REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

RICK ROSS IN DA BUILDING !!!!!.HAPA HAPA BONGO

8:03:00 AM Add Comment




MGUU PAAAAAAH......MPAKA CLOUDS TV, Si ndio nikakutana na BO...,BO...BO...BO...BONGE LA PROMOOOO!!!!
Eti kwamba....Wale wakali wa Matamasha U.R. of T. (United Republic Of Tanzania) namaanisha Area 255-Bongo...Clouds Entertainments Group, kupitia SERENGETI FIESTA 2012...BHAAAAAAAAAAAAAAAASSS...watamdondosha "Teflon Don, The Big Bous, Rozay" akifahamainka kama RICK ROSS hapa Bongo.

Unataka Kufahamu zaidi?...Stay In Touch..Hiyo nimekuibia Tu!!!!!!!

SUDAN KUSINI NA SUDANI KASKAZINI ZAFIKIA MAKUBALIANO

2:24:00 AM Add Comment

Sudan Kaskazini na Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya usalama wa mpaka na usafirishaji mafuta baada ya mazungumzo ya siku nne katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Rais Omar al Bashir wa Sudan na mwenzake Salva Kiir wa Sudan Kusini ambao wamekutana mara 6 tangu Jumapili iliyopita wanatarajiwa kutia saini makubaliano hayo leo Alhamisi. Makubaliano hayo yatafungua njia ya kuanza tena usafirishaji mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba ya Sudan.

 Hata hivyo nchi hizo mbili zimeshindwa kuafikiana juu ya masaula kadhaa yanayohusu mpaka. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Sudan El Obeid Morawah amesema masuala hayo yatajadiliwa katika siku zijazo.

Nchi hizo mbili zimekuwa zikishinikizwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumaliza hitilafu zao.

KENYA WAIPIGA AL-SHABAAB TENA

2:19:00 AM Add Comment
ASKARI WA JESHI LA KENYA AKIWA KAZINI

Kenya imesema kuwa jeshi lake la majini limeshambulia vituo vya waasi wa kundi la as Shabab katika bandari ya Kismayu huko kusini mwa Somalia, kabla ya kufanywa mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya waasi hao.


Msemaji wa jeshi la Kenya Cyrus Oguna amesema, kikosi cha majini cha Kenya kimefanya mashambulizi hayo baada ya vikosi vya anga kulenga ghala la silaha karibu na uwanja wa ndege wa Kismayu.

NEMBO YA KUNDI LA AL- SHABAAB

 Oguna ameongeza kwamba, shambulizi hizo linaonyesha jinsi jeshi la Kenya lilivyoshadidisha operesheni zake huko Kismayu na kwamba mashambulizi ya nchi kavu bado hayajaanza. 

Msemaji huo wa jeshi la Kenya amesema, askari wa nchi hiyo wanatarajiwa kuanza kuingia Kismayo wakati wowote mwafaka kuanzia sasa.

KUNDI LA AL- SHABAAB

 Vikosi vya jeshi la Kenya vikishirikiana na askari wa Burundi, Uganda na Djibouti kwa wiki kadhaa vimekuwa vikipambana na waasi wa as Shabab katika operesheni inayofanyika chini ya mwamvuli wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM. 

Askari hao wamefanikiwa kuwafurusha waasi hao kutoka katika ngome zao.


LAANA YA MWAKA.....HAWA AKINA DADA WANAMAANISHA NINI?...HEBU WAONE WANAYOYAFANYA!!!!!!!

2:06:00 AM Add Comment












Unaweza Ukadhani ni Masihala....lakini hivi ndivyo Swahiba wangu MPEKUZIO alivyowagundua Akina Dada Hawa.

Hii Ni Laana !!!!

MNADA BANNER