REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WHAT THE FUNKY IS THIS?..EXCLUSIVE: HIVI NDIVYO RICK "rozay" ROSS ALIVYOOMBA MSAMAHA

8:04:00 AM Add Comment
UKIJIFANYA Mbishi Mbele ya Mashabiki zako na Wadhamini wako, yatakutokea puani kuliko kiburi ulichokuwa nacho. Hivi ndivyo Rick Ross The Baus alivyoomba Radhi ikiwa ni Siku moja tu baada ya kutemwa na Kampuni ya REEBOK kama mto ambaye ni ICON wao, na baada ya kuandamwa na Wapenzi wa Muziki kuhusu maneno aliyoyatamka, ya Ubakaji katika Track yake Mpya :


KAULI YA 1 :  "Before I am an artist, I am a father, a son, and a brother to some of the most cherished    women in the world. So for me to suggest in any way that harm and violation be brought to a woman is one of my biggest mistakes and regrets."

KAULI YA 2 : "My choice of words was not only offensive, it does not reflect my true heart. And for this, I apologize."


KAULI 2 ZA REEBOK KUHUSU KUVUNJA MKATABA NA RICK ROSS

6:16:00 AM Add Comment

HATUTAKIIII : MAKUNDI YA WANAWAKE katika Maandamanao Mbele ya Ofis za REEBOK


KAULI YA 1 : ‘While we do not believe that Rick Ross condones sexual assault, we are very disappointed he has yet to display an understanding of the seriousness of this issue or an appropriate level of remorse’, 

KAULI YA 2 : ‘At this time, it is in everyone’s best interest for Reebok to end its partnership with Mr Ross’,

BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA KAMPUNI YA REEBOK:










TAMKO LA ASAP ROCKY DHID YA RED LIPSTICK KWA WANAWAKE WEUSI : RAPA TRINA NA TOCCARA JONES WAMTOLEA UVIVU

5:44:00 AM Add Comment
HAHAHAA..Ile Kauli ya Mkali wa F*** Problems, Asap Rocky kuhusu kuwakandia Wanawake Weusi kupaka Red Lipstick Finaly imetolewa Uvivu na Rapper Trina Pamoja na Mwenzake Mwanamtindo Toccara Jones.

Kwa Mujibu wa TMZ leo, Mwanamitindo huyo Jones, alisema kuwa Asap anaichukia Red Lipstic kwa sababu anajichukia yeye mwenyewe pia, na aache mbwembwe zake

"Maoni yake na Maneno yake yanaonesha kuwa anajichukia yeye mwenyewe. Unaweza vipi kusema maneno hayo wakati we Mwenyewe ni Mweusi?", Alifunguka mwanamama huyo wa America's Next Top Model, Toccara Jones

Kwa upande wake Rapper wa Million Dollar, Trina, alikiri kuwa ASAP Hajui analolifanya na hata analolizungumza



MPEKUZI: MLELA KATIKA SKENDO NZITO...ICHEKI

4:39:00 AM Add Comment

STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja  kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.

 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.

“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo  anachosoma hakijui.

“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko,  kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.

SINGIDA: MWANAFUNZI HATIANI KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MINNE

4:27:00 AM Add Comment


Na Nathaniel Limu., SINGIDA
Jeshi  la polisi mkoa wa Singida linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Chief Senge mjini Singida Ibrahimu Saidi (17), kwa tuhuma ya kumwingilia kimwilia kinyume na maumbile  (kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne (jina tunalo).

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili 11 mwaka huu saa 11.30 jioni katika mtaa wa Majengo manispaa ya Singida.

Amesema mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa manispaa ya Singida, amepanga nyumba moja na wazazi wa mwaathirika/mlalamikaji.

Kamanda Kamwela amesema mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama alikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwa manafunzi huyo na hakukuwa na matatizo.

Amesema siku ya tukio, kama kawaida alipomwona mwanafunzi anaingia chumbani kwake, mtoto huyo naye alimfuata na kuingia chumbani humo.



Kamwela amesema mtoto huyo baada ya kuingia chumbani kwa mwanafunzi, mwanafunzi huyo alitumia fursa hiyo kumfanyia kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali.

 Amesema hivi sasa wanakamilisha uchunguzi ili waweze kumfikisha mahakamani mwanafunzi huyo ili kwenda kujibu shitaka linalomkabili.

Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo Agnes Paulo, amesema siku ya tukio akiwa amepumuzika na wapangaji wengine, alimwona mtoto wake akitokea chumba cha mwanafunzi huko akilia kwa uchungu mkubwa.

“Nilipomuuliza, aliniambia kuwa Ibarahimu amemfanyia kitendo kibaya huku akionyesha kwa kidole sehemu yake ya siri ya nyuma.Baada ya kumchunguza,niliona damu zikimtoka kwenye hiyo sehemu ya siri”,alisema kwa masikitiko.

MAHUSIANO: Zanzibar Na China Sasa Imara

1:20:00 AM Add Comment

ZANZIBAR,

Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China  Zanzibar Bibi Chen Qiiman akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China inatarajia kuikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Mwana kwerekwe C katika kipindi cha siku chache zijazo baada ya kukamilika ujenzi wake.

Ujenzi huo umekuja kufuatia ziara ya aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Hui Liangyu ambae ameshastaafu aliyoifanya Zanzibar na kutia saini Mkataba kati ya serikali yake na Zanzibar katika masuala ya Uchumi na Ufundi ukiwemo pia mradi huo wa ujenzi wa skuli ya Mwanakwerekwe C.

Mkataba huo uliotiwa saini umelenga kuipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  jumla ya RMB Milioni Sitini { 60,000,000 } sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ujenzi wa skuli hiyo pekee umegharimu jumla ya dola za kimarekani Milioni 1.6. 

Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bibi Chen Qiiman alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi hapo Katika Ofisi yake iliyopo katika Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


MNADA BANNER