REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WANAVYOSEMA !!! : ETI RIHANNA HANA MVUTO TENA JUKWAANI

2:26:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
WATU Wa Mungu kuna baadhi huwa wanapenda kuwa na muonekano wa Unene, na kuna wengine huwa hawapendi kuwa na muonekano wa Unene maana huwa kuna mengi sana wanashindwa kuyafanya.

Lakini ukiachilia hilo, kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakiandamwa sana na maneno ya Mashabiki wao hasa wanapoamua kujiachia na kunenepa, kitua mabcho wasanii wenyewe wanaweza kukipokea kama changamoto ama kikwafanya wakawa na stress sana

RIHANNA aliwahi kuzungumziwa sana kuhusu Unene alionao kwa hivi sasa na yeye akasema kuwa haimuumizi na wala haimtatizi katika kazi zake, lakini kwa hili, imebidi waseme tu

Katika Tuzo za Grammy zilizofanyika hivi majuzi tu, waungwana wanadai kuwa Rihanna amepoteza Mvuto wa Jukwaani ukilinganisha na kipindi cha nyuma alipokuwa mwembaba...kiufupi wanasema Rihanna hawezi tena kucheza, yaani amekuwa ni mzembe.

Wengi wanadai kuwa, Kipindi Riri yuko mwembamba, alikuwa ni mtundu sana jukwaani hasa katika Perfomance zake, lakini katika hili la unene, amekuwa hawakoshi mashabiki hata kidogo

Rihanna alionekana katika hali hiyo akiwa na DJ KHALED na Bryson Tiller wakiperform wimbo wa WILD THOUGHTS katika usiku wa Tuzo Hizo

INAUMA : BINTI AJIUA LIVE ONLINE ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU 10 AFUNGE NDOA, KISA EX-WAKE KAMTISHIA HILI .......

2:12:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
WATU wa Mungu hakuna kitu kinauma kama pale unapogundua kuwa Ex wako yuko Tayari kutoa Baadhi ya Siri zako za Ndani , siku chache kabla hujafunga ndoa na Mume Mpya, kiufupi inaumiza sana

Sasa Iko Hivi
NISHA DEVIDAS, Binti Mwenye asili ya kihindi kutoka Nchini humo humo, amejiua akiwa Live kupitia kupiia Mtandao wa kijamii (haijawekwa bayana ni upi) bvaada ya kupata vitisho kuwa Ex Boyfriend wake ataanika hadharani kuwa sio BIKIRA tena, siku chache kabla hajaolewa na mwanaume mwingine Mpya

Nisha ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha ROHINI Nchini India, alifanya tukio hilo zikiwa zimebaki siku 10 afunge ndoa na mume wake, na hii iloikuwa ni kuepusha kuadhirika pamoja na kuidhalilisha familia yake ambayo haikuwa ikifahamu kama marehemu tayari alishakutana na mwanaume kabla hajaolewa

Kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Familia yake ndiyo ilikuwa imeandaa Ndoa hiyo kwa ajili ya kuhakikisha Binti yao anaagwa na kuishi na mumewe, lakini mwisho wa Siku, Marehemu akiwa LIVE kwenye mtandao wa Kijamii, alikunywa Sumu kali na kisha kupoteza maisha yake huku mamia ya watu wakishuhudia tukio hilo.

Kaka yake anasema hivi, tunamnukuu
"Ndoa ya Dada Yangu ilikuwa ifungwe Februari 04 Mwaka huu, lakini akaamua kujiua zikiwa zimebaki siku 10. Mtu ambaye anahusika na kila kitu, ni Mwanaume ambaye alihusika kumdanganya dada yangu kuwa wafanye tendo la ndoa, kwa ahadi ya kumuoa, lakini mwisho wa siku akawa anampiga Chenga za hapa na pale, lakini tunashangaa alimuambia kuwa atamtangaza kuwa Hana BIKIRA endapo ataolewa na mwanaume mwingine. Naamini hicho ndicho kilichomuondoa Dada yangu duniani"

Hata Hivyo, baada ya kubainika kuwa amekunywa sumu, wahusika walijitahidi kumpeleka katika hospitali ya ya Wilaya ya BHANDARA ili kuokoa maisha yake, lakini bahati mbaya alikuwa ameshapoteza maisha


TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO-TCRA

12:13:00 AM Add Comment




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema
kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za
vidole.


Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka hiyo, Semu Mwakyanjala
alisema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.

Mwakyanjala alitoa ufafanuzi huo baada ya mwandishi wa Mwananchi kuuliza
kuhusu ujumbe unaotumwa kwa wateja kutoka kampuni za simu za mkononi
ukiwajulisha kuhusu usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

“Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole
zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea
maduka yetu,” ni ujumbe ambao umekuwa ukitumwa kwa wateja wa kampuni za
simu.

Mwakyanjala alisema mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni
wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.

“Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka
kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema.

Alisema TCRA imeziruhusu kampuni zote za simu za mkononi kutumia mfumo huo.

Akizungumzia mfumo huo, meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson
Mmbando alisema kampuni hiyo itaanza kusajili kwa majaribio.

“Ni kweli tutaanza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole kwa sababu
hiyo ndiyo njia salama ya usajili,” alisema.

Alisema katika mpango huo wa majaribio wataanza kusajili katika mikoa
minne ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, utafanyika
Zanzibar. “Katika mikoa hiyo tutaanza kusajili wateja wapya kwa kutumia
alama za vidole,” alisema.

Alisema baadaye wataendelea kwa wateja wengine hata ambao walishasajili
laini kupitia mfumo wa zamani. “Lengo ni kuboresha zaidi mfumo huu.” 

MNADA BANNER