REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WEDNESDAY VIDEO: LOVE ME-Dun Shimo

6:42:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
Mkwaju Unafahamika Kwa Jina la LOVE ME kutoka kwa Msanii wa Kanda ya Ziwa (Mwanza & Kahama) DUN SHIMO.

Audio Imekunjwa na Producer H-POL kutoka PANGO RECORDS ya Jijini Mwanza, na Video Imekuwa Directed na KENNY UKIYZ Kutoka Jijini Mwanza Pia

Check It Out

MKWAJU WA SIKU : BADO NIKO NAYE- Lau Wa John

6:27:00 AM Add Comment
   
Na Rich Sam   
WATU WA MUNGU Kutoka Hapa hapa Mwanza, Leo tunakupa "ACCESS" ya kupata na Kusikiliza "Mkwaju Of The Day kutoka kwa Kijana ambaye Jitihada zake zinaonekana sana katika kuusukuma Muziki wake

Anaitwa LAU WA JOHN, na mkwaju wake unaitwa BADO NIKO NAE. Unaweza kuudownload pia kwa ajili ya kumpa Support.

Unaweza kusukuma Track/Audio pia kupitia juti7788@gmail.com ili tuweze kuhusika nao katika Segment Yetu mpya kwa Wasanii mbali mbali "MOTD-Mkwaju Of The Day"

NEW VIDEO: BONTA MAARIFA FT. NIKKI WA II- Beautiful

4:44:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WAUNGWANA, Bonta akiwa na Nikki wa Pill chini ya Mikono ya CHIZZAN, ameamua kushusha Mzigo Mpya Kwenu

Unaitwa Beautiful

PICHA: NYUMBA ALIYOKULIA RAPPER KANYE WEST IMETELEKEZWA NA KUTIA "KINYAA" KIASI HIKI !!!

2:53:00 AM Add Comment

Rich Sam  
WAUNGWANA Nyumba ambayo Rapper Kanye West alikulia tangu utotoni, imetelekezwa na mpaka kufikia Hatua ya Kutia Kinyaa Kiasi Hiki.

Nyumba hiyo ambayo Iko Chicago, awali iliripotiwa kununuliwa na Charity ya Kanye West kwa ajili ya kumbu kumbu ama maalum kwa ajili ya kumuenzi mama yake, lakini cha ajabu ni kwamba haitamaniki na mpaka hivi sasa haijulikani mipango ya kuiboresha itaanza lini

    TIZAMA PICHA    

















MIND YOUR OWN BUSINESS: IRENE UWOYA NA HUDDAH MONROE..... KUNA JAMBO LIMEWAKUTA?

2:27:00 AM Add Comment

Na Insta Cop
WAUNGWANA, leo bwana katika  pita zangu za huku na kule, nikaamua kuingia kwa Irene Uwoya, huyu Bibie hatari pia kwa Bongo Movie, lakini pia amewahi kukunjuka na mastaa tofauti akiwemo H BABA na MSAMI BABY

Ukiachilia mbali Uigizaji wake, pia aliramba Deal na kampuni ya simu ya ITEL ambayo mpaka hivi sasa anafanya nayo kazi kama Balozi wao

sasa Instagram account yake usiku wa Kuamika Leo, ilipostiwa Picha nzuri tu huku ikiwa na Caption tata ambayo inasema "MIND YOUR OWN BUSINESS" yaani Jali Mishe zako... na kauli hii hutolewa mara kwa mara pale ambapo mtu anakuwa ameandamwa sana katika maisha yake ama mishe zake Private

Lakini katika Hali Nyingine pia, Tukakuta neno hilo hilo la "Mind Your Own Business" lipo kwa Socialite kutoka Kenya-HUDDA MONROE ambaye pia ni Ex-wa CMB PREZZO na mshiriki wa BIG BROTHER AFRICA.

Yeye pia aliandika caption kuhusu Kujali mishe zako usiku wa kuamkia Leo, kitu ambacho kimetupa maswali kama Leo ni Siku ya Ku-mind your Own Business au Lah !!

TODAY: WORLD ANIMAL DAY

2:25:00 AM Add Comment

DAYS OF THE YEAR    
While he may be rolling in his grave to discover that he was not the first person to be able to talk to animals, Doctor Doolittle would almost certainly be a keen advocate of World Animal Day which takes place on the Feast of St Francis of Assisi, October 4th. Started in 1931 in Italy, this annual celebration of all things furry is now a popular day in which we remember the important role that animals have to play in our world, as well as the people who devote their lives working to protect and care for them.

