUJIFUNZA KUTUMIA LUGHA NYINGINE (YA KIGENI) KWA UFASAHA ZAIDI

2:47:00 AM Add Comment

Na baba Juti
UCHUNGUZI umefanyika na kubainika Kuwa Unywaji wa Pombe unaweza kumfanya Mtu akazungumza Lugha za mataifa Mengine

Uchunguzi huo umebaini kuwa, unywaji wa Pombe kiasi fulani (hasa Kidogo) kinaweza kumfanya Mtumiaji akawa na ujuzi wa Lugha Nyingine hasa kutoka mataifa Mengine

Team ya Utafiti Kutoka Liverpool Uingereza, Vyuo Vikuu vinavyofahamika kwa Majina ya MAASTRICHT UNIVERSITIES,  Na KING'S COLLEGE zilitoa taarifa kuwa, unywaji wa Pombe husababisha athari ama hudhuru sehemu kadhaa za binadamu ikiwemo Nguvu ya Kufanya kazi kwa Ubongo, na Nguvu ya Mwili.

Tofauti na hayo, Ilidaiwa kuwa kupoteza kumbu kumbu, kukosa nguvu na uwezo wa Kufikiria, lakini pia uvivu wa kimwili, husababishwa na Unywaji wa Pombe

Ila sasa, kuna faida mpya ambayo imebainika safari hii, kuwa kunywa Pombe kunaweza kumfanya Binadamu akatumia Lugha zaidi ya Moja hasa zile kutoka Nje ya Nchi ambayo binadamu husika anatumia Lugha yake Mama au ya kitaifa.

Pia watafiti hawa Wapya wameongeza kuwa, Pombe hujenga Ujasiri Binafsi kwa Mtumiaji na hata kutumia Fursa hiyo kuzungumza na mwenzake ama wenzake ama Wenyewe Lugha Nyingine za Kigeni zaidi kuliko hata Lugha yake Mama

Hivyo, kwa utafiti wa Awali, imegundulika kuwa, Mtumiaji wa Pombe kwa kiasi fulani, hata kama hajui, huweza kukusanya hata maneno mawili matatu licha ya kuchapia katika lugha ya kigeni, lakini atazungumza na kueleweka kwa kiasi Fulani


Pia Mtumiaji wa Pombe, hupendelea mara kwa mara kutumia Lugha Nyingine tofauti na ile ambayo huizungumza siku zote katika Majukumu yake ya kila siku

Mmoja kati ya Watafiti, Dr. Inge Kersbergen kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, taasisi ya Saikolojia, Afya na Jamii alisema Hivi, tunamnukuu
" Utafiti wetu unaonesha kuwa unywaji wa Pombe, unaweza kuwa na manufaa katika kutamka maneno ya Kigeni hasa kwa wale ambao anagalau wameshajifunza Lugha hiyo. Hii pia husaidia ama huleta faida ya kujifunza zaidi hasa ukiizungumza ukiwa na wale ambao wanaifahamu lugha husika kwa ufasaha zaidi"

SIKU YA HESHIMA DUNIANI: VANESSA MDEE ANASHUKURU KUIMALIZA VIZURI NA WANAFUNZI WA AGAKHAN MZIZIMA SECONDARY SCHOOL (PICHA)

2:05:00 AM Add Comment

Na Insta Cop  
SIKU ya jana, October 18, ilikuwa ni Siku ya Heshima Duniani (Global Dignity Day) ambayo hufanyika Kila Mwaka katika Mataifa Mbali mbali

Lakini kwa Mwaka huu, Mahali fasaha pa kuiadhimisha , ilikuwa ni katika Shule mbali mbali Duniani, ili kutoa hamasa kubwa na heshima kubwa kwa wanafunzi mbali mbali ambao wamekuwa wakijituma zaidi katika masomo na malengo yao ya Baadaye.

