REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KUPOTEA KWA SAA YA BINTI YAKE: TIMBERLAND NIMUONGO

5:21:00 AM Add Comment
JAPO KWA UFUPI.
MKALI Carry out,Timberland,ameitwa Muongo Mkubwa na Kampuni Moja ya Insurance nchini Marekani ikiwa ni katika Ishu ya kupotea kwa saa ya mkononi ya Binti yake.

Kwa mujibu wa malalamiko ya Kampuni hiyo ya Insurance ambayo tayari imemfungulia Kesi rapa Huyo na Prodyuza,inayofahamika kwa jina la AMERICA HOME INSURANCE COMPANY, inasemekana kuwa kampuni hiyo imelalamika kuwa Timberland amekuwa akitoa maelezo yanayokinzana dhidi ya upotevu wa Saa hiyo ya Binti yake MwenyeUmri wa Miaka 2, iliyogharimu Dolari za Kimarekani Milioni 1.8 ambazo zinadaiwa kuwa na gharama za uwongo.

Kampuni hiyo imedai kuwa,Timberland aliinunua saa hiyo yenye madini tupu ya Diamonds,kwa kiasi cha Dolari za Kimarekani 900,000,na alitoa taarifa kuwa saa hiyo iliibiwa,na baada ya Miezi Minne alidai kuwa iliwekwa katika sehemu isiyofahamika

JOMBAAAAAKE TIMBERLAND!!!!!!

PICHA: DAVIDO NDANI YA SKENDO NZITO

9:20:00 AM Add Comment


IKO HIVI:

Mkali wa DAMI DURO toka pande za OBINA LAND, namaanisha Nigeria, DAVIDO yumo ndani ya Wakati Mgumu baada ya Picha zake alizopiga na Binti mmoja Kitandani kwake kusambaa kwa kasi ya Ajabu katika Mitandao Mbali mbali.

DAVIDO ANASEMAJE:
Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo ni rasmi, inasemekana kuwa Davido amezikana Picha hizo huku akisisitiza kuwa, Binti huyo ambaye hata yeye hamfahamu, aliingia katika Chumba chake cha kulala baada ya kuusahau mlango wake wazi, na hatimaye kufanikiwa kupiga Picha hizo pasipo yeye kujua.
JOMBAAAAAKE  HUYO DADA!!!!!

HE: MENEJA MASOKO WA STAR TIMES KORTIN

9:11:00 AM Add Comment



MENEJA Masoko wa Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes jijini dar es salaam David Kisaka (37) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shtaka la kujipatia vitu kwa njia ya udanganyifu.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mahakamani kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 5, mwaka huu eneo la Akiba, Wilaya ya Ilala.

Katuga alidai siku hiyo ya tukio katika eneo hilo mshtakiwa kwa njia ya udanganyifu alijipatia ving’amuzi 110 na Antena 30 za StarTimes vikiwa na thamani ya Sh8.4 milioni mali ya Jonathan Mkanaka.

Mshtakiwa alikana shtaka na hakimu Joyce Minde aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 22 mwaka huu itakapotajwa tena. Mshtakiwa yupo nje ya dhamana baada ya kupata wadhamini wawili wa kuamina ambao walisaini bondi ya Sh6 milioni.

SAFARI YA SOUTH AFRICA : DOGO JANJA...YAMEKUWA HAYA?

9:05:00 AM Add Comment




Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu, Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.

Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”

Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”

Mbaula amesema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”

KUMRADHI : NILIKWENDA KIJIJINI KWETU KUSABAHI

1:11:00 AM Add Comment
Ndugu Zangu Wadau....
Sikuweza kuwa online kwa Muda wa Majuma Matatu...nilikwenda kutembelea kijijini kwetu, ikiwa ni sehemu ya Projects zangu

KIMBEMBE NCHINI SYRIA : WANAFUNZI 15 WAUAWA

1:08:00 AM Add Comment

DAMASCUS, Syria.


Wanafunzi wasiopungua 15 wameuwawa kufuatia shambulizi la waasi dhidi ya chuo kikuu cha Damascus nchini Syria. 

Shirika la habari la serikali limesema wanafunzi hao walikufa wakati makombora yalipopiga mkahawa katika kitivo cha usanifu majengo kwenye chuo kikuu hicho. 

Chama cha kitaifa cha wanafunzi wa vyuo vikuu kimelaani vikali mauaji hayo kikiyataja kuwa "shambulizi la uoga la kigaidi." Wakati huo huo, Uturuki imekanusha ripoti kwamba imewarudisha nyumbani mamia ya wakimbizi wa Syria kufuatia mapigano kwenye kambi moja ya mpakani.

PICHA: MHE. MOHAMMED DEWJI ALIVYOTOA USHIRIKIANO KWA TAASISI ZA KIDINI MKOANI SINGIDA

12:58:00 AM Add Comment




HALI YA MANDELA: NELSON MANDELA ANAENDELEA NA MATIBABU

12:55:00 AM Add Comment



Madaktari wanasema Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea kupata matibabu baada ya kulazwa hospitalini kutokana na maradhi ya mapafu. 

Mshindi huyo wa zamani wa tuzo ya amani ya Nobel alipelekwa hospitalini muda mfupi kabla saa sita usiku siku ya Jumatano. Ofisi ya Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, imetoa taarifa ikisema kiongozi huyo aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi, mwenye umri wa miaka 94, anapata matibabu bora kabisa kadri inavyowezekana. 

Rais Zuma amewataka Waafrika Kusini wasiwe na wasiwasi na wamuombee Madiba. Serikali ya Afrika Kusini imelaumiwa kwa kutotoa taarifa za kina kuhusu hali ya afya ya Mandela.

MNADA BANNER