REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

STOPA RHYMES : STYLE TATU ILIWAFANYA WASANII WABADILIKE NA KUANZA KUIFUATA TONGUE TWISTA NA KUPATA UJASIRI WA KUTUMIA LUGHA ZA KIGENI KATIKA NYIMBO ZAO

6:44:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
RAPPER kutoka Arusha na Hitmaker wa STYLE TATU, Stopa Rhymes Okoyi, kupitia Hit Zone, ameweka wazi kabisa kuwa katika Game kwa asilimia kubwa, kuna baadhi ya Wasanii ambao huangalia kuna kitu kimefanyika halafu na wao wafuate

Akiweka Wazi kuhusu Hilo, Mkali huyo ambaye aliua pia na Zigo la Boom Bye Bye, amesema kuwa, Kipindi ambacho yeye anaachia Style 3, Wasanii Wengi walianza kupata Ujasiri wa kufuata Mfumo na kutumia Tongue Twista na hata kutumia Lugha za kigeni kama Vile Kiingereza
Tofauti na Hilo, Stoppa anaamini kuwa, Support ya Mashabiki katika Kipindi hiki Imekuwa Ngumu, maana wanasupport kwa kucomment tu, kulike, na mengineyo, lakini katika kununua bidhaa zao, imekuwa Ngumu

MAADHIMISHO YA SIKU YA MABOGA: IZZO BUSINES ANADAI KUWA UBACHELOR ANAOISHI DAR, UMEMFANYA ASHINDWE KULA MABOGA MPAKA ATAKAPORUDI KWA MAMA YAKE (AUDIO)

6:39:00 AM Add Comment

Na Baba Juti & Cathberth Mazigo
KAMA wewe unapenda kula kula kama wengine ambao tulishajaliwa kula vyakula vya aina tofauti tofauti sana, basi utakubaliana na mie kabisa kuwa, Kuna Chakula ambacho ni Jamii ya Tunda kinachoitwa BOGA

Boga haizalishi Tunda tu, bali hata majani yake huwa ni Mboga Nzuri, na unaweza kuiita Msusa, au kuyapika Kama Mrenda kwa jamii mbali mbali kama vile wasukuma, Wanyamwezi na wengineo
Lakini Kama Haitoshi , unaweza kufurahia Juice ya Maboga, na Hata Ile Mbegu yake, hutumika kama kitoweo pia, na hunoga sana ikiwa na Viazi Vitamu

LEO, OCTOBER 26, Ni Siku Maalum ya Maboga, na huazimishwa Sehemu Mbali mbali Hapa Duniani, lakini Pia Huazimishwa kwa Njia Tofauti.

Baadhi ya Mataifa Husherekea na kutumia Maboga kama kihisishi cha Siku ya HALLOWEEN, Lakini kuna Badhi ya Mataifa hupinga Vikali matumizi hayo ya Maboga katika Siku Hiyo

Mataifa hayo huamini kabisa kuwa, Heshima ya Boga Ni Chakula Maalum na siku ya Maboga ni Siku ya kufaidi kitu Kizuri na Rahisi zaidi kupika ama kuandaa.

Tofauti na hayo, Boga kwa Kiingereza huitwa PUMPKIN , jina liliotokana na Lugha ya Kigiriki ambao huliita PEPON wakimaanisha TIKITI MAJI KUBWA

Ukiachana na Hilo, Ufaransa huliita Boga kama POMPON, Kisha Uingereza wakaliita PUMPION, lakini Wamarekani Wakaliita PUMPKIN na ndivyo linafahamika hivyo Tayari.

Izzo Business , Msanii wa Kizazi Kipya Hapa Nchini Tanzania, anasema kabisa kuwa Ni Kitu ambacho Huwa anakipenda, ila kutokana na Maisha ya Kibachelor ambayo anaishi Dar, hajala Boga Muda Mrefu wala Mboga ya Msusa, lakini akienda Mbeya kwa Mama yake, lazima alikule
Lakini Pia, anakiri kuwa anapenda sana hicho kitu na anajivunia kulipenda


NISHER: ANAAMINI KUWASIKILIZA WATU, NI NJIA YA KUPIGA HATUA

6:31:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
DIRECTOR Nisher Kutoka Hapa Hapa Nchini Tanzania, amepotea kidogo katika Industry ya Production, but Guys, mujamaa yuko na mashine Very Classic na Expensive Bya Hatari !!!

