REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

#DakaHiiFasta JASON DE RULO NI KINYOZI?

6:53:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
TOFAUTI na ishu nzima ya kufanya muziki, wasanii wengine wamekuwa na uwezo wa kufanya shughuli Nyingine kama kitu ambacho walianza nacho kabla ya muziki au kama ni kitu ambacho kilikuwa kichwani mwake na Muziki umekuwa kama Daraja lake.

JASON DE RULO yule yule wa "Wigle Wigle Wigle Wigle" tofauti na kufanya muziki ama kipaji cha Muziki, Ni Kinyozi hatari tena yule ambaye hategemei mashine, bali ni Kiwembe.

Akifafanua kuhusu Hilo, Jason De Rulo ambaye hivi sasa anadai kuwa hawezi kuzungumzia mahusiano yake, amedai kuwa, Kipaji cha Kunyoa, alikitoa kwa Baba Yake, ambaye zamani alikuwa akipenda kumnyoa pale ambapo alikuwa akibaini kuwa mwanae nywele zake hazijakaa poa.

Tofauti na kutokukaa poa, Pia Baba Yake Jason De Rulo alikuwa akimyoa pindi ambapo Bwana mdogo ahuyo alipokua akinyoa Style ambazo hazikuwa zinaingia akilini Mwake.

MSIKILIZE HAPA



#DakaHiiFasta KUTOKA KWA MTOTO WA MAREHEMU NOTORIOUS B.I.G

6:44:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
CHRISTOPHER JORDAN WALLACE maarufu kama CJ WALLACE ni Mtoto Marehemu NOTORIOUS BIG, ambaye ameweza kuunyaka Umaarufu Kupitia Kipaji tofauti na Baba Yake, Nazungumzia UIGIZAJI WA FILAMU.

Kama Ulikuwa Hujafahamu kuhusu Bwana Mdogo huyu ambaye mama yake ni FAITH EVANCE, ameweka wazi kabisa kuwa, Baba Yake alifariki akiwa na miezi 7, hivyo hakuufaidi utamu wa baba yake, kitu ambacho anakimiss hadi hivi sasa.
Lakini kitu ambacho kilikuja kumfanya Mtoto huyu aufahamu Umaarufu wa Baba Yake, ni kipindi ambacho alikuwa Shule, na baadhi ya Watu kuanza kumzungumzia Baba yake kila walipokuwa wakikutana naye.

LAKINI tofauti na kujaribu kujihusisha na Muziki, SEPTEMBA 9, Mtoto huyu wa NOTORIOUS anatarajia kuonekana katika Filamu Mpya THE KICKS ikiwa ni Filamu yake Nyingine na akizidi kukua haswa katika Soko la Filamu.

TIZAMA TRAILER YA MOVIE YA KICKS

MPIGA DEBE- BIRTHDAY

2:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
Binafsi Niliwahi kuwaza Sana, Nikagundua kumbe anhaaaaa... Kuna Birthday Party za aina Toifauti, lakini Aina Hii, inabidi niwafikishie Wapiga Debe wa HIT ZONE kupitia MPIGA DEBE ya 93.7 JEMBE FM

Sikiliza Hapa

#DakaHiiFasta: TIZAMA PICHA 6, UJIONE JINSI "KITUMBO" CHA ZARI KILIVYOJICHOMOZA TAYARI

2:46:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.
HAYA sasa, Diamond Platnumz Mwenyewe Kaomba Mumchagulie Jina la Mtoto Ajaye, maana Ujauzito Wa Zari Ndi Huoooooo, Ushaanza Kuchomoza.

Kama alivyofanya Mwaka Jana wakati Zari, ana Ujauzito wa Mtoto Tiffah, Chibu Dangote ameomba Mumtafutie Tena Jina la Mtoto Ajaye.

Tizama Kitumbo Cha Zari:









MPIGA DEBE- SELFIE

2:16:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.
HIVI kweli kuna Mtu anayechuklia Selfie?, au Kuna Mtu ambaye hatamani kufyatua Selfie Japo Moja?, au Kuna Mtu ambaye anachukia sana Kitu kinachoitwa Selfie?.

Kupitia "Mpiga Debe: ya HIT ZONE  kuptia 93.7-Jembe Fm Mwanza, Mambo yako Hivi Kuhusu Selfie. SIKILIZA


#DakaHiiFasta: ANACHOKISEMA NIKKI WA II KUHUSU RECORD LABEL ZINAZOANZISHWA NA WASANII NCHINI TANZANIA

2:06:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
HIVI sasa Tunafahamu Fika Kuwa, Pengine "Label" za Muziki Zimekuwa Ni Deal, na Ndio maana zinachangamkiwa sana na Wasanii Kadha Wa Kadha, ama Huenda kakawa Ndio ka Njia ka kuzuga kuwa na wewe Una Label.

