REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

AKILI YANGU ILIVYO FINYU

2:09:00 AM Add Comment

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Fashion Hii isiingie Tanzania....Maana ikiingia tu, Dada zetu wataivaa hivi hivi, unadhani kwa akili yangu ilivyofinyu nitawaza nini, na kitu gani kitanitokea?
Nina akili Finyu jamani, Vitu vingine Msinishangae !!!!!!!!!!!!!!

HALI YA SAJUKI YABADILIKIA JUKWAANI, JIJINI ARUSHA

1:27:00 AM Add Comment
 Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.

 Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.


Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya kuwasalimia mashabiki wake
                                            *********************************************************

Na: Mahmoud Ahmad,Arusha

HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.

Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.

Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.

Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.

"Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”
alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi

Hata hivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.

Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.

“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”
alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba

CHADEMA WAKO TAYARI KUMSHINIKIZA RAIS KIKWETE...

1:17:00 AM Add Comment

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

Na Mwandishi wa TANZANIA DAIMA
 KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imemaliza kikao chake cha siku mbili jijini Dar es Salaam, na kuazimia kuanza Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa ajili ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete, atekeleze madai yao.
Katika kikao hicho, mbali na ajenda nyingine, wajumbe walipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji kutokana na maazimio ya kikao cha dharura kilichokutana Septemba 9, mwaka huu.
Miongoni mwa maazimio hayo, ilikuwa na kupata majibu ya utekelezaji wa madai yao katika barua rasmi waliyomwandikia Rais Kikwete kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Baadhi ya masuala hayo ambayo yaliazimiwa ni kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.

MHE. LOWASA AFUNGUA JOSHO LA KISASA...MONDULI

1:12:00 AM Add Comment
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo katika kijiji cha Mfereji Monduli juu 


  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu

  Wakazi wa kijiji cha Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani)


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya kuzindua josho la kisasa la Mifugo

MNADA BANNER