Kitu ambacho Director huyu aliyewahi kusumbua kabla hata ya akina Hascana kutake Over, ni kwamba kuwaheshim na kuwasikiliza Watu sometimes, inakusaidia kuzingatia na kufanya kazi yako kwa Ufanisi...


Akizungumza hayo kupitia Channel yake ya Youtube, Nisher ambaye hivi sasa ameachia Series yake ya ALEX, amesema kuwa, kwa asilimia kubwa huwa anapitia Comments za Wadau wake na kuchambua vizuri, ili kuweza kupata japo kitu cha msingi katika Kazi yake
Tofauti na Hayo, Nisher amesema hajaacha kufanya Video za Muziki kama ilivyokuwa awali, bali hivi sasa anafanya kwa Malengo, tofauti na zamani alvyokuwa akifanya kwa sababu ya kutafta jina, na alikuwa akifanya hata kama ni Kulipua
Kwa Upande Mwingine, Nisher amesema kuwa, anapenda kuwasuprise zaidi, hivyo hatoshea vitu vingine, ila ni bora mkamfuatilia katika mitandao yake ya kijamii ili kujua what is Next.

KEKO: HATIMAYE AMERUDI KATIKA FLOW..KUPIGA SHOW NCHINI KENYA

6:26:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
ANGALAU sasa wale ambao tulikuwa tuna hamu na Flows na Matamshi Matamu kutoka kwa Ugandan Female Rapper - KEKO, tunaweza anaza kupata matumaini ya Ujio Wake

Baada ya Kuhusishwa na matumizi ya dawa Za Kulevya, ikiwemo pia kufulia kimuziki, na hata kuminywa sana na management yake na hata kutamka kuwa sasa anabwaga manyanga katika Music Industry, hatimaye Keko hivi sasa ana matumaini ya kurudisha heshima yake katika Stage.

Hit Maker huyo wa  HOW WE DO IT, anatarajia kupiga Show  katika Jukwaa litakalofungwa katika Makao Makuu ya KENYA, Nairobi, katika Show ya QUEENS OF THE MIC itakayokunjwa  November Mwaka huu

Keko ambaye kwa asilimia kubwa ana hamu ya kurejesha heshima yake katika Muziki wa Africa Mashariki , aliwahi kupitia majanga kadha wa kadha ya kukatishwa tamaa, baada ya kufutwa katika Mfululizo wa COKE STUDIO kwa Mwaka Jana, na hata kutimuliwa katika Moja ya Hotel Kubwa Nchini Kenya, kwa madai kuwa alilewa sana na kusababisha fujo.

ALL THE BEST KEKO.

ANGELINA JOLIE: AMESITISHA MASUALA YA MOVIE KULE HOLLYWOOD ILI KUWA KARIBU NA WATOTO WAKE,

6:23:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
MUIGIZAJI Angelina Jolie ameamua kuweka Kando suala zima la Kuporoduce Filamu aliyokuwa na hamu nayo sana, ili kuwa Karibu na Watoto wake

Uamuzi huo unatokana na Vuguvugu la Talaka na Mumewe wa Muda Mrefu, BRAD PITT, ikiwa ni baada ya kuwepo kwa Madai kuwa, Mumewe huyo amekuwa akiwanyanyasa watoto wao kutokana na matumizi ya Pombe pamoja na Madawa ya Kulevya.

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Hollywood ni kwamba Bibie huyo hivi sasa hajihusishi tena katika Kumalizia Filamu yake ya FIRST THEY KILLED MY FATHER ili kuhakikisha kuwa suala la malezi linaenda sawa kwa watoto wake


Tofauti na hilo, inasemekana kuwa, Watayarishaji wa Filamu hiyo wamekuwa wakijitahidi kumuhusisha Angelina Jolie kwa Njia ya SKYPE, lakini amekuwa hajibu Chochote.
Pia inawezekana kabisa Angelina Jolie akahamia LONDON.

Lakini Kwa Upande Mwingine, Mume Wake Brad Pitt anatarajia kutokea katika RED CARPERT ya Uzindz wa Filamu ya ALLIED itakayoachiwa Rasmi na kuingizwa Sokoni NOVEMBER hii.