Lakini Hii Imefumuka Ghafla na kwa Mfuatano Mkubwa, ambapo ukifanya Uchunguzi wako, utabaini kuwa, Wasanii zaidi ya 20 Tanzania Nzima, wana Record Label Zao Binafsi (Wakiwa wametangaza au hawajajitangaza), na wanawasimamia wasanii kadha wa kadha.


Lakini Hii Inaweza kuwa na Faida kwa wasanii Wachanga hasa katika Soko la Muziki , au Ikawa ni Hasara Kubwa Sana Katika Soko la Muziki, hasa pale Tunapobaini kuwa wasanii waliohitajika katika Label Fulani, hawawezi kupewa yale mahitaji yanayohitajika.

NIKI WA PILI, Msanii wa Muziki wa HIP HOP Nchini tanzania, na Mwanafamilia wa WEUSI, ana hili la Kusema Kupitia Kipindi #Imekaaje Ya HIT ZONE kupitia 93.7 Jembe FM-Mwanza:

#DakaHiiFasta: ALICHOKIJIBU NUH MZIWANDA, BAADA YA JAMAA KUJITOKEZA NA KUDAI KUWA NAWAL, AMBAYE NI MPENZI MPYA WA NUH MZIWANDA, ALIKUWA DEMU WAKE

1:54:00 AM Add Comment
Nuh Mziwanda na Mpenzi Wake Wa Hivi sasa-Nawal, anayedaiwa kumkimbia Valle Welle
Na Baba Juti
Siku Si Nyingi Sana, Kulizagaa Taarifa japo hazikupewa Uzito sana, Kuwa Kuna Msanii Chipukizi katika Muziki wa Kizazi Kipya, anayefahamika kwa Jina la VALE WELLE, amedai kuwa, Mpenzi Mpya Wa Nuhu Mziwanda, alikuwa "Mpenzi" wake ingawa hakufahamu ni Kwa Nini aliamua Kumuacha na kumfuata Nuh Mziwanda ambaye ni Hit maker wa Jike Shupa (Inayofanya Poa Katika JEMBEKA 20 za Jembe Fm-93.7Mwanza).
Valle Welle
Vale Wele ambaye ameamua kuandika Mkwaju wa "TEA" ikiwa ni Maalum kwa Umma kufahamu kuwa hiyo nji Story ya Kweli na Inamlenga Mchumba wa Nuh Mziwanda, ameongeza Kuwa, kitu ambacho anahisi Kilimfanya , ndicho ambacho amekizungumzia katika Mzigo huo, na aliumia sana

MSIKILIZE HAPA:

NUH ANASEMAJE.
Katika Kujibu Tuhuma Hizo, Nuh Mziwanda anasema kuwa, ni Kweli amesikia Tuhuma Hizo, na Vale Welle analenga Kutafuta "Kiki", sababu hakuona sababu ya Yeye kujitokeza katika Kipindi Hiki.
Nawal
Pia Nuhu hakuishia Hapo, ameongeza kuwa, Jamaa alkilazimishwa sana Picha Zake ziwekwe katika Gazeti la Udaku.

MSIKILIZE HAPA:

KUTANA NA MAGARI "LUXURY"-MAKALI HATARI

7:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SHOW OFF ya Magari Yenye Gharama Zaidi Ulimwenguni, imekuwa na Mvuto Hatari Jijini Londoni, ambapo Magari Mengi sana "Luxury" yaliweza kuoneshwa na wamiliki wa Magari hayo.

Tukio Hilo lililofanyika Maeneo ya MAYFAIR, lilihusisha magari makali kama Vile Chrome Mercedes-Benz, SLR McLaren na silver Lamborghini Aventador

Magari Mengine pia kama ROLLS-ROYCE, kutoka KUWAIT na SAUDI ARABIA yalikuwa Kivutio kwa Watu waliofika kuyashuhudia





















CHAMELEON: MIMI NA DIAMOND NI MARAFIKI, MEDIA NDIZO ZILITENGENEZA BIFU LETU.

2:51:00 AM Add Comment

BAADA ya Chameleone Kuandika Ujumbe Mzito kuhusu Bifu lake na Diamond, Manyangumi tumemnasa Chameleone akizungumzia Kinaga Ubaga hasa kuhusu Chanzo cha Yeye kutajwa kuwa na Bifu na Chibu Dangote.

Akizungumza kwa "Konfidensi", Hitmaker huyo wa TUBONGE amedai kuwa, Kiukweli kabisa, yeye na Diamond ni Marafiki na huwa anamchukulia kama Mdogo Wake, hata wakikutana katika Maeneo tofauti, husalimiana na hata kupiga Story.

Lakini Kitu ambacho kilikuja kutengeneza Story za Bifu ndani yao, ni MEDIA ambazo zimekuwa zikifanya kitu Kibaya sana, yaani kuchuanisha nani mkali kati ya Chameleone na Diamond.

Pia Chameleon ameongeza kuwa, Diamond ni Msanii ambaye amepata mafanikio haraka sana, na ana jina kubwa katika Himaya yake ambayo ni TANZANIA, ili hali Chameleone ana himaya Yake pia ambayo ni UGANDA.

MNADA BANNER