REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

INAWEZEKANA??? : MAMA HUYU ATASHTAKIWA KWA KUMFANYA MWANAE WA MWAKA MMOJA AGONGWE NA NYOKA MAKSUDI?

3:00:00 AM Add Comment

Na Baba Juti 
SOURCE : ABC NEWS
#WatuWaMungu kuna hili jambo ambalo natamani tulitafakari na kulizungumzia vizuri sote kwa pamoja ili tujue kama inawezekana au lah

Mwanamke mmoja Nchini Marekani katika Jimbo la Florida, huenda akafunguliwa Mashtaka ya kujeruhi na kutaka kuua, baada ya kuruhusu Nyoka amgonge Mtoto wake wa Kike mwenye Umri wa Mwwaka mmoja, kwa Makusudi kabisa

Tukio hilo limetokea Hivi karibuni  ambapo mwanamke huyo anayetambulika kwa jina la Chartelle St. Laurent aliruhusu tukio hilo kufanyika huku akirekodi kwa Njia ya Simu na kisha kupost katika Mitandao ya Kijamii


Hata Hivyo, Polisi kutoka Florida, inadai kuwa Kitendo hicho ni Kinyume cha Sheria na Kanuni ambazo zinalinda Haki za Mtoto mdogo hasa ambaye ana mwaka mmoja, maana huwezi jua madhara ambayo anaweza kuyapata na hata kupoteza Maisha

Akijitetea kwa ujasiri Mkubwa Mama huyo anadai kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kumfundisha Ujasiri Mtoto wake huyo na hata kuwa makini na vtu ambavyo ni hatari, yaani asizoeane na vitu ambavyo vinaathari….

“Mwanangu wa Kiume pia alishawahi kungatwa na wala haikumdhuru chochote hata kumuachia alama. Hata kwangu pia. Hivyo nilidhani ilikuwa ni nafasi nzuri kutambulisha tukio hilo kwa motto wangu wa kike pasipo yeye kudhurika. Tatizo ni kwamba, watu wana hisia sana. Wanadhani nimemdhuru mwanangu kwa makusudi. Watu wanaonifahamu, wanajua kabisa siwezi kumdhuru mwanangu. Meno ya Nyoka huyo ni madogo sana kuidhuru Ngozi ya mtu yeyote. Hivyo hajajeruhiwa hata Kidogo”



DAWA IMEFANYA KAZI !!!! : MUME “AGANDANA” NA MDOGO WA MKE WAKE WAKIFANYA TENDO LA NDO… MKE NA MGANGA WAONGEA !!!

2:12:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
SOURCE : K24-KENYA 
#WatuWaMungu kwanini Msitulie na Wake ama Wame zenu mpaka mje kuadhirika kiasi hiki lakini Aisee?... Kuna shida gani kwani kwenye Hizo “Naniliu” zenu Eti?

Nchini Kenya katika Mtaa wa Tanners huko Nakuru, Mwanaume mmoja (Jina lake limehifadhiwa) amejikuta akiaibika Mbele ya Umati wa Mtaa Mzima baada ya “Kugandana” na Shemeji yake, yaani Mdogo wa Mke Wake , wakati wakifanya Usaliti

Kwa Mujibu wa Tukio zima, Jamaa huyo ambaye Mke wake anamfahamu na kuelewa kuwa ni “Muasherati” kupita Melezo aligundua Fika kuwa kuna jambo ambalo linafanyika bila yeye kujua vizuri, na Ndipo akatega Mtego hupo ambao ulizaa Matunda, na wawili hao “kunasiana” usiku mzima wakati wanafanya Mambo yao, huku tatizo lao likibainika Kesho yake asubuhi

Akifafanua Vizuri, Mganga ambaye alipewa Kazi hiyo, alidai kuwa Mke wa Jamaa huyo alimfuata na kumlilia shida yake, na yeye kumuahidi kuwa atamkamilishia Kazi husika

