REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANZA : KIWANDA CHA DWA ZA BINADAMU

6:25:00 AM Add Comment

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana.

Ndikilo amesema haiwezekani hata ajira kama za kukata majani badala yakuwapa wananchi wanaozunguka maeneo haya mkaenda kutafuta mtu kutoka mbali, kwani kwa kufanya hivyo mtawafanya wananchi hawa wasiwe rafiki wa kiwanda na wakati mwingine wanaweza kufanya uhujumu.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze  kukifungua kiwanda hicho mapema na  shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja.

 " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu  wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" 

Huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.



Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi 
wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho Prince Hetal Vithlani, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,


Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali  kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.

Prince Phamaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.

CREDIT: G-SENGO


MKUBWA HAMIDU-MUZIKI WA KIBIASHARA HAUTOSHUSHA NGOMA YANGU.

6:05:00 AM Add Comment

LEO ilikuwa Ni Guud day Kwa MKUBWA HAMIDU ambaye ameweza Kutambulisha Track yake kupitia Kituo Cha Redio Cha Metro Fm 99.4 Mhz –Mwanza, katika Kipindi cha Jam Session.

Track hiyo ambayo Inafahamika Kwa jina la NDOTO ZA MKEO, ina mahadhi Fulani hivi ya Kizazi kipya, huku Mkubwa hamidu akisimulia Stori ya Aina yake na Ya kibunifu kabisa, kwa Mtindo wa Rap.

Katika Interview ambayo ameifanya kunako kipindi hicho cha JAM SESSION ambacho huruka kila Jumatatu Mpaka ijumaa, kuanzia 7:00 Mchana mpaka 10:00, HAMIDU amesema kuwa Track yake iko tofauti na Nyimbo ambazo Zinafanya Vema Hivi sasa katika Soko la Muziki 

Nchi, lakini bado anaamini itafanya Vizuri sana na hata Kuliko hizo.

“Nyimbo yangu Ni kali, wala Sitishiki na Nyimbo za Kibiashara Kwa hivi sasa. Story yangu inakushawishi Utamani kusikiliza Verse ya pili mpaka ya tatu.”

Tofauti na hayo, Hamidu amesema kuwa kitu ambacho kinapatikana Kunako Track hiyo, kinazungumzia Athari za watu hasa katika jamii Yetu Kukurupuka katika Maamuzi.

“Ninashukuru sana Track yangu inaeleweka, na Inastory Nzuri. Mpaka hivi sasa, kunako mtandao wa Hulkshare, Ngoma hiyo imesikilizwa na watu zaidi ya 900, huku ikiwa Downloaded na watu zaidi ya 500. Hivyo ni hatua Nzuri Kwangu nab ado inazidi kunihamasisha kuwa itakuwa zaidi ya hapo.” Alisema Mkubwa Hamidu.


Katika kuongezea, Mkubwa Hamidu amesema Kuwa, Ngoma Hiyo imetengenezwa ROCK TOWN RECORDS iliyoko Mwanza, na Producer ni Yeye Mwenyewe

RAIS OBAMA ANAPOMSAIDIA MKE WAKE ASIDHARIRIKE

5:40:00 AM Add Comment

TUKIO Hili limetokea Huko HAUSTON ambako alikwenda kwa ajili ya Ziara ya Kikazi.






MO MUSIC AZUNGUMZIA MAHUSIANO YAKE NA MANAGEMENT YAKE BAADA YA KUFANIKIWA NA TRACK YA “BASI NENDA”

5:28:00 AM Add Comment

BAADA ya Video ya Basi Nenda Kuachiwa rasmi Wiki Kadhaa zilizopita, Ulianza Kuzuka Uvumi Kuwa MO MOSIC ambaye Ndo Mlengwa wa Track Hiyo, hayuko katika mahusiano mazuri na RECORD LABEL yake ya K- RECORDS iliyopo jijini Mwanza.

Moja kati ya Uvumi Huo, Ni Pamoja na kutokutoa Taarifa Kuwa anaenda Kufanya Video Jijini Dare s Salaam, jambo ambalo Eti liliwachukiza sana wasimamizi wake hao.

Akipiga Story na TTM, MO MUSIC amesema kuwa Uvumi huo sio wa Kweli hata Asilimia Sifuri, kwa Sababu yeye na K-Records wako Vizuri sana, na Wana mahusiano mazuri tokea tangu na Tangu.

Pia Moe Amezungumzia Uandishi wa Track yake hiyo, ambapo amesema Kuwa, mashahiri hayo matamu katika Track yake, ni ushirikiano Mzuri baina yake na Producer wake LOLLIPOP, ingawa Idea alikuwa nayo Muda Mrefu.


Leo Utapata nafasi ya Kusikia kile alichkisema Kunako ROCK CITY PROBLEM TOP 5 CHART, ambapo ameshika nafasi ya Kwanza Wiki Hii, Ikipanda kutoka nafasi ya Pili Wiki iliyopita

YMCMB WAMEKANUSHA KUMSAJILI RAPA SHOGA KATIKA CHAMA LAO.

