REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

DUH: MHESHIMIWA FILIKU NJOMBE ATAKA WAZIRI ACHAPWE BAKORA

6:27:00 AM Add Comment

Na Martin Malera
MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), ameliomba Bunge kubadilisha kanuni ili Waziri wa Kilimo na Chakula, Mhandisi Christopher Chiza, achapwe viboko bungeni akamuonyeshe mkewe.

Filikunjombe, alisema kanuni hiyo iruhusu mawaziri wote wanaoshindwa kujibu maswali ya wabunge kwa ufasaha, wachapwe viboko na kutolea mfano wa Waziri Chiza kwamba, alipaswa kuchapwa viboko kwa kushindwa kujibu swali la Mbunge wa Mwibara, Kange Ligola (CCM), juzi.

Akiomba mwongozo wa Spika jana bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Filikunjombe, alisema Waziri Chiza mwenye dhamana ya kilimo, jana alishindwa kujibu swali la Ligola na badala yake aliishia kutoa maneno ya kejeli kwa Mbunge huyo.

“Jana wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Waziri Chiza alishindwa kabisa kujibu swali la Ligola aliyetaka Serikali kutoa kauli juu ya mazao ya wakulima yaliyonunuliwa kwa mkopo na yale ambayo hajanunuliwa na yako kwenye hatari ya kuharibika wakati wa msimu wa mvua…

“Badala ya kujibu swali hili, Mheshimiwa Waziri aliishia kutoa maneno ya kejeli kwa Ligola kwamba yeye anayeshindwa kuelewa ndiye mzigo…
“Mwalimu Nyerere alisema wakati wa utawala wao hawakuwa na mswalia mtume kwa wala rushwa, maana hawakumuachia hakimu kuhukumu, kwani walikuwa wanawachapa viboko sita wakati wa kuingia na sita wakati wa kutoka wakawaonyeshe wake zao.

“Na sisi tusiwe na mswalia mtume kwa mawaziri wanaoshindwa kujibu maswali ya wabunge, tuwachape viboko bungeni wakawaonyeshe wake zao,” alisema Filikunjombe na kuibua vicheko kwa wabunge ukumbini hapo, akiwemo Chiza mwenyewe.

Katika swali lake la nyongeza juzi, Ligola alisema Waziri Chiza ni mzigo, kwani ameshindwa kuwasaidia wakulima wa mahindi, mpunga, pamba na mazao mengine ambao hawana uhakika wa soko na mazao yao yanaozea kwenye maghala.

Alisema katika jimbo lake la Mwibara, baadhi ya wakulima wa mahindi mazao yao yamekopwa na haijulikani watalipwa lini huku mazao mengine yakikosa soko.

Akijibu swali hilo kwa jazba, Chiza alisema yeye sio mzigo bali Mbunge huyo ndiye mzigo kutokana na uelewa wake mdogo.

Chiza alitajwa kuwa mmoja wa mawaziri mizigo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati wa ziara zake mikoani ambako alishuhudia kilio kikubwa cha wakulima huku wakilalamikia kwamba, hawajawahi kumwona Waziri Chiza kwenda kusikiliza na kujionea matatizo yao.


KUMBE HAMISA MOBETO BADO ANAKULA UJANA. HAFIKIRII KUOLEWA

6:09:00 AM Add Comment

Baab Kubwa Magazine:
“MGEUZA shingo za Wanaume” kila anapopita mbele yao, Hamisa Mobeto, huenda akawa amezima kabisa kila nia uliyokuwa mnayo hasa katika Kumvuta, na kushare naye Maisha, yaani Ndoa.

Sasa kupitia ndugu zetu Baabkubwa.com, tumepatamo ka-taarifa kuwa, the Sexy Baby huyu ambaye ni hatari sana unapomkabidhi Scene Kadhaa kwenye Video yake, hafikirii kabisa kitu kuolewa

Hapa Tunanukuu:
“Suala la kuolewa hapa kwangu hata silifikirii kabisa, mimi bado binti mdogo sana nitawezaje kukimbilia ndoa, hiyo ni mipango ya Mungu kila kitu kinaenda kwa wakati, muda utakapowadia nitaolewa,”

WACHA WEEEEEH !

RIHANNA ANATAFUTA MAZINGIRA YA KUFUNGIWA TENA INSTAGRAM?...CHUKUA HII

5:52:00 AM Add Comment

FRANK MAGNUS & RIHANNA INSTAGRAM
Ndani ya Wiki Hii, Rihanna amerudishiwa account yake ya Instagram @badgalriri, ikiwa ni baada ya kufungiwa kuanzia mnamo Mwezi May

Tatizo ambalo liliwafanya Instagram waifunge account hiyo ni pamoja na kupost Picha za Utupu/ Nusu Utupu ambazo alizipiga maalum kwa ajili ya Jarida Fulani hivi

SASA, Siku ya jana, Nimekutana na Picha moja hivi “Ya Kichokozi” ambayo akili yangu ilinituma kuhisi kuwa Rihanna anajaribu kuichokoza Instagram na utawala wake


Ukifuatilia kwa umakini, utabaini kuwa, Rihanna amepiga Piocha hiyo huku akionesha baadhi ya Maeneo “Chokovu” ingawa sio Kivile sana, lakini Mtu Mzima anaelewa

IMEBAINIKA ; KISERENGETI BOY CHA MAMA WA KIM KARDASHIAN KILIDANGANYA UMRI- ANA MIAKA 33 NA SIO 41

5:37:00 AM Add Comment


DAILY MAIL
TTM tumenyaka Full Mtonyo Kuwa, “Serengeti Boy” wa mama wa Kim Kardashian. KRIS JENNERS, umri wake ni Miaka 33, tofauti na awali ilivyokuwa imetajwa kuwa 41.

Kris Jenners, ambaye ana Umri wa Miaka 59, ameachana na aliyekuwa mumewe Bruce Jenners ambaye hata yeye pia alikuwa ana umri mdogo kwa mama huyu wa Kim kardashian.

Wawili hao wameonekana kutaka kuusukuma zaidi uhusiano wao wa Kimapenzi, ukizingatia kuwa familia ya Kris imeshamruhusu COREY GAMBLE kuishi na mama yao, katika Nyumba watakayoishi.


Ukifuatilia kwa Umakini, Corey anapigwa “Gap” la Umri wa Miaka 26 na Kris Jenners, na kama haitoshi, Kim Kardashian na Kourtney wanamzidi Umri Kijana huyo.












WEWE NDIO PACHA WANGU : MCHEKI KANYE WEST, KIM KARDASHIAN NA MTOTO WAO NORTH WEST WALIVYOPENDEZA

4:47:00 AM Add Comment










MNADA BANNER