To get into the festive mood on October 4th you are encouraged to ditch the fur fabrics, refuse to buy products tested on animals and – probably of greater concern to the majority of folk – convert to vegetarianism. Was St Francis a meat eater? Answers on a postcard…

TCRA : KUNA WATOTO WADOGO AMBAO WANATUMIA MITANDAO YA KIJAMII (VIDEO)

1:59:00 AM Add Comment
 
Na Baba Juti     
KWA mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) kuna baadhi ya watoto wadogo ambao wanatumia mitandao ya Kijamii ingawa Utafiti bado haujabainisha ni idadi Gan  na maeneo Gani Zaidi

Kauli hiyo imetolewa Siku ya Jana Wakati TCRA wakizindua kampeni yao mpya ya Kuwalinda na kutokomeza udhalilishaji wa Watoto wadogo kupitia Mitandao ya Kijamii, iliyopewa jina la C-SEMA

Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma-TCRA, SEMU MWAKYANJALA amesema kuwa, TCRA kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali, inahakikisha kabisa Watoto wadogo hawapati madhara kutokana na huduma za mawasiliano na ndio maana walitoa namba maalumu ya CHILD HELP LINE ambayo ni 116, ili kuhakikisha kama kuna tatizo lolote kuhusu mtoto, basi taarifa itolewe ili kutoa msaada haraka

Naye THELMA DHAJE ambaye ni Meneja wa Simu ya Huduma kwa Watoto ya C-SEMA, amedai kuwa ukuaji wa Utandawazi, umesababisha pia baadhi ya watoto wadogo kutumia mitandao ya Kijamii ingawa hakuna takwimu kamili ambazo zinaonesha kuwa ni Idadi gani ya watoto ambao wanauwezo wa ku-access katika mitandao hiyo ya kijamii.

VIDEO : ALIYEKUWA MAMA MKWE WA RAPPER TYGA ATOA MSAADA WA "SIGARA" KWA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA PUERTO RICO

1:29:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
WAUNGWANA sijui hili tuliweke vipi ama tulitafsiri vipi lakini ni jambo ambalo limetokea na kuchukua Nafasi yake katika Matukio ambayo ni vema pia tukayashusha kwenu

Aliyekuwa Mama Mkwe wa Rapper TYGA, Tokyo Tonny, ambaye pia ni mama Mzazi wa Blacc Chyina, amefanya tukio ambalo limeshtua kidogo baada ya kuamua kutoa msaada wa SIGARA kwa Waathirika wa Kimbunga huko PUERTO RICO

Tukio hilo amelifanya usiku wa kuamkia Leo huko Puerto Rico ambapo alikuwa akizunguka kunako mitaa kadha wa kadha ambayo ilikuwa na Raia ambao wamekosa Makazi yao, yaani wanaolala mitaani, na kuwawekea Pakti za Sigara wakiwa wamelala

Ingawa Wengi wameonekana kumshambulia zaidi katika Suala Hilo huku wakimuambia kwa nini asiwapati japo hata vyakula au mashuka kwa ajili ya kujisadia zaidi katika Tatzio hilo, Bado Mama huyo hajaonekana kuumizwa na maneno hayo na badala yake ameahidi kuendelea kugawa Sigara zaidi.

PICHA: WATU WAKWAZIKA SANA NA KITENDO CHA RAIS TRUMP KUWARUSHIA "TISHU" WAHANGA WA KIMBUNGA KATIKA KISIWA CHA PUERTO RICO (PICHA)

1:02:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
MMOJA kati ya Wawakilishi katika Bunge Nchini Marekani, ameungana na Mchekeshaji kutoka huko Huko Nchini Marekani "kukemea" kitendo cha Rais wao, Donald Trump kurusha "Tishu" ama Paper Towels (Wengine huziita Toilet Papers) kwa waathirika wa Kimbunga kule Puerto Rico.

Mwakilishi huyo LUIS GUTIERREZ, alizungumza kwa Hisia kali hatua ambayo aliifanya Rais Trump kwa Wakazi wa Kisiwa hicho, huku akidai kuwa ni kukidharau na kushindwa kukithamini hasa katika Tatizo kubwa kama hilo ambalo limewaacha wakazi wengi katika wakati Mgumu hasa kukosa Makazi, Chakula, na huduma Nyinginezo Muhimu

Trump alihudhulia Eneo hilo akiwa na Mke Wake Melanie Trump kwa dhumuni la kuwapa Pole, lakini mwisho wa siku aliishia kuzungumza masuala mengi zaidi ya kisiasa na hata kufikia hatua ya Kuwarushia Paper Towers, kitu ambacho hakijawahi kufanywa na Kiongozi yeyote Nchini humo

LUIS alidai kuwa, Kama Trump angepata nafasi ya kwenda Vietnam na kutizama majina ya Wanajeshi na Wengi ambao walikufa huko, angeelewa ni namna Gani Puerto Rico kuna umuhimu na hawahitaji kudharauliwa

Naye Mchekeshaji na muigizaji Mkongwe wa Tangu miaka ya 1990 huko Nchini Marekani, MICHAEL DAVID RAPAPORT alionekana kukwazika sana na kitendo hicho alichokifanya Trump huku akiishia kumtukana kwa maneno makali baada ya kukwazika na Kitendo Hicho.

     NYONGEZA      
Rapper JAY Z alichukua Jukumu la kumsaidia Rapper Fat Joe Ndege ambayo itawasaidia wahanga wa PUERTO RICO kupata Msaada wa aina mbali Mbali. FAT JOE alichukua jukumu la kumshukuru kwa Dhat Jay Z kwa kutoa msaada huo na kufanikisha sehemu ya Msaada.
  
   TIZAMA PICHA NYINGINE ZA DONALD TRUMP     










MNADA BANNER