REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HAPPY BIRTHDAY NAY WA MITEGO...HII NDIYO MIAKA YAKE...

11:34:00 PM Add Comment

Nay Wa Mitego anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo (June 9) na kufanya sherehe ya kwanza ya kusherehekea siku hii kwa kuwa hakuwa na utaratibu huo.

Nay amesema kuwa ameamua kufanya sherehe hiyo kwa kuwa mwaka huu kwake ni tofauti na miaka mingine kwa kuwa amepiga hatua kubwa sana katika maisha kupitia muziki wake hivyo ameamua ajipongeze kwa hafula fupi.

Mara nyingi kibongobongo watu huficha umri pale wanapofanya sherehe za siku ya kuzaliwa, utaambiwa tu ‘nimeongoza mwaka mmoja…nina miaka mingi…’, lakini hii ni tofauti kwa True Boy Nay wa Mitego ambaye ametaja umri wake bila kuficha kutokana na furaha aliyonayo.

“Leo natimiza miaka 29 labda niwaambieni. Kwa wale ambao walikuwa hawajui mimi sio mtu wa kuficha mimi ni niko live siku zote.” Amesema Nay.

“Leo natimiza mwaka wa 29 nashukuru, Mwenyezi Mungu amjalie miaka mingi mama yangu aendelee kuwepo aone mafanikio yangu. Na kingine, leo ni siku yangu ya furaha sana ntakuwa nasherehekea nikiwa home na washikaji zangu wawili watatu.” Ameongeza.

Nay ameendelea kuonesha utofauti kwa kuwa ameamua kujinunulia zawadi ya gari la kifahari (kibongobongo) ambalo linagharimu shilingi milioni 36.


“Nimejinunulia gari aina ya Murano nafikiri ndio gari yangu ambayo leo ntakuwa nayo na ndio birthday yangu. Inagharimu milioni 36, hii ni ya mwaka 2007…bado mpya bado inadai. one love kwa mashabiki wangu.” Ameeleza Nay wa Mitego.

MNADA BANNER