REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MANI FONGO : SIJAMSHAWISHI MKALI WENU AACHANE NA TIMAMU MEDIA

2:42:00 AM Add Comment


Na Shaibu Ali & SASA TV (Dar Es Salaam)
#WatuWaMungu tunaamini kuna watanzania wengi sana wamekuwa wakivutiwa mno na Vichekesho vya Mchekeshaji MKALI WENU ambaye wengi tulikuwa tunafahamu kabisa kuwa alikuwa chini ya Timamu Media.

lakini Hivi karibuni, kumekuwa na Taarifa kuwa Mkali Wenu aliamua kupiga Chini Makubaliano ambayo yalikuwa yameundwa na Timamu Media na yeye, na kuamua kuchukua Zake.

KISA HIKI HAPA
Lakini kwa Taarifa za Chini Chini ambazo pia tulizinyaka, ni kwamba , Mani Fongo ambaye ni msanii wa Muziki wa Singeli kutoka hapa hapa Nchini Tanzania, ndiye alikuwa chachu ya kumshawishi apige Chini Timamu Media, na kuchukua maisha Yake Mengine.

Katika Ufafanuzi wake, Manifongo alidai kuwa, Mkali wenu ni zaidi ya rafiki yake, kuna kipindi alilalamika kuwa, anajisikia Vibaya kuwaona wenzake (akina Manifongo) wakiwa na maisha Mazuri, wakiendesha Magari, ilihali yeye ni Msanii Mzuri na anakubalika na hana Kitu

KAPIGA HATUA !!!!: HATIMAYE AZEALEA BANKS KAFUNGUA RECORDS LABEL YAKE?

2:32:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWa Mungu kama mtakuwa ni wafuatiliaji wazuri wa Muziki wa Hip Hop Ulimwenguni kote basi mtakuwa mnafahamu Vizuri kuwa kuna Bibie ambaye ana majanga kupita maelezo aisee

Mamito huyu anaitwa AZEALEA BANKS ambaye ni Rapper wa Kike ambaye kimuziki amekuwa Chini sana kupita maelezo, yaani mpaka inaboa.

Lakini baada ya kukutana na anguko kubwa, alianza kutamani kubakisha jina lake katika akili za watu, hali iliyomtu akutane na majanga Mengi ikiwemo kupigwa, kujichubua na hata kuachia Picha za Utupu Hivi karibuni, kitu ambacho kiliwashtua wengi sana sana sana

Lakini kitu ambacho kimewashangaza wengi, ni baada ya Bibie Huyu kudai kuwa hivi, Hivi sasa amefungua Records Label yake na ilikuwa ni Ndoto yake ya Muda Mrefu sana

Records Label hiyo inafahamika kwa jina la CHAOS & GLORY RECORDS.

AISEE !!!! : AVRIL AMEKIRI KUWA AMESHAWAHI KUWA NA MAHUSIANO NA.............

2:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Katika Maisha ya kawaida, Mwanaume yoyote akipewa Gape la kukutana na Msanii AVRIL kutoka Nchini Kenya, basi lazima atapata kigugumizi hasa pale atakapoona lile tabasamu lake.

Lakini ukiachilia mbali hayo, wengi tunafahamu kuwa Hivi sasa Avril yuko Single ingawa hatuna uhakika kama she is Ready To Mingle.

Hivi Sasa Hit Maker Huyu wa CHOKOZA, anafanya Vizuri sana na Mkwaju wake wa BABBIEE akiwa amemshirikisha Msanii wa Reggae & Dance hall kutoka Uganda, A PASS.

Ukiachilia Mbali masuala yote Kiujumla, kama ulikuwa hujui, ndani ya hii wiki, Avril ameweka wazi kuwa katika Mahusiano yote ambayo amewahi kuwa nayo, amewahi kukunjuka na Kijana ambaye ana Umri Mdogo kuliko yeye.