VANESSA MDEE, maarufu kama Vee Money, alikuwa katika Shule ya AGA KHAN MZIZIMA SECONDARY SCHOOL iliyoko Dar Es Salaam kwa ajili ya kujumuika na wanafuzni wa Shule Hiyo

Hivi Ndivyo ilivyokuwa








NICKI MINAJ: "NITATOA $ 100,000 KWA ATAKAYENIPA USHAHIDI JUU YA HILI"

1:45:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAUNGWANA wameamua kumfanya Nicki Minaj apate Hasira za kutosha mpaka kutangaza Dau la USD 100,000 kwa yeyote atakayempatia Ushahidi ambao mpaka hivi sasa umemuweka katika wakati mgumu hapa Duniani aisee

Hitmaker Huyu wa "ANACONDA" alijikuta akimiminiwa "Ndimu" za Kutosha ikiwa ni baada ya kudaiwa kuwa aliropoka kwamba yeye ndiye kawafanya Wasanii Wote wa Rap kwa Jinsia ya Kike wawe katika Ramani ya Muziki, kitu ambacho kwa upande wake amekikanusha na kuamua kuandika walaka Mrefu sana kupitia Instagram account Yake.

Katika Post alioipost bibie huyu baada ya kukutana na janaga hilo, aliandika kuwa, anahitaji kuweka sawa kuhusu kauli hiyo ambayo imenukuliwa Tofauti na Mitandao ya Kijamii na Tv Station mbali mbali, huku akimtaka yeyote yule atakayeona "nukuu" hiyo, basi amcheki na kumpatia USD 100,000.

Tunamnukuu tafadhari
     NICKI MINAJ     
"Ninanona Watu wana-remix maneno yangu, hivyo ngoja nipost kile nilichokisema haswa kwa wale ambao wana uelewa. Sasa, kama utapata Sehemu ambayo nilisema "Nimewafanya Rappers wa Kike kuwa katika Main Stream", nitakupatia USD 100,000. Blogs na Tv shows mbali mbali huwa hawajalishi utafiti, huwa wanajali kuchukua hisia zako. Hebu fikiria mie kusema nimewaweka katika Ramani ya Muziki rappers wa Kike wakati kuna wengi ambao tayari walishaingiza albums zao Platnum kupitia Nguvu zao. Lauryn mpaka nakala Milion 10 ya moja kati ya Albam zake. Eve alikuwa na Nyimbo zilizogusa Pltnum akiwa na Alicia Keys, Gwen Stefani, Tv Show yake na Mavazi yake, Missy Eliot Pia Nyimbo zake. Foxy Brown na Lil Kim walikuwa Album ambazo ziliingia Pltnum na walitengeneza vizuri Sound ya Wasanii wa Kike wanao Rap kutoka New York. Akina Queen Latifah, Trina naye alikuwa na Album ambayo ilifika mpaka Billboard. Ninapenda sana upendo wa watu lakini sijawahi kusema hivyo.........."


I see ppl remixing my words so let me post "exactly" what I said for the intelligent ones in the back. Now, if you can find the part where I said "I made female rappers mainstream", I'll give you $100,000.00. 😅 blogs & tv shows don't care to do actual research these days, they only care about what grabs your attention... at anyone's expense. Imagine me saying I made female rappers mainstream when there were so many women who already had platinum albums under their belts. 🙃 Lauryn sold 10 million off one album, Eve had platinum singles w/Alicia, Gwen Stefani, her own tv show & clothing line. It doesn't get more mainstream/pop than Missy's biggest singles. Foxy&Kim had platinum albums & shaped the sound of NY female rappers, Latifah had her own sitcom, Trina was on billboard with hits, etc-🙂 I appreciate the love but I never said that. 🦄🦄🦄 now what I DID say is right here for anyone w/their own brain to decipher words on their own. I know it's hard in the social media band wagon era, but try. It's fun. 🙈. When I came out, there had been a drought of a few years where NO female rap album had gone platinum, females weren't getting budgets, the industry did NOT believe in the female rapper anymore. They had stopped generating MONEY for labels. Ask any rap historian or just anyone with a brain. These are facts and nothing but the facts. So I "REINTRODUCED" the "successful" female rapper back to POP CULTURE. Showed big business we were major players in the game just like the boys were. ♥️😍😘 love you guys for holding me down but what's true is true & whats not is just simply not. 🙂 update your blogs & tv shows with what I actually said please 🙄🤣. I can't believe this lil interview made it to tv. Haha. See u guys on tour next year. I got a cpl BIG surprises. AHHHHHHHHHH!!!!!!! 😘
A post shared by Barbie® (@nickiminaj) on

MAHABA NIUE !!!: JENNIPHER LOPEZ ANAUZA NYUMBA YAKE KWA SABABU ANAHITAJI KUISHI PAMOJA NA ALEX RODRIGUEZ

1:21:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
JENNIFER LOPEZ kwa Kinywa Chake alitamka Rasmi kuwa mahusiano yake na Alex Rodriguez ndiyo mahusiano yake Ya Kwanza kabisa kufurahia, na hilo limeanza kuthibitika rasmi.