3:17:00 AM Add Comment

KUMEKUWA NA UVUMI WA KUMIMINA KUWA KUNDI LINALOHESHIMIKA ULIMWENGUNI KOTE KATIKA MUZIKI WA HIP HOP DUNIANI, YOUNG MONEY CASH MONEY BROTHERS (YMCMB), LIMEMSAJILI RAPA MMOJA ANAYEJIHUSISHA NA USHOGA NCHINI HUMO.

Baada ya Uvumi huo Kuenea kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii, Finally mmoja kati ya Membaz wa kundi  la YMCMB, MACK MAINE, amejitokeza kupitia Mtandao wa Twitter na Kukanusha Kuwa habari hizo sio za Kweli nab ado hawawezi kufanya kitu cha aina hiyo.

Uvumi huo ulionekana kwa mara ya kwanza kunako mtandao wa 24 HOUR HIP HOP, KUWA Rapa Huyo Shoga anayefahamika kwa Jina la FLY YOUNG RED, amesaini Mkataba katika Team hiyo, na ataanza kupiga Kazi kama ambavyo Membaz wengine wanafanya.

Hata hivyo Jamaa huyo FLY YOUNG RED ambaye hivi sasa amechukua Tention ya watu kwa video yake ya THROW THAT BOY PUSSY , naye aliweza kuanika Vema kupitia Tweet yake ambayo Kitengo cha chimbua chimbua kiliweza kuinyaka,  kwamba hayuko YMCMB na wala hajalamba Mkataba katika Chama hilo kubwa.

Aidha katika interview yake na Mtandao wa Huffington Post, FLY alisema kuwa, sababu kubwa ambayo ilimfanya kutengeneza Track ya THROW THAT BOY PUSSY  ambao unamaudhui ya Kishoga, ni baada ya kutembele kwenye Club ambayo ni maalum kwa wapenzi wa jinsia Moja ya Kiume, na kubaini kuwa, walikuwa wakicheza sana nyimbo ambazo Waimbaji wa Kiume huwaimbia Wanawake.

Lakini Kiujumla anavutiwa sana na mapenzi ya Jinsia moja, na Ndiyo maana akaamua kuwatengenezea Wimbo Huo ili uwaburudishe katika Club zao.



Hata hivyo amesisitiza kuwa Wimbo huo hakuutengeneza Maalum kwa ajili ya Kupigwa Redioni, wala kuhamasisha Ushoga katika Nchi za Africa ama Kuwashawishi Vijana kujihusisha na Ushoga, bali ni kwamba amefanya hivyo kwa hulka yake na Faida ya Wapenzi wa Jinsia Moja.

RAY JAY BADO ANAWAUMIZA WATU…AZUA TAFLANI KUNAKO NIGHT CLUB MOJA..

3:08:00 AM Add Comment

KUNA UWEZEKANO RAY JAY akawa na Kitu adimu sana kwa Wanawake mbali mbali hasa ambao wanabiringika naye katika Kiwanja Cha Seremala.

This Time limezuka Timbwili kali baina ya akina dada wawili walioonekana wakimgombania Hit maker huyo wa I HIT IT FIRST, katika Night Club Moja Nchini marekani.

Kwa Maelezo ambayo TTM tumeyapata, ni kwamba wanawake hao ambao walianza Kukwaruzana kwa ajili yake, Ni pamoja na Muimbaji TEIRRA MARI pamoja na Girlfrienda Wa sasa wa Msanii huyo anayefahamika kwa Jina la PRINCES LOVE huku sababu ikiwa ni ya kukuacha ukistaajabu.

Aidha TTM iliweza kufuatilia Kwa kina Kuhusu chanzo cha Ugomvi huo ambao ulitokea katika Moja ya Night Club, na kubaini kuwa ni baada ya Mwanadada Teirra Mari ambaye alihit sana na Track ya Sponsor aliyomshirikisha Gucci mane na Soulja Boy, yuko karibu sana na Ray J.

Aidha Ripoti bado zinamiminika kuwa, Baada ya Princess kuona Hivyo, aliamua Kumfuata Tirra Mari na Kuanza kumhoji kwa sauti ya Juu kuwa, kwanini amesimama karibu na Mpenzi wake huyo ambaye Ni Ray J.

Pia Princess hakuwa na hilo tu, bali lilimuuma zaidi na huenda alihisi kuna jambo ambalo linaendelea baina ya Mpenzi wake na Teirra kwani alishawahi Kuona Picha za wawili ingawa haijawahi kuwekwa qwazi kama ni Picha tatatinishi, au ni Athari za Wivu wa Mahaba Niue.


Mpaka Ugomvi huo Unaisha, Teirra mari hakuonekana kujiskia vibaya, bali alitoa jibu Moja tu, kwamba Hajalishi, jambo ambalo lilimfanya Princess Love Kumrushia Ngumi.

MNADA BANNER