Ingawa Hakumuweka wazi Mtu huyo, ila Bibie huyo hakuona aibu wala haya kukiri mbele ya wanaafrika mashariki kuwa tayari ameshawahi kufanya hivyo na ni sehemu ya historia ya maisha yake.

BAADA YA KUDHALILISHWA !!: BOBY VALENTINO KAAMUA KUFANYA HILI WATU WA MUNGU

1:36:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.   
#WatuWaMungu Hatimaye Bobby Valentino ameamua kuamka na kufungua Makucha yake baada ya Wiki Kadhaa zilizopita kudhalilika vibaya  sana kupitia Mitandao ya Kijamii

Hatimaye Msanii Bobby Valentino na Yule Mwanamke aliyejibadili Jinsia kutoka uanaume (Transgender) anayefahamika kwa jina la Reima Houston, wanatarajia kuvaana uso kwa uso Kizimbani, ikiwa ni baada ya Reima kumrekodi Boby Valentino na kumpost Mitandaoni

Kama hukufahamu, ni kwamba, Reima ambaye ndiye Mwanamke, alichukizwa na Kitendo cha Boby Valentino, cha kugoma kumlipa Hela yake baada ya kumpa huduma ya Ngono, kitendo ambacho kilimlazimu amrekodi Mkali huyo wa TELL ME akikimbia Peku peku kutoka katika Chumba alichokuwa akipewa Huduma

Bobby V ndiye aleyefungua Mashtaka na kutoa taarifa ya kutaka Reima akamatwe kwa kosa la kumdhalilisha kwa sababu ya USD 2000, na alifungua mashtaka hayo kupitia Mwanasheria wake GERALD GRIGGS

Hata Hivyo, Reima alikuwa akitoa taarifa kupitia Interview Kadha wa kadha kuwa Alifanya hivyo kwa sababu alidhurumiwa

Madai makubwa ya Bobby ni kwamba mwanamke yule ni Kahaba, hivyo alitumia kila njia, ili amlipe USD 2000, kitu ambacho hakustahili kukipata, bali ilikuwa ni kumtishia.

MUNGU LINDA WATOTO WETU ; DEREVA WA GARI LA SHULE AKUTWA AMELEWA HUKU AKIENDESHA GARI LA WANAFUNZI 31

1:22:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WAZAZI sanjari na Walezi, naamini tunatakiwa kuwa na tahadhari kubwa sana hasa linapokuja suala la Watoto Wetu ambao wanachukuliwa na kurudishwa Nyumbani kwa Gari la Shule

Na Hii Pia sio kwa Wazazi na Walezi tu, bali hata kwa Walimu na Wamiliki wa Shule ambazo hutoa huduma ya Usafiri kwa Wanafunzi wao.

Dereva Mmoja Nchini Marekani katika Jiji la Georgia, ameangukia katika Mikono Ya Sheria baada ya kubainika kuwa anaendesha Gari ambalo limebeba Wanafunzi 31, huku akiwa yuko "Mtungi" kichwani mwake

Kwa Mujibu wa Taarifa Rasmi kutoka Jeshi la Polisi huko Huko GEORGIA, Bi Carole Eutheridge, amefikishwa mahakamani Jumatatu ya Wiki hii baada ya kubainika katika Hatia

Katika Gari hilo la Wanafunzi, Carole alikutwa akiwa ameficha Chupa kubwa ya TEQUILA, chupa Ndogo za Vodka pamoja na Chupa Ndogo Nyingine za Vidonge ambavyo havijaainishwa Mpaka Hivi sasa

Wanafunzi ndio waliofichua Uovu huo baada ya kutoa Taarifa kwa Wazazi wao kuwa Dereva wa Gari la Shule yao, huwa ni mtu ambaye anapiga "Makali" kwanza, kisha anawaendesha.

Hata Hivyo, mmoja wa Waajiri wa Zamani wa Dereva huyo, alidai kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya Bi. Carole, na wao walimtimua Kazi January Mwaka Huu


MNADA BANNER