Mahusiano hayo ambayo yameanza mwaka huu wa 2017, yanaonekana kupiga hatua nzuri kadri ambavyo siku na Muda unavyosonga Mbele mpaka kufikia maamuzi ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyafanya.

Jennifer Lopez anasadikiwa kuiweka Sokoni Nyumba yake ya Kifahari iliyoko NEW YORK Marekani hivi sasa, maana anahitaji kuishi Pamoja na Mpenzi wake huyo Alex Rodriguez.

Taarifa zinazidi kumiminika kuwa, Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wawili hao kuanza kuishi pamoja na kuanza kutekeleza Mipango yao Muhimu zaidi katika Maisha yao, Mapenzi yao, na Kazi zao

Tofauti na Hilo, wawili hao wanatajwa kuwa, wako katika Harakati za kuwekeza pamoja katika Biashara zao za pamoja ambazo zitazidi kuwaweka imra katika Mahusiano na maisha yao kiujumla

NDOA YA BIRDMAN NA TONI BRAXTON HAIPO WAUNGWANA JAMANI !!!!!

1:12:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
#WatuWaMungu kumekuwa na Taarifa ambayo Pia kupitia Sehemu kadha wa kadha zimekuwa zikizungumzwa sana kuhusu "ndoa" ya wapenzi wawili BIRDMAN na TONI BRAXTON ambayo inadaiwa kuwa ni Ya Siri na ilifungwa Miezi miwili iliyopita.

Taarifa hizo pia zilitolewa na chanzo aminifu kabisa ambacho kipo karibu na "wapenzi" hao kwa kudai kuwa Birdman hakutaka kabisa Ndoa yao ijulikane ingawa wapo mbioni kuandaa Sherehe yao maalum hivi karibuni ikiwa ni njia ya kujitangaza Rasmi kuwa tayari ni Mke na Mume

Sasa Siku ya Jana, Taarifa Nyingine zimeibuka na kukana kabisa kabisa kabisaaaaaa !!!...kuwepo kwa Ndoa ya Birdman Na Toni Braxton

Msemaji Maalum wa Toni Braxton alidai kuwa Bibie huyo hajasema "I Do" kwa Rapper Huyo Mkongwe na Mwenye "Mkwanja" mrefu, ila Bado wanadate tu.

Katika kuongezea juu ya hilo, Msemaji huyo alisema kuwa hivi sasa Toni Braxton ana mkwaju unaoitwa "DEAD WOOD" ambao utatoka kwenye Album yake mpya ya SEX & CIGARETTE itakayoachiwa Rasmi 2018

MNAONAJE !!!: HUU NDIO MUONEKANO MWINGINE WA BARAKA THE PRINCE KATIKA SEKTA YA KICHWA

1:00:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu Hakuna Mtu ambaye anapenda kuwa na muonekano wake huo huo tangu alivyoanza ama kwa muda fulani, lazima tu atabadili kidogo ili awe tofauti.

Hii tumekuwa tukiiona kwa wasanii wengi sana hapa Duniani wakifanya hivyo, ili angalau kuwa na mvuto wa aina fulani katika mwili wake  na hata katika biashara yake kiujumla

Nchini Tanzania katika Muziki wa "Bongo Flava" kuna wasanii wengi ambao hubadili muonekano wao mara kwa mara, Mfano Mzuri ni Young Dee, Diamond Platnumz, Janjaro, Harmonize, Young Killer, na wengine wa kutosha

And This Time, Msanii ambaye Origin yake ni MWANZA, Barakah Da Prince au "The African Prince" naye pia katuletea Muonekano wake Mpya kichwani. Kama hujauona, basi hebu utizame tafadhari






MNADA BANNER