REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NICKI MINAJI AFUNGUKA KUHUSU OMBI LA DJ KHALEED

11:36:00 AM Add Comment

ZIMA NIKUPE MTONYO;

HATIMAYE Badaa ya kusubiriwa kwa Muda Mrefu sana kuhusiana na Ombi la Ndoa kutoka kwa Dj Khaleed, NICKI MINAJ amefunguka rasmi..Heheheiyaaaa...Kudaaaadeki !

Baada ya DJ KHALEED kuelezea Hisia zake juu ya Mtoto Mrembo Minaji kupitia Kituo cha MTV, kila mtu amekuwa yuko kimya sana kusikia ni kipi ambacho atakijibu Sweetie huyu, kama ni NDIYO, ama Kibuti

KAULI YA NICKI MINAJ
Lakini licha ya Nicki Minaji kutokuichukulia ishu hiyo Serious kihivyo, bado aliwaacha Mashabiki wa KHALEED na Yeye Mwenyewe Kinywa Wazi baada ya Kusema haya:

"Nilishtuka sana kama ambavyo Ulimwengu Mzima ulishtuka. Nilicheka pia kama ambavyo ulimwengu Mzima ulifanya hivyo, kwa sbabu Khaleed ni Mtu anayesimamia kila anachokifanya."

Bora hata ya Kauli hiyo, lakini ya kushangaza zaidi ni Hii aliyoisema mwanamama NICKY
" Ilikuwa ni Njia nyingine ya kipekee, kwa yeye kutoa sehemu ya Ujumbe ama maneno ambayo yatapatikana katika Wimbo wake Mpya"

TRACK HIYO PAMOJA NA ALBAM MPYA:
Hilo lilikuwa ni neno la kuitengenezea Njia Track yake pamoja na Albamu yake Mpya. Ngoma yake hiyo inaitwa "I WANNA BE WITH YOU" ambayo amemshirikisha Nicki Minaj, Future na Rick Ross. Albam yake itatambulika kwa Jina la SUFERRING FROM SUCCES

NICKI ALICHUKULIAJE TAMKO LA DJ KHALEED.

"Khaleed Ni Kaka angu, na hakuwa Serious wakati anatamka ombi hilo la Ndoa kwangu. Ifahamike hivyo Tafadhali. Alikwa anatania. Khaleed hajavutiwa na Mimi na wala hanihitaji Kimapenzi. Ni Mtu na Dada Yake" Alisema Nicki




LHRC - "TUTAMBURUZA PINDA MAHAKAMANI"

9:07:00 AM Add Comment

Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wiki hii kinatarajia kumburuza mahakamani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumtaka afute kauli yake aliyoitoa bungeni mwezi uliopita kwamba Polisi wawapige raia wanaoleta uchokozi na kuashiria uvunjifu wa amani hapa nchini.

Mwezi uliopita Pinda katika mkutano wa Bunge la bajeti mjini Dodoma alitoa kauli ya kulitaka jeshi la Polisi nchini kuwapiga raia wanaokaidi amri halali ya jeshi hilo wakati aikijibu maswali ya Papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia, alisema taratibu zote za kisheria za kumfikisha Pinda mahakamani zimekamilika na siku yoyote wiki hii watafungua kesi.

Sungusia alisema kauli ya Pinda, imevunja katiba ibara ya 13 na kwamba lazima sheria ichukue mkondo wake kwa mkumfikisha mbele ya mahakama.

Alifafanua kuwa ibara ya 100 inayompa kinga mbunge anapotoa jambo lolote bungeni inamweka kando Pinda, kwa kuwa yeye hakuzungumza bungeni kama mbunge bali alikuwa anatoa msimamo wa serikali yake.
 Alisema kauli ya Pinda ilikuwa kali na mbaya na kwamba, walimtaka Pinda aifute siku chache baada ya kuitoa, lakini mpaka sasa amekaidi na hivyo wameamua kuchukua hatua ya kumfikisha mahakamani ili haki iweze kutendeka.

Pinda alitoa kauli hiyo nzito alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyetaka kujua kauli ya serikali juu ya vyombo vya dola kudaiwa kuwapiga raia hususani katika mikoa ya Mtwara na Arusha.

Akijibu swali hilo Pinda alisema “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu.”

 Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu,"
“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga,” alisema Pinda.


T.A.T NIPASHE

ZIMA MOTO : OLE WENU MNAOTUCHEZEA.....

8:59:00 AM Add Comment


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, limesema liko mbioni kupata ‘mwarobaini’ kwa wananchi wanaotoa taarifa za udanganyifu na lugha za matusi kwa kupiga simu za uongo kwa jeshi hilo.

Jeshi hilo limesema katika kukabiliana na hali hiyo, litafunga mtambo wa kuwabaini wahusika hao.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Jenerali Saimon Mgomba, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akiwatunuku vyeo maofisa tisa wa jeshi hilo.

Alisema changamoto kubwa inayolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini ni kupokea taarifa za uongo kutoka kwa baadhi ya wananchi kuwa kuna tukio la moto.

Mgomba alisema jeshi hilo hupokea wastani wa taarifa za simu za uongo 20 kwa siku kwamba kuna matukio ya moto yametokea katika maeneo fulani.

Aliongeza kuwa mbali na kuwapo kwa miito ya uongo, pia hupokea lugha za matusi kutoka kwa baadhi ya wananchi. “Haya ni mateso makubwa tunayoyapata, nasema siku zao zinahesabika ndani ya wiki mbili hadi tatu tutafunga mtambo wa kuzijua namba hizo pamoja na majina yao,” alisema Mgomba.

Alisema zoezi hilo litaanzia Dar es Salaam na litakuwa endelevu katika mikoa mingine muda mfupi ujao.

Aidha, alisema malengo ya Jeshi la Zimamoto kwa sasa ni kufika katika eneo la tukio ndani ya dakika 15 lakini wanakwamishwa na tatizo la miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na foleni.


Pia alisema tatizo la visima vya kuchotea maji bado ni changamoto na kueleza kuwa hadi sasa wana visima vitano vinavyofanya kazi na zaidi ya 1,000 vibovu.

MNADA BANNER