REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

ISABELLA : KAMA LUTEN KARAMA ANALALA NA MIE WIKI MBILI, HIYO NI NDO GANI?, NA HUYO MWANAMKE AJIANDAE KUPATA TALAKA MAANA AMESHAACHIKA MARA 3

7:36:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.
KIPINDI cha Nyuma, Wengi tulikua tunajua kabisa kuwa ISABELA , Member wa Scorpion Girls, na Luten Karama-Msanii wa Muziki wa Kiazi Kipya, walikuwa katika Mahusiano mazito, na kila mtu alikuwa anajionea mahaba yanayoendelea.

Lakini Baada ya Muda Kadhaa, zikavuma kuwa Wawili ao wamepigana Chini na mpango wao wa ndoa Umeyeyuka kabisa

Na Ili kudhihirisha Hilo, Luten karama aliamua kuvuta Jiko, yaani Kuoa, na Picha Zikawa Wazi katika Mitandao mbali mbali ya kijamii, huku Wengi wakimpongeza

Lakini Baada ya Isabella kuulizwa kuhusu uamuzi wa Luten Karama kuvuta Jiko, Bibie alijawa na "Sumu: kibao, huku akimkandia Luten Karama

Lakini Siku Kadhaa za Hivi karibuni, Wengi Tulipigwa na Butwaa kuona kuwa, Luten Karama na Bella wako pamoja tena Katika mahaba Mazito sana, ilihali kila mtu anajua kabisa kuwa Luten karama ana Ndoa kwa Hivi Sasa. Hii ilitokana na Video Clip aliyopost Isabella Mwenyewe katika account yake, akilia kuwa anampenda Luten Karama.

Kupitia Kipindi cha Hit Zone cha 93.7 MHz - JEMBE FM Mwanza, Isabella alisema kuwa, ni kweli kabisa kuhusu Video Hiyo wala hakuna Uwongo na yule ni Luten Karama. Na akaongeza kuwa, hakuna kitakachomtenganisha Luten Karama na Yeye maana wamekuwa pamoja kwa Takriban Miaka 6, na Licha ya Luten Karama kuwa katika Ndoa, bado anauwezo wa Kulala kwa Isabella hata Wiki Mbili na asirudi kwa Mke wake
MSIKILIZE HAPA

Lakini Tofauti na Hilo, Isabella alidai kuwa, Yule Mwanamke aliyeolewa na Luten Karama, alikuwa ni Rafiki yake (Shost), lakini alikuwa akizusha maneno ya Uongo kwa Luten Karama, na hata kuanza kumtongoza. Lakini kwa sababu Luten ameshafahamu kila kitu, ameamua kurejea kwa Isabella, na huyo bibie ajiandae kupokea Talaka any time
 MSIKILIZE HAPA

SHILOLE: KUZAA MAPEMA NAKO KUNA RAHA YAKE

2:21:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI
KAMA hujafahamu, watoto wawili wa Bad Gal Shishi, Muite Shilole, hivi sasa wamekuwa, na ni kitu ambacho yeyote angejivunia.

Kudhihirisha Hilo, Shilole ambaye huwa hana tabia ya kuwapost watoto wake katika Social Networks, hatimaye amejivunia jitihada na nguvu zake juu ya kuwalea mabinti zake wawili huku akimshukuru Mungu.

Kupitia Instagram account yake, Bibie huyu ambaye hivi sasa anasumbua na Track ya MTOTO MDOGO, amepost picha akiwa na mabinti zake hao wawili na kuelezea kuwa, kumbe kuzaa mapema nako kuna Raha yake

Nukuu
"Asante sana Mungu huwa siamin kama hawa ni watoto wangu... kuzaa mapema nako kuna raha yake "

MAINO: MAREKANI, MAGAIDI WANAISHI ILA WATU WEUSI TUNAUAWA

2:05:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI
RAPPER Maino bado hajachoka kuzungumzia namna ambavyo Wa-Marekani Weusi wanaonewa na Polisi Nchini Humo.

Safari Hii Hitmaker huyu wa ALL THE ABOVE  amedai kuwa, limekuwa ni jambo la ajabu sana hasa inapokuwa wazi kuwa, Polisi Nchini Humo, wanawaua Wamarekani Weusi hadharani, lakini magaidi wanazidi kutesa tu na kula raha.

Rapper huyo amefafanua kuwa, Gaidi anaweza kulipua Bomu ama kuhfanya ugaidi sehemu fulani, na watu wengi sana wakadhurika, lakini bado wataendelea kuishi na kutesa, lakini Watu weusi hata kama hawana hatia, huwa hakuna longolongo, bali ni kuwafyatua Risasi mpaka kuwaua, jambo ambalo anasema sio haki hata kidogo.



