REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DEEY CLASSIC NA PROJECT NYINGINE IN TOWN

8:41:00 AM Add Comment

DEEY CLASSIC ana jina Lake Kubwa Tu hapa Bongo baada ya Kuzalisha (Producing) Mikwaju kadha wa kadha ikiwemo DEAR GOD ya KALA JEREMIAH, na Nyinginezo Kibao kama JANA NA LEO ya YOUNG KILLA akiwa na STAMINA & QUICK RACKA

Apart From Music ambao ndio Sehemu kubwa ya Kipaji Chake, DEEY Mwenye makazi yake ROCK CITY Mwanza, akisukuma Beats na Voices katika Studio kali za REVOLUTION Sound, hivi sasa yuko na “Mkato” huu kwa ajili ya Friends Wote ambao wanahitaji Kung’aa.
Ziko Available kwa Bei ambayo Inakidhi Kiwango Chako..
MCHEKI Kupitia 0653 252 526 & 0752 420 903











2 FACE NA MKEWE ANNIE, WAMECHEFULIWA….WAJIBU MASHAMBULIZI.

12:31:00 AM Add Comment

MSANII Mwenye Heshima Yake Nchini Nigeria 2 FACE IDIBIA, pamoja na Mkewe ANNIE IDIBIA, Wameamua Kujibu mashambulizi baada ya Kuchafuliwa na Jarida la ICON WEEKLY, pamoja na Mtandao wa AFRICAN CELEB SPY Nchini Humo, ambao sasa Unafahamika THE AFRICAN EYE.

Kwa Mujibu wa habari Hiyo, Jarida Hilo la ICON WEEKLY liliandika Kuwa 2 FACE anatarajia Kupata Mtoto na Mfanya kazi wa Benki Nchini humo, anayefahamika kwa jina la TENIOLA

Jarida hilo linadaiwa kuandika Taarifa ya Uwongo zaidi Kuwa TENIOLA ambaye alikuwa ni ACCOUNTANT OFFICER wa 2 FACE IDIBIA kwa Muda Mrefu sasa, alikuwa na Mahusiano naye , huku Uhusiano huo ukizaa Matunda ya Kupata Ujauzito kwa mamito Huyo.

KATIKA Kutafuta Data zaidi, KITENGO CHA CHIMBUA CHIMBUA Kutoka TTM, Kilibaini Mtonyo Mwingine Kuwa, Eti, 2 FACE ambaye ni Baba wa watoto 7 Hivi sasa, alikuwa akimbembeleza TENIOLA Kutokuhusisha Ujauzito huo na ndoa yake, na kuacha Kuvujisha Siri Nzima, huku akimshawishi zaidi kwa Kumpa GARI.

Sasa basi, Wanandoa Hao baada ya Kuinyaka Stori hiyo ambayo ilihamishwa kama ilivyo na Mtandao huo wa Kijamii wa The African Eye, waliamua Kuvunja Ukimya na kusema Kuwa, Habari Hizo Si za ukweli na Zina Nia ya Kuharibu Jina lao na Familia yao Kiujumla, jambo ambalo si Jema hata kidogo.


Katika Tweets ambazo 2 face aliandika alidhihirisha Kuwa Upuuzi ulioandikwa na Jarida hilo pamoja na Mtandao huo, ni UZUSHI wa asilimia 100 bila kupinga kabisa, maana Habari hizo hazina hata chembe ya UKWELI 


CHECK TWEETS ZAO:





RIHANNA ASHINDA KESI DHIDI YA MUHASIBU WAKE………..

12:22:00 AM Add Comment

KAMA Utakuwa unakumbuka vizuri, Siku kadhaa Zilizopita TTM tulikupa Mchakato Kuwa RIHANNA anamshtaki MHASIBU WAKE kwa Kumsabababishia hasara Kipindi hayuko katika Suala Zima la Kiuchumi Miaka Kadhaa iliyopita.

SASA baada ya Kusikilizia kwa Umakini zaidi ili tufahamu kipi ambacho Kimetokea, FINALLY TTM tumezinyaka Kuwa, The beautiful Baby wa WE FOUND LOVE, Rihanna, ameshinda Kesi hiyo.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Rihanna, anayefahamika Kwa jina la EDWARD ESTRADA, amesema Kuwa, Mhasibu wake Huyo Peter Gounis alimshawishi Rihanna kununua Jumba la kifahari lenye Tjhamani ya Dola za Kimarekani Milioni 7 huko SOUTH CALFONIA, kipindi Hicho akiwa Si sawa kabisa Kiuchumi mnamo Mwaka 2009.

Tofauti na hilo, akaongeza kuwa, Mhasibu wake huyo huyo alimshawishi RIRI kununua Nyumba nyingine LOS ANGELS ili kuitumia kama Njia ya Uwekezaji hasa Kibiashara, lakini Mwisho wa siku mambo hayakuwa Ndivyo.

Mwanasheria Huyo alizidi kutonya kuwa, Bado Mhasibu wa RIRI  alimshawishi kufanya marekebisho makubwa yaliyogharimu Dola milioni 2 katika Nyumba hiyo ambayo haikuwa imara na ilihitaji marekebisho makubwa.

Aidha baada ya Kugundua Hilo, RIRI aliamua Kumtimua Kazi, na Kumfungulia Shitaka la madai ya Dola Milioni 35 Mwaka 2012.

Aidha baada ya Hukumu Kutoka, Mshtakiwa aliahidi Kurejesha Dola za Kimarekani Milioni 10, ili kumaliza Madai yake.

SOULJA BOY AWAAGA MASHABIKI WAKE..NI KATIKA SAFARI YA KUELEKEA JELA.

12:17:00 AM Add Comment

INAHUZUNISHA lakini hakuna Jinsi, Sheria inabidi kuchukua Mkondo wake.

Ladies And Gentlemen, SOULJA BOY TELL EM atatupwa Jela Wiki Hii kwa kosa ambalo kipindi cha Awali tulikugusia.

Kama Hukupata Chance ya Kusikia kilichotokea, ni kwamba The young Rapper huyo alikamatwa Huko LOS ANGELS Marekani kwa Kusa la Kukutwa na Siraha ya Moto (Bunduki) katika Gari lake, ikiwa Loaded, yaani tayari kwa Kufanya kazi.

Kupitia Tweet yake, SOULJA BOY amewashukuiru sana Marafiki zake wa karibu kwa Kuwa naye karibu katika Kipindi Chote cha Ugumu Kuhusu Kesi hiyo, na Kutoa Tamko rasmi kuwa, zimesalia Siku kama 2  alekee Jela Kutumikia kifungo Chake.

Katika Uendeshaji wa Kesi, SOULJA BOY alijitetea kuwa hakuwa na habari kama Kulikuwa na Silaha hiyo katika gari lake.

Aidha naye Meneja wa SOULJA BOY ametilia Mkazo katika Utetezi huo, kuwa kijana wake hakuwa na habari kama kulikuwa na Silaha ya Moto katika gari alilokuwa akilitumia Siku hiyo alipokamatwa

MNADA BANNER