TONI BRAXTON: NI MBISHI BALAA, AMEAMUA KUPIGA SHOW AKIWA NA KIFAA CHA HEART CONTROL

6:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
SIKU Kadhaa zilizokata, kama utakuwa unakumbuka Vizuri, tulikupa Info Kuwa, Mwanamama Toni Braxton, alikumba na tatizo baya la Kiafya hali ambayo ilimlazimu apelekwe Hospital Mara mbili kabla ya Show yake na hata kuahirishwa Mara Kadhaa.

Lakini Ili Kuonesha kuwa ni Mbishi Kupita Maelezo, Hit maker huyo wa Breath, aliamua kupanda jukwaani na kifaa maalum cha Kupima muelekeo wa Moyo Wake yaani HEART CONTROL.


Tatizo kubwa la LUPUS ambalo madhara yake huvamia kila sehemu ya mwili hasa Ngozi na sehemu ya Moyo, ndilo lilikuwa likimsumbua sana Bibie Huyu, lakini Hiyo bado haikumzuia yeye kufumua Show yake huko maeneo ya Savanna, lakini alionekana akiwa na kifaa hicho.

Kwa Mujibu wa Maagizo ya Madaktari wa Toni Braxton, bibie huyo anatakiwa  kuvaa kifaa hicho masaa 24 kwa Wiki, ili kubaini Maumivu ya Kifua, pamoja na Shambulio la Moyo au Stroke kama ikibidi.

JUSTIN TIMBERLAKE HUENDA AKAINGIA MATATANI BAADA YA KUPOST PICHA AKIPIGA KURA.

6:16:00 AM Add Comment
Na Baba Juti
SIJAFAHAMU kwa Nchi ya Tanzania kama ni Kinyume cha Sheria kupost Picha ukiwa unapiga Kura hasa ya kumchagua kiongozi wa Nchi au lah, lakini asilimia kubwa huonekana wakiwa Tayari wana wino katika Vidole vyao.

JUSTIN TIMBERLAKE huenda akautana na kifungo cha Siku 30 Jela pamoja na Fain ya Mkwanja, baada ya kupost Picha akiwa anapiga Kura, katika Maeneo ya TENNESSEE huko Nchini Marekani


Kwa Mujibu Mawanasheria wa Jimbo la SHEBY huko huko Tenessee, inasemekana kuwa Hitmaker huyo wa Cant Stop The Feeling hivi sasa yupo katika mahojiano na ukaguzi mkubwa hasa kubaini kwanini alikiuka Sheria za Nchi Hiyo, kupiga Picha ukiwa unapiga Kura, na kupost katika Mitandao ya Kijamii

katika Sheria ambayo iliboreshwa na kuhimizwa kufutawa zaidi kuanzia mwaka Jana, Ni Marufuku kwa Mtu yeyote kupiga picha au kurekodi mazungumzo ya aina yoyote yanayotokea katika Eneo la Kupiga Kura. na Endapo itabainika kuwa, umevunja Sheria hiyo, basi unakula Nyundo ya Siku 30 Jela, pamoja na Faini ya USD 50


ANNE KANSIIME : KUWANIA TUZO ZA UK AWARDS - BAWR

5:31:00 AM Add Comment


Na Baba Juti
HAKIKA kila mtu hivi sasa anamfahamu vizuri Binti mchekeshaji kutoka Nchini Uganda, ANNE KANSIIME !!!

YEs, The Good News ni kwamba Bibie huyu ambaye amejichukulia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki, amechaguliwa kuwania Tuzo za Kimataifa za UK BLACK AFRICAN WOMAN ROCK (BAWR) ambazo zinatarajia kufanyika Uingereza , DECEMBER 03 2016

Tuzo hizo ambazo zilianzishwa na LINDANI MOYO mwaka 2013, ziko maalum kwa ajili ya kuwapa Moyo wanawake wa Kiafrica, kuelimisha, na hata kuhamasisha wanawake ambao wana mizizi ya Kiafrika katika harakati zao

Kansime amekuwa ni Msanii wa Vituko wa Kike Pekee kutoka Afrika mashariki, asiyeogopa kuthubutu na hata kupambana mpaka kupata Deals Nyingi sana

MNADA BANNER