VIDEO: JUICY J- GREEN CARPET (EXPLICITY)

1:22:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI
Kwa Mara Nyingine Tena, Rapper JUICY J ameamua kuishusha kwako Video ya GREEN CARPET

Mwezi kama mmoja uliokata, aliachia Rasmia audio ya Green Carpet


VIDEOS: REMY MA AMECHEFUKWA..MNAOMSAKAMA KUHUSU YEYE JIBU LENU LIKO HAPA

1:03:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI.
KWA yeyote yule ambaye amemzingua na kumchukulia Poa REMY MA katika Mtandao wa Instagram, haki ya nani sijui, mtanyooka.

Kupitia account yake ya instagram na Snapchat, Remy Ma amedai kuwa, muda mwingi amekuwa akijitahidi kuacha maisha yake ya zamani ambayo yalijaa ubabe na hata ukali wa hali ya ju, na kuamua kuanza Prand New Life, yaani Remy Ma Mpya, lakini kuna baadhi ya Wajinga jinga wanataka kumkwaza na kumuingilia katika mishe zake

Hii inatokana na kauli zake katika Video Clip hiyo akidai kuwa, kuna baadhi ya Pages za instagram ambazo zinamchokonoa na hata kutaka kuingia katika mstari wake, sasa yeye hajali na anaweza kutindua wote watakaomzingua...

TIZAMA VIDEO.

BABA LEVO: UDIWANI KAZI KWELI KWELI.

12:29:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KAMA ulikuwa umemsahau baba Levo katika Tasnia ya Muziki, basi inabidi ufahamamu kabisa kuwa majukumu yamemuelemea, ukizingatia hivi sasa ni Diwani

Hitmaker Huyu wa YALLAH, amekuwa Kimya huku watu wakianza hata kumiss vile vituko vyake, pamoja na mikwaju yake ambayo kwa asilimia kadhaa itabeba utani kidogo.

Kupitia Instagram account yake, Baba Levo medai kuwa hivi sasa anawashughulikia wananchi wa Kata yake ambao walimchagua kupitia chama ca ACT WAZALENDO ,na Yuko tayari Kichwa Kipasuke

Naomba Kumnukuu:
Udiwani ni kazi kweli kweli ... Kichwa kinataka kupasuka.. Lakini kwa KIGOMA yangu ni bora KIPASUKE TU.. Ila nahitaji kuona wananchi wangu wanapata walichokitaka kwangu

WADAU: DULLY MSHIRIKISHE ALI KIBA.

12:26:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
UKIZUNGUMZIA mkwaju wa Inde kwa Hivi sasa, basi moja kwa moja unazungumzia Kuapatwa kwa Dully Sykes kwa Kishindo kizito baada ya kuwa kimya kwa Muda kadhaa

Lakini Tofauti na Kuwa Kimya kwa Muda Huo,  Pia Dully hakuwa akifanya Vizuri katika Baadi ya Tracks ambazo amekuwa akiziachi hapa kati kati kitu ambacho kilifanya ukimya wake uwepo katika Soko lake hasa Kimuziki.

Lakini baada ya Inde kufanya Poa, Prince Dully Sykes ameamua kuwahoji Mashabiki wake katika Maeneo mbali mbali kuwa hivi sasa, amshirikishe msanii gani katika Ujio wake.

Lakini kama hujafahamu wengi wanatamani amshirikishe msanii gani, basi Comments ambazo zilijirundika katika Post Hiyo, zilikuwa zikimtaja ALI KIBA, kama msanii atakayefuata katika kolabo ambayo anatakiwa kuifanya baada ya Harmonize

Ingawa wengi walipendekeza pia amshirikishe RAY VANY, alakini wengi wamempendekeza sana ALI KIBA.

"WAPENDWA BAADA YA HARMONIZE WIMBO UNAOFATA NIMSHIRIKISHE NANI? .....maoni yenu please!"


COMMENTS:
george_prince_King kiba1000000000000000000000000000000000 much respect for u

silvafreva buraza imba na t.i.d
rasta_diana Kiba
pauloernest898 Reyvanny
freezzykulaya alikiba
queennnell Kiba
agrey_ndonde Kiba au mziwanda au gnako au joh makin
kevy_mjunky King kiba...
stanzaofficial kwa Africa @diamondplatnumz | @wizkidayo au mimi bro @stanzaofficial
naima111.nnAlikiba nyimbo yako tamu sana kaka dully mwaaaa we nipe bila kipimo macho mpaka kisigino nikumwagilie wino yangu sio mbilikimo Hahaha yani hapo huwa nacheza huku nacheka ukitoa nyimbo na alykiba itanoga sana

MNADA BANNER