REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USIKOSE..HII NI HAKI YAKO YA MSINGI....FANYA HIVYO SASA..GOOD MORNING

2:32:00 PM Add Comment

HUYU NDIYE ALIYEMALIZA KAZI KABISA.....

12:45:00 PM Add Comment

Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.

Mrembo Catherine Masumbiga jana usiku ameibuka mshindi kwenye shindano la Unique Model lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam. Nafasi ya pili ilikamatwa na Cesilia Michael huku Amina Ayubu akikamata nafasi ya tatu







Washiriki waliongia tano bora.

CHAMBO RABA RABA KUSHUSHA "DOUBLE- DROP"

11:58:00 AM Add Comment


Here we Go !!
Young Disturbing Artist  RABA RABA Himself all the way from ROCK CITY, ameamua kupiga “Double Droping” kunako mwezi wa Kwanza mwakani, yaani 2013, ambapo anatarajia kudondosha Mkwaju wake mpya, utakaotoka katika Audio na Video kwa Wakati Mmoja.

Kupitia Account yake ya Facebook, Mkali huyo wa “raba raba” amemwaga hadharani kuwa amekuwa Kimya kwa Muda Mrefu sasa, so anarudi kwa ujio mpya kupitia Joint hiyo ambayo ataidrop kwa Mpigo na Video Yake. Jamaa mwenyewe kamwagika hivi :

“Sasa kwa kipindi kirefu nilikuwa Kimya. Narudi kwa ujio mpya. Napenda kuwaamba mashabiki zangu hasa pande za kanda ya ziwa, mwezi ujao natambulisha ngoma yangu mpya ambayo naamini mtaelewa nini nafanya. Nashusha mzigo kwenu Audio pamoja na video kwa pamoja. Napenda kuwaambia ni bonge ya ngoma zaidi ya ngoma ya kwanza iliyokuwa inatambulika kwa jina la RabaRaba. Kaeni tayari kwa ujio huu. Nawapenda shabiki zangu.”

TUNAUNGANA NA WANANCHI WA INDIA KATIKA MAOMBOLEZO YA MWANAMKE ALIYEBAKWA

11:47:00 AM Add Comment
Hivi Sasa Wananchi wa India hasa Wanawake, wapo katika Maombolezo mazito, baada ya Mwanamke aliyebakwa December 16,2012 na kusababishiwa majeraha na Maumivu makali, kufariki Dunia mapema leo hii.

www.joachimjunior.blogspot.com, inaungana na Wananchi wa India duniani kote kuomboleza Msiba huo uliosababishwa na Unyama Mkubwa.
Tuko pamoja kuhakikisha kuwa Unyanyasaji wa Wanawake Duniani kote unakomeshwa.
Mwenyezi Mungu aliaze Roho ya Marehemu Mahali pema Peponi, Amen
BWANA AMETOA, NA BWANA AMETWAA..JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE , AMEN

Imetolewa na 
Frank Magnus Joachim
C.E.O 

MAANDAMANO YA AMANI YAFANYIKA INDIA

11:16:00 AM Add Comment



Maelfu ya watu wamejiunga katika maandamano ya amani katika mji mkuu wa India, Delhi, kupinga kitendo kilichosababisha kifo cha mwanamke mmoja ambaye alibakwa na kundi la wanaume mjini humo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye bado hajatambuliwa, amekufa kutokana na na majeraha Jumamosi huko Singapore alikopelekwa kupata matibabu maalum.

Wanaume sita wanaoshikiliwa kuhusiana na tukio la kumbaka mwanamke huyo, sasa wamefunguliwa mashitaka ya mauaji.

Shambulio hilo la aibu lilifanyika tarehe 16 Desemba 2012 na kusababisha maandamano kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa wanawake nchini India.

Maafisa wawili wa polisi tayari wamesimamishwa kazi.

Mwili wa mwanamke huyo unarejeshwa India katika mazishi yatakayofanyika kwa siri kuepusha ghasia zaidi za waandamanaji.


"Kwa kweli wanawake wengi nchini India wanakabiliwa na kitisho katika maisha yao katika mambo mbalimbali kama vile kunapozuka ghasia, ukosefu wa huduma za afya, kukosekana kwa usawa, kupuuzwa, lishe duni, kutojaliwa kwa afya ya mtu na utu wake"

Polisi wa kuzuia ghasia wamefunga eneo la katikati ya Delhi ili kuzuia maandamano zaidi.

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh amesema anaelewa hasira ya wananchi, ametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kufanya India kuwa mahali salama kwa wanawake kuishi.

Maandamano pia yamefanyika katika miji mingine ya India ikiwemo Calcutta, Bangalore na Mumbai.

Mwandishi wa BBC, India anasema kwa zaidi ya wiki mbili, mwanamke huyo ambayo hajatambulishwa amekuwa ishara ya mateso makubwa wanayopata wanawake wengi nchini humo.

Amesema, hata baada ya mazishi, mawazo yataendelea, kwa wananchi kuisukuma serikali kuchukua hatua kuhakikisha namna haki za wanawake zinavyoweza kulindwa.

CHANZO: BBC NEWS

MNADA BANNER