REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

AKAMATWA NA BUNDUKI YA KIVITA

8:25:00 AM Add Comment




IGP SAID MWEMA



Na Edwin Moshi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Jonathani Charles Naftari (26) mkazi wa kijiji cha Uruila baada ya kukamatwa na bunduki ya kivita na risasi 37 ndani ya hifadhi ya Katavi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa hapo jana majira ya saa 8:00 mchana katika eneo la Kalumbi ndani  ya hifadhi ya Katavi akiwa na Bunduki Sub-Machine Gun  (SMG)yenye namba M22 – 13350 pamoja na risasi 37 zikiwa ndani ya magazine yake na risasi nyingine saba zilikuwa ndani ya mfuko wa serikali.


Mtuhumiwa alikamatwa siku hiyo kufuatia msako mkali ambao ulifanywa na askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya kataviKidavashari alieleza kuwa mtuhumwa ambaye alikuwa na wenzake watatu walipozungukwa na askari wa polisi na Tanapa na kutakiwa kujisalimisha walikataa kutii amri hiyo na ndipo walipoanza kuwafyatulia askari risasi hovyo kuwalenga askari


Ndipo askari walipojibu mapigo ya risasi na hatimaye majangiri hao walianza kutimua mbio na askari kwa ustadi mkubwa walifanikiwa kumkamata Jonathani na silaha hiyo ya kivita.Baada ya mtuhumiwa kukamatwa alipekuliwa na kukutwa na risasi saba ndani ya mfuko wa saluari pamoja ana panga na kisu ambacho kilikuwa na damu.


Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa alipofikishwa katika kituo cha polisi  alidai kuwa silaha hiyo ilikuwa ni mali yake na    yeye na wenzake waliingia ndani ya hifadhi kwa lengo la kuwinda wanyama.

"MADIWANI TOENI USHIRIKIANO"-IMELDA ISHUZA

8:21:00 AM Add Comment




Na Edwin Moshi
MAKETE


Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete wametakiwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu na Makazi wilayani hapo linalotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu


Akifungua mafunzo yahusuyo sensa kwa madiwani wa halmashauri hiyo mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amesema madiwani hao wana nafasi kubwa ya kuisaidia serikali kukamilisha zoezi hilo kwa kuwaelimisha wananchi waliopo kwenye kata zao


Pia Matiro ameongeza kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi halitaathiri shughuli za wananchi za kujipatia kipato hivyo kuwataka madiwani hao kwenda kuwaelimisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa zoezi hilo


“Waheshimiwa madiwani serikali inatambua nguvu mliyonayo kwa wananchi mnao waongoza, tunategemea ushirikiano wenu pindi mnapokutana na wananchi huko, tafadhalini sana mtusaidie kuielimisha jamii kuhusu suala la sensa ya watu na makazi itakayofanyika siku chache zijazo” alisema Matiro


Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Geofrey Masaki amesema serikali imelipa kipaumbele zoezi la sensa ya watu na makazi na ndio maana imeweza kutoa mafunzo kwa makarani wote watakao husika na utekelezaji wa zoezi hilo , na hata kwa wadau mbalimbali wakiwemo madiwani
 
Amesema wasisite kuielimisha jamii kushiriki katika zoezi hilo , na kutaka zoezi la sensa kutohusishwa kisiasa

Akizungumza mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo diwani wa kata ya Iniho ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Makete Mh. Jison Mbalizi, amesema anaamini yeye pamoja na madiwani wenzake wataielimisha jamii kuhusu umuhimu wa sensa na pia hawatarajii kuhusisha suala la sensa na siasa kama inavyodhaniwa na watu wengi

Pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuondokana na dhana potofu kuwa sensa haina umuhimu wowote na kuwataka wananchi hao kushiriki bila woga

Sensa ya watu na makazi itafanyika usiku wa Agosti 25 kuamkia Agosti 26 ikiwa na kauli mbiu isemayo sensa kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa



MARIAH CAREY AMTOLEA UVIVU NICKI MINAJ

8:17:00 AM Add Comment


Mariah Carey


Kimbembe cha AMERICAN IDOL katika Uteuzi wa Majaji umevaa Sura Nyingine Tena Kudadadeki

HALI IKO HIVI……..

