REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DIAMOND PLATNUMZ : NINATAMANI MGEFAHAMU KITAKACHOFUATA

5:17:00 AM Add Comment
Na Baba Juti  
WatuWaMungu Tunafahamu Vizuri kuwa Diamond Platnumz kutoka hapa hapa 255, ameachia Tracks kadhaa ambazo kama hazikuchukua nafasi ile ambayo tumekuwa tukiizoea, maana mjomba huyu akiachiaga mzigo lazima usumbue akili za Wasanii wenzake

Licha ya Kuwa Busy sana na Perfume yake "Chibu Perfume" Diamond Pia inaonekana ameamua kutoa "Gepu" kidogo kwa Wasanii ambao wako ndani ya LABEL yake "Wasafi" sambamba na kutambulisha mtandao wa WASAFI.COM

Sasa Siku ya Jana, Mondi alipost Picha yake akiwa na Meneja wake, BABU TALE, huku akiandika kuwa "I wish you know What Next"

Ingawa kuna lolote anaweza kulishusha, lakini wengi tunahisi huenda akaporomosha "Dude" ambalo linaweza kuwa ni Audio Track ama Video Track

We Unadhani ni nini


A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

TAYARI !!!!: MUIGIZAJI HALLE BERRY MWENYE MIAKA 50 HATIMAYE KAUNYAKA UJAUZITO MWINGINE

4:56:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
 #WatuWaMungu Hebu Tuwe Mashahidi katika Hili. Halle Berry ambaye ana Umri wa Miaka 50 kwa Hivi sasa, ana Ujauzito na yeye mwenyewe ndine aliweka Wazi kabisa

Alipokuwa katika Pozi la Picha Kwenye Red Carprt ya Party la  16th Annual Chrysalis Butterfly Ball  kule Beverly Hills, Bibie huyu alikianika Wazi Kitumbo chake na kuwataarifu watu kwa Njia hiyo kuwa ni Mjamzito

Halle Berry ambaye anasifika sana kwa kufunika kunako Movies atakazopewa ahusike nazo, tayari ana watoto wawili kutoka kwa wanaume wawili tofauti akiwemo mtoto wake wa kike Nahla Ariela Aubry  aliyempata na mwanamitindo  Gabriel Aubrey, pamoja na mtoto wa kiume  Robert Martinez  a;iyemzaa na muigizaji mwenzake Olivier Martinez.

    TIZAMA PICHA ZAKE   





WOOOZAAAAH !!!! ETI AMBER ROSE KAGAWA "UTAMU UTAMU" KWA MTOTO HUYU WA P.DIDDY

4:41:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
#WatuWaMungu AMBER ROSE anadaiwa kugawa tena utamu kwa Mtu ambaye hata tulikuwa hatumfikirii hata kidogo kwenye Huu ulimwengu aisee

Kwa Mujibu wa Taarifa kamili ambazo tumezipata japo ni kutoka Upande mmoja, ni kwamba Ex- Wife wa Wiz Khalifa aliamua kugawa "Uroda" kwa Mtoto wa Kuasili wa P.Diddy anayeitwa QUINCY (26)

Moja kati ya Shuhuda ambaye ndiye alimimina utamu huu, JASON LEE anadai kuwa, katika Birthday ya Quincy, Amber Rose (33) alionekana kuwa Karibu, na kisha kutoweka kusiko Julikana, hali ambayo inamfanya aamini kabisa kuwa Amber Rose ambaye ni Ex- wa Kanye West Pia, "ametinduliwa" na Mtoto huyo wa P Diddy
We unasemaje?


MAJANGA YA DONALD TRUMP: ARNOLD SCHWARZENEGGER AMTOLEA UVIVU TRUMP

4:28:00 AM Add Comment



Na Baba Juti  
#WatuWaMungu kumbe sio wamarekani weusi tu ambao wanamtolea Uvivu Rais wa Marekani, DONALD TRUMP, bali kuna hata wengine ambao hata hatukutarajia kusikia kama wanammaind sana Prezdaa huyu

Muigizaji Mkongwe ambaye pia amewahi kuwa Kiongozi katika Ngazi ya Ugavana, Arnold Schwarzenegger ameamua kumtolea Uvivu Donald Trump kwa kitendo chake cha kusitisha Makubaliano katika Hatua za mabadiliko ya hali ya Hewa na Nchi ya Ufaransa

Siku ya Alhamisi iliyokata, Rais huyo mwenye Vituko kila ukicha, alitangaza kupiga Chini Makubalino ambayo yaliundwa mwaka 2015 na mataifa zaidi ya 200 duniani katika kuhakikisha yanachukua hatua katika kupinga Matumizi ya Binadamu ambayo husababisha Hali ya Hewa kuwa Mbaya na kuwepo kwa mabadiliko ya Tabia ya Nchi


Sasa  Schwarzenegger ambaye hivi sasa ni Mwanasiasa Mzuri tu, ameamua kupingana na kitendo Cha Trump kutaka kupinga Kitu hicho ambacho kilikuwa na Faida kubwa katika Hali ya Nchi yoyte Ulimwenguni akidai kuwa, haiwezekani mtu mmoja avuruge mipango yenye Faida

Tunamnukuu
“ Mtu mmoja hawezi kuharibu na Kuvuruga Mipango yetu endelevu. Mtu Mmoja hawezi kuzuia Nguvu yetu safi ya Mabadiliko. Mtu mmoja hawezi kuturudisha Nyakati za Nyuma. Kulinda Mazingira yetu hakumaanishi kuharibu Uchumi wetu. “
INSERT: ARNOLD SCHWARZENEGGER

ETI NINI !!? : WAKATI SAKATA LA TALAKA LIKIENDELEA BAINA YAO, INASEMEKANA MKE WA T.I AMESHAUNASA UJAUZITO TAYARI

4:23:00 AM Add Comment



Na Baba Juti   
TUMEKUWA tukiimba sana hapa kuhusu taratibu za rapper T.I kutaka kutoa talaka kwa Mke wake Tinny, jambo ambalo limechukua asilimia kadhaa ya sababu za huku na kule kwa wawili hawa kuachana ama kupigana Chini.

Lakini katika hali ambayo sio ya kawaida, kumekuwa na fununu ambazo zinadai kuwa Mke huyu huyu wa T.I ambaye hivi majuzi majuzi tu alijifungua, hivi sasa pia ni Mjamzito


Kwa Mujibu wa wadakuzi ambao kawaida yao huwa wakiona kitu hawafichi kumimina Umbea wao, inasemekana weekend iliyokata, bibie huyu alionekana dhahiri kitumbo chake kikiwa na Mabadiliko, na mabadiliko yenyewe ni ya kubeba kiumbe ndani yake na wala sio Kushiba hata kidogo

Ingawa mpaka hivi sasa haijawekwa wazi na familia ama wahusika wa Familia ya T.I na Tinny, bado wengine wanazidi kusisitioza kuwa ni kweli bibie huyo anatarajia kushusha Kichanga pale muda utakapofika.

MNADA BANNER