Kwa Upande wa Mke wa Jamaa, anasema kuwa, amekuwa akinyanyasika kwa Muda Mrefu, na ndipo alipoona ni Bora aje Kumuona Mtaalamu huyo kwa ajili ya Shughuli hiyo

Lakini katika Hilo, Bado wadau huwa hawakosi la Kuongea, na Mashuhuda waliongea Hivi

Hata Hivyo, shughuli haikuwa Ndogo kama ambavyo tunadhani, Maana jamaa alilazimika kuachanishwa na Shemeji yake kwa Mchanganyiko wa Dawa ambazo zilihusisha Waganga wawili. 

Na Jamaa aliomba Msamaha, ingawa ndo tayari ameshakamatwa, huku akitakiwa kulipa Pesa ama Ada ya Huduma za Mganga



KULA WAYAAA !!! : RAPPER MMOJA “ALIMWA” KONDE AKIWA JUKWAANI NA KUPOTEZA FAHAMU PAPO HAPO

1:50:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Kama wewe ni Msanii wa Hip Hop, halafu ukaanda Show na kuanza kuwazingua Mashabiki, basi utazimia bila we Mwenyewe Kupenda

Rapper mmoja Maarufu kwa Matukio kadha wa kadha, XXXTENTACION, alijikuta akipokea Ngumi Nzito sana na shabiki mpaka kupoteza fahamu

Chanzo halisi cha Shabiki huyo kumtufua Konde Rapper XXXTENTACION akiwa jukwaani, ni kitendo cha Msanii huyo kupiga Mikwaju ambayo haikumuingia shabiki huyo ambaye alilipa Mkwanja Mrefu kuja kushuhudia Perfomance yake

Waliokuwepo eneo la Tukio wanadai kuwa, Rapper huyo ambaye pia alishawahai kusimamisha show kwa ajili ya kumsaidia shabiki wake aliyeumia , miaka kadhaa iliyopita, aliingia akiwa hana energy yoyote, jambo ambalo liliwafanya watu wengi kuanza kumrushia matusi ya hapa na pale

Lakini wakati akiendelea ku-perform, ghafla aliibuka jamaa from no where, na kumlima Ngumi heavy, mzigo ambao ulimfanya Rapper huyo kupoteza Fahamu

Walinzi ambao walikuwepo eneo la Tukio, walimuwahi Shabiki huyo na kumpa Vyake kidogo, huku wakimsaidia Msanii wao

Cha ajabu badala ya mashabiki wengine kuchukizwa na kitendo hicho, waklianza kushangilia huku wakiimba kwa sauti kuwa F- TANCION !!!


Hata Hivyo, Baada ya Muda kadhaa, XXTENTACION alijibu kupitia Instagram live kuwa anaendelea Vizuri

SHETTA: KAMA UMEONA "SS" BASI NI JINA LA STUDIO YANGU

1:45:00 AM Add Comment


Source:  HZB TV  
#WatuWaMungu tukubali tukatae haka ka Utaratibu ka Record Label naona kanaanza kama kutokusikika Masikioni mwa watu hasa kwa kila msanii ambaye ameshafanikiwa tayari

Lakini mpaka hivi sasa, kuna wasanii ambao kweli tunawaona wako Active katika Suala Hilo, akiwemo Chibu (WASAFI), Ommy Dimpoz (PKP), Baraka Da Prince (Bana Music), Quick Racka (Switch Records) na wengineo ambao tumewakaushia Kidogo

Kama ulikuwa ukikutana na Bidhaa za Shetta ambazo zina Logo ya SS, basi maana yake ni Srtudio yake ambayo inaitwa SHETTA SHOWBIZZ ambayo mpaka hivi sasa Official Producer wake ni JOBANJO

Lakini undani wa Studio hii ni kwamba Sio Record Label kama Wengi wanavyodhani, Ba;li ni Studio ya Kawaida, maana anaamini bado hajawa tayari kuwa na Record label

MNADA BANNER