REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MONICA: NIMEFANYIWA UPASUAJI KWA MASAA NANE

11:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Mnakumbuka Ule Mkwaju wa THE BOY IS MINE?, na wahusika ni watu wawili, ambao ni Brandy Nolwood na Monica

Sasa Monica ambaye kama amekuwa Kimya kwa Muda kadhaa hivi, amedhihirisha Kufanyiwa Upasuaji wa Masaa 8 baada ya kupata Tatizo linalofahamika kwa jina la endometriosis, kitu ambacho hakuwa anafahamu kama kinamsumbua

Kupitia Instagram account Yake, Monicah amedai kuwa Tatizo hilo amekuwa nalo kwa Muda Mrefu na alikuwa hafahamu kwa Miaka kadhaa mpaka ilipofikia hatua Hiyo
Naomba nimnukuu

“May 30 nimefanyiwa Upasuaji uliodumu kwa Masaa 8 ili kuondoa ENDOMETRIOSIS”

Endometriosis ni Tishu ambayo huvimba ndani ya UTERUS katika Kizazi, na kusababisha Maumivu makali. Dalili za Tatizo hili hupatikana hasa katika Mzunguko wa Hedhi na huweza kuleta Matatizo zaidi katika Hatua ya Kushika Ujauzito

MNADA BANNER