Mariah Carey amtolea Uvivu Nick Minaji, mara baada ya uvumi wa Nick kuidhinishwa kuwa atakuwa Ni moja kati ya Majaji wa Shindano kubwa la American Idol kuzagaa.
Licha ya Uvumi huo kuzagaa kila kona kuwa Niki Minaji ameidhinishwa kuwa Jaji wa Shindano hilo, Taarifa nyingine zimetolewa mapema Leo Hii kuwa Msanii huyo wa HIP HOP hajawa Jaji RASMI kama ilivyokuwa
Kwa Mujibu wa TMZ, Maprodyuza wa Show hiyo ndio watakaoamua kama Randy Jackson abaki kwenye Panel ya Majaji wa Shindano Hilo, au wamtafute Mtu mwingine atakayeungana na Mariah Carey katika Pannel hiyo.
Imesemekana kuwa, kama ingekuwa ni Nafasi ya Mariah Carey kuchagua Jaji mwenzake, basi asingemchagu Minaji

 Nicki Minaji akiwa Mzigoni

MARIAH CAREY AKAKASIRIKA VILIVYO……..

Baada ya kusikia kuwa kuna Uwezekano Mkubwa wa Nick Minaji kuajiriwa katika American Idol, Mariah Carey alikata Simu kwa hasira. Sababu kubwa ya Mariah Carey “kumaindi” ishu hiyo, ni kuona kuwa anakuja mwanamke mwingine kuwa Jaji, tena akiwa amempiga Gepu la Miaka 13 kiumri, ambaye kwa ni Mtoto

Unamfahamu "BINTI YANGU?"...Huyu Hapa...

8:07:00 AM Add Comment








Gwiji la uigizaji katika tasnia ya filamu Swahiliwood Hashimu Kambi amejitosa rasmi katika uandaaji wa filamu akiwa mtayarishaji wa filamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la “Binti Yangu“, filamu hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilika na kuingia sokoni mwezi huu wa nane. Kwa mujibu wa Hashimu Kambi  kuwa filamu ya Binti yangu ni kazi yake ya kwanza ambayo ameiandaa na kuwashirikisha wasanii wakali lengo anataka kuelekea katika kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu za Swahiliwood.
Hasheem Kambi


Wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Grace Mapunda, Lucy Komba, Mohamed Funga funga ‘Jengua’, Heriety Chumila, Diana Exavery, Jennifer Raymond ‘Penina, Jumanne Mshindo, Hashimu Kambi ‘Ramsey’ na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu Swahiliwood.

KWA MASHABIKI WA RIHANNA HILI LINAWAHUSU......

7:51:00 AM Add Comment



Rihanna



Robbin Fentty “Rihanna” Bado anahisia kali kinoma noma dhidi ya aliyekuwa Mpenzi wake, Chris Brown “Chris Breezy- Pretty Boy”,

ILIKUWA HIVI…….

Hayo yamesemwa na Bibie Huyo katika Sehemu ya Pili ya Kipindi cha Mwana mama Oprah Winfrey, ambapo alibainisha kuwa aliwajibika na kuhusika  vilivyo kuhusu Brown kuliko hata yeye, baada ya Kudundwa na Mkali huyo wa R&B, alipokuwa akizungumzia kuhusu maisha yake katika Mahusiano ya Kimapenzi na Chris Brown
“Kila nikimuona Chris, huwa Napata wakati Mgumu sana, maana Bado ninampenda sana, na hilo halitotoweka kwangu kirahisi. Hisia zangu kwake zilikuwa ni za dhati kabisa”


INAKUWAJE AKIMUONA BROWN NA MPENZI WAKE MPYA…

Rihanna alidhihirisha Live kabisa kuwa huwa anajihisi kuumia sana pindi anapomuona Chris Brown na Mpenzi wake mpya Karruche Tran.
NI KWELI BHANA….
Pia mwanamama Rihanna alipoulizwa iwapo Chris Brown alikuwa ni Mwanaume wa Maisha yake, Rihanna alijibu….
“Ni dhari kabisa. Nahisi alikuwa ni Mwanaume wa maisha Yangu”


MNADA BANNER