REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JAMANI WATANZANIA...HAKUNA KINGINE MLICHOKIONA KWA MAMA YAKE DIAMOND TOFAUTI NA HILI?..MSIMFANYIE HIVYO !!!

5:06:00 AM Add Comment
 Na Ibra-The Insta-Cop  
#WatuWaMungu Nyie mnataka nini lakini?...maana kila kinachokuja kwenu huwa hakikosi kasoro.... mmepewa Macho ya aina gani lakini

Haya, Wakati napita huku na kule kwenye Instagram account za Watu mbali mbali, nikakutana na Instagram account ya Mama Mzazi wa Diamond Platnumz-KENDRA MICHAEL

Nikakagua kagua weeeeee, nikavutiwa na kile ambacho amepost kuhusu yeye na Mwanaye Diamond Platnumz, hasa ukizingatia huu ni Mwezi wa Toba (Ramadan), pamoja na picha mbali mbali za wajukuu wake, yaani kiukweli anawapenda sana inavyoonekana

Lakini nikaona kitu kama Simu Hivi, nikasema basi ngoja niangalie Kile alichopost Bi Mkubwa Wetu...Well, ni Simu nzuri, kali, SAMSUNG EDGE...safi sana kiteknolojia...

Ila Watanzania sasa walivyo "Wakuda" hawakujali simu, ishu nzima ikahamia kwenye Vidole Vyake...
Mbona viko poa Tu jamani?...au Nyie mnasemaje?

JAMANI !!! : AFARIKI KWA KUOGELEA NA TATTOO MPYA

4:30:00 AM Add Comment


  Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Ni wangapi Mnapenda Kuchora Tattoo Jamani?. Na Wangapi huwa mnatamani Siku moja mjekuwa na Tattoo?


Sasa, haijalish kama unataka Uichore Puani ,Mdomoni, ama Shingoni ni Wewe tu, lakini kuna hii Taarifa Hebu tuchangie wote na Tufahamu.

Mwanaume mmoja Mwenye Umri wa Miaka 31 huko TEXAS Marekani, amepoteza Maisha ama amefariki baada ya Kuoga akiwa na Tattoo Mpya

Kwa Mujibu wa Taarifa kamili kutoka kwa Daktari ambaye alikuwa akimuhudumia ,Jamaa huyo alikuwa amechora Tattoo, lakini baada ya Siku 5, Tattoo ikiwa bado ni Mbichi Mbichi hivi, alienda kuogelea Baharini na huko ndiko lilitokea la kutokea

Inasemekana Jamaa huyo alienda kuogelea huko GULF OF MEXICO, hali ambayo ilimfanya ashambuliwe na Backteria ambao walimsababishia Kifo Hicho.

Dr. Nicolaus Hendren ambaye ndiye alimhudumia, anadai kuwa jamaa alifika Hospitalini hapo akidai kuwa Mguu wake wa Kulia ambao ndo wenye Tattoo ulikuiwa ukimuuma, na Ndipo ilikuja kubainika kuwa katika Tattoo yake ambayo ilichorwa na kuandikwa “YESU NI MAISHA YANGU: ilikuwa Imeshambuliwa na Bacteria hao

Pia Daktari huyo anadai kuwa, hali hiyo ilisababisha Miguu yake yote kuuma na kisha kupatwa na Homa kali, huku upande wa Tattoo ukiwa umetafunwa tayari

LIL KIM: NDO KWISHA HABARI YAKE?

4:26:00 AM Add Comment




Na Baba Juti
#WatuWaMungu Tunafahamu Vizuri Heshima ya Rapper wa Kike LIL KIM hasa linapokuja suala zima la Hip Hop haswa kwa Wanawake

Lakini Najua mnalifahamu hili kuwa Lil Kim amekuwa akiishi maisha ambayo kila Mtu huwa anasema daah, bibie huyu hawezi Fulia hataSiku Moja
.
Sababu kubwa ni kwamba, amekuwa akivaa mavazi ya gharama sana, Kuendesha Ndinga za Gharama, na hata kuhang out na watu ambao wana maisha Fulani Heavy kidogo, lakini Kumbe hizo zote ni Mbwembwe za kutuzuga tukupitia Ma-social Networks

Hakim kutoka Mahakama ya NEW JERSEY ,Marekani, ameamuru Lil Kim kunyang’anywa Mjengo wake baada ya kushindwa kulipa Deni la Mkopo

Bank inayofahamika kwa jina la HSBC ilimfikisha Mahakamani Lil Kim mwaka 2010 kwa madai ya kusitisha Ulipaji wa Deni la Mkopo huo ambao ulikuwa ni Mkopo wa Nyumba

Pia Bank hiyo ikaongeza kuwa, Mwaka 2002, walikubaliana na Lil Kim kuwa wampe Mkopo wa Nyumba na atakuwa akilipa USD 10,000 kwa Mwezi kama mallipo ama marejesho ya Mkopo.

Ingawa mpaka Hivi sasa haijafahamika kama ni kwanini Lil Kim aliacha kulipa Mkwanja huo, mpaka hivi sasa, Lil  kim anatakiwa kulipa USD Milioni 2 kitu ambacho huenda ni kweli asifanikiwe kukilipa hata kidogo

MAKUBWA !!! : ETI WATOTO WA J-LO HAWAMPENDI BABA YAO WA KAMBO MPYA !

4:20:00 AM Add Comment



  Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Mahusiano ya Mwanamama Jeniffer Lopez a.k.a J-Lo na jamaa anayefahamika kwa jina la ALEXANDER RODRIGUEZ yamekuwa na Mwendokasi wa hali ya Juu, na inabidi tulipokee kama lilivyo.

Lakin ipia, wawil ihao ili kuwekama husiano yao yawe Imara zaidi, tayari wameshatambulishana kwa watoto  wao, maana ukizingatia kila mmoja alikuwa tayaria na watoto kabla hawajaanza mahaba yao ya Mwendokasi

Lakini Picha kali lipohapa, ambapo Taarifa zilizotufikia zinadai kuwa, Watoto wa JLo ni kama hawajamkubali ama kumpokea kwa moyo mweupe Baba yao wa kambo, ambaye ni “Mupenzi ya Mama Yao”

Inasemekana kuwa, watoto hao hawajaonesha “Amsha” yoyote mpaka Hivi sasa kwa Alexander Rodriguez kama ambavyo ilikuwa kwa Casper Smart, kitu ambacho kinamfanya hata J-Lo Mwenyewe ajiulize maswali Mengi

Mvujisha Umbea ambaye yuko karibu na J-Lo anadai kuwa Mapacha wake ambao wana Umri wa Miaka 9 Hivi sasa wanaonekana dhahiri kabisa kama  wanamuogopa Mzee Mwenzetu Alexander ingawa bado wanavuta Subira kuona kitakachoendelea

Tofauti na Hilo, Alexander anajitahidi sana kuwa karibu nao na hata kuwafahamu vizuri mapacha hao ambao J-Lo alizaana Marc Anthony lakini bado kama inakuwa Ngumu

Pia Hitmaker huyo wa “LOVE DON’T COST A THING” amedai kuwa hatakama watoto wake watamchukia au kutokumpenda Mupenzi wake mpya, haimzuii kuendelea kula maraha ya kimahaba naJamaa huyo, watazoea tu

MNADA BANNER