REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KENYA: 9 WAUAWA MJINI GARRISA KENYA

8:24:00 AM

Idadi ya watu walioaga dunia kwenye shambulizi alhamisi usiku mjini Garissa imefikia 9, baada ya wengine watatu kufariki wakikimbizwa hospitalini.

Hii ni baada ya watu wasiojulikana kuvamia hoteli moja mjini humo wakiwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK-47 na kuwamiminia risasi wateja waliokuwa ndani ya hoteli hiyo kwa jina 'Kwa Chege'. Mkuu wa polisi mkoa wa kaskazini mashariki Charlton Muriithi amesema kuwa kufikia sasa hawajabaini lengo la mauaji hayo ambayo yamesababisha taharuki kutanda mjini Garissa.

 Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu mwanafunzi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa baada ya watu waliojihami kutekeleza uvamizi katika kioski kimoja mjini humo.
Vile vile, mwanzoni mwa mwezi Aprili, maafisa wawili wa polisi waliuawa na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Al